Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Kichuguu, Mkuu namiliki paso, na safari zangu ni mwanza dar huwa naenda mara kwa mara na paso yangu na huwa siipumnzishi njiani kwa imani kwamba huwa natembea naangalia gauge ya heat.. Naweza kuwa naiumiza gati
Hiyo gari haina shida hata usafiri kila siku na mimi ninayo Passo ndiyo gari yangu ya kwanza mpaka leo ipo yaani ni service tu hata usafiri kila siku ni gari tu kama gari zingine ukiona mtu anaidhararau huyo hana akili kwani zilitengenezwa ili watu waendee sokoni! Huwa nasafiri nayo sana yaani gari inatembea mkoa wowote ule ukipiga service
 
Niambie model ya gari na ni ya mwaka gani, nitakutafutia kwenye Catalog zangu ingawa bado nina imani 99% kuwa ni 10W-30 full synthetic hasa kwa gari inayopiga safari za mara kwa mara.
Yangu ni Toyota Townace van cc 1780, imetengenezwa 2005.
 
Kichuguu, mbona umenisahau mkuu? Nilikuuliza juu ya user manual ya kiingereza ya gari hiyo!
Samahani; model hiyo ya Toyota haipatikini kwenye database zetu za kimarekani. Nadhani magari hayo hayakutengezwa kwa ajili ya soko la Marekani na Canada.
 
Kichuguu ubaeikiwe sana. Na Mungu akuongezee katika kazi yako. Nimefuatilia Hii thread. Naweza sema hii ni thread bora kabisa ya magari jamii forum.
 
Mkuu nina noah voxy engine 1az fse. Inakula mafuta sana na haina nguvu. Kwa kuwa mi ni mgeni wa magari mafundi wamekuwa wakipiga ramli na kuninunulisha vitu vingi vya gharama na shida imeendelea kuwepo.

Fundi wa kwanza aliniambia ni cylinderhead tukafungua engine nzima ikafanyiwa overhaul, kusaga valve na kuosha carbon. Shida ikaendelea kuwa vile vile ulaji wa mafuta, gari haina nguvu, na check engine light inawaka.

Fundi wa pili Nikabadilisha oxygen sensor pia, pump ya mafuta, fuel pressure pump(D4). Tatizo likaendelea vile vile.

Fundi wa tatu tukabadilisha fuel pump ya kwenye tank, fuel pressure pump(D4), Driver injector, Nozzles zote na bomba lake, MAF sensors lakini bado gari haina nguvu na ina misfiring na check engine light inawaka.
Jana nikaita fundi akaifanyia diagnosis na computer ikaleta code P0172 na Code P1349. Naomba msaada wa utatuzi wa tatizo langu. Nianzie wapi ?
 
Attachments

  • IMG_20240913_200633.jpg
    IMG_20240913_200633.jpg
    1.8 MB · Views: 5
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.

Hatutumii ma Fordi na ma Chrysler sisi huku...

Na hata wageni wa USA kutoka Afrika, hawanunui magari ya kimarekani, wanajua mjapani tu!

Come on Diaspora generation, you need to catch up!
 
Pumba tupu
 
Mkuu nina noah voxy engine 1az fse. Inakula mafuta sana na haina nguvu. Kwa kuwa mi ni mgeni wa magari mafundi wamekuwa wakipiga ramli na kuninunulisha vitu vingi vya gharama na shida imeendelea kuwepo.

Fundi wa kwanza aliniambia ni cylinderhead tukafungua engine nzima ikafanyiwa overhaul, kusaga valve na kuosha carbon. Shida ikaendelea kuwa vile vile ulaji wa mafuta, gari haina nguvu, na check engine light inawaka.

Fundi wa pili Nikabadilisha oxygen sensor pia, pump ya mafuta, fuel pressure pump(D4). Tatizo likaendelea vile vile.

Fundi wa tatu tukabadilisha fuel pump ya kwenye tank, fuel pressure pump(D4), Driver injector, Nozzles zote na bomba lake, MAF sensors lakini bado gari haina nguvu na ina misfiring na check engine light inawaka.
Jana nikaita fundi akaifanyia diagnosis na computer ikaleta code P0172 na Code P1349. Naomba msaada wa utatuzi wa tatizo langu. Nianzie wapi ?
Fundi aliyefanya overhaul ya injini yako huenda ndiye aliyeiharibu zaidi.

Kwa vile ulishabadilisha Oxygen senor na fuel pump na bado tatizo liko pale pale, ninakushauri pia ubadilishe MAF sensor ( Mass Air Flow Sensor) ili kuondoa hiyo code P0172. Halafu pia huenda fuel pressure regulator yako imeshachoka na hivyo kushindwa ku-controll kiasi cha mafuta yanayokwenda kwenye injini na kuruhuru mafuta mengi yaende. Kama fundi wako anaweza kutest fuel pressure regulator, huenda hiyo ndiyo chanzo cha matatizo yako yote. Magari mengi ya siku hizi fuel pressure inakuwa regulated electronically kwenye fuel pump, lakini kama gari yako ina umri mkubwa kidogo basi huenda inatumia vacuum fuel pressure regulator ambazo huchoka baada ya kufikia umri fulani, inabidi uibadilishe.

Mambo mengine ya kuangalia ni adjustment ya breki zako. Hilo ni jambo dogo sana lakini iwapo breki zinabana utashangaa gari inakosa nguvu na kula mafuta sana. Mafundi wasiokuwa makini hukimbilia kwenye injini badala ya kuanza kukagua breki na parking brake. Kagua jambo hilo.

Kuhusu code ya P1349 hiyo husababishwa na mambo mengi sana. La kwanza kabisa ni oil kuwa chafu au oil filter siyo nzuri. Kama Oil ni safi na oil filter ilibadilishwa wakati wa kubadili oil basi kosa linamrudia tena fundi aliyekufanyia overhaul kwani huenda alivuruga timing au alichafua valve lifters au hakufanya adjustement ya tappets vizuri.
 
Mass flow sensor nilibadilisha pia
 
Hiyo fuel pressure regulator kwenye 1az fse ndio ikoje?? Maana nikimtajia fundi anaweza asijue

Nachokumbuka Nilibadilisha hii kwenye picha, sasa sijui ndio fuel pressure regulator???
s-l1200.jpg
 
Na kabla ya oberhaul gari ilikuwa na shida hiyo hiyo. Kunywa mafuta sana na kukosa nguvu. Fundi akashauri overhaul. Na baada ya overhaul shida ikaendelea. Nikabadilisha hiyo kwenye picha hapo juu. Fuel pressure pump, Oxygen sensor, MAF sensor, nozzle na bado shida imeendelea. Break pia zimelegezwa. Taa ya check engine inaendelea kuwaka na imetupa code P0172 na P1349.
 
kama uko Tanzania, wewe nitumie message hapa inbox tu. Auto repair shop yangu ya mtaani iko Marekani, halafu ninafanya kazi nyingine ya kufundisha.
Hongera sana Braza. Watz wenzangu tujifunze mnaona wanaoishi Marekani walivyo na upendo?
 
Hiyo fuel pressure regulator kwenye 1az fse ndio ikoje?? Maana nikimtajia fundi anaweza asijue

Nachokumbuka Nilibadilisha hii kwenye picha, sasa sijui ndio fuel pressure regulator???
View attachment 3096085
Nadhani hiyo ni fuel pump ya Toyota; hiyo haina fuel pressure regulator. ngoja kesho nitakuangalilia kujua fuel pressure regulator inaeyoendana na fuel pump hiyo. Nimechukua namba zake.
 
Marekani hakuna Run X, Kichuguu anaijulia wapi RunX 1.5 ?????

Uninformed, naive, audience base

hahahahahaa......
Toyota Corolla Runx 1.5i zilikuwapo marekani pia ila hazikuwa maarufu sana na nadhani model ya mwisho ilikuwa ya mwaka 2006
 
Professor kichuguu, hongera mingi sana kwako, na Mungu akubariki, ninaomba msaada gari yangu ni runx 1.5 ikifika spid 40 mlio unabadilika japo ni nyepesi na Ina nguvu,msaada pliz
swali lako haliko kamili kwa vile hukusema mlio unabadilikaje. Jibu la haraka haraka ni huenda transmission yako ina matatizo. Ila jibu kamil linahitaji information zaidi kuhusu tatizo la gari
 
2AZ engine inayofungwa kwenye Alphard, RAV4 miss Tanzania, Vanguard na Klugger Ina matatizo gani hasa zile zilizotokea kabla ya 2007?
 
Na kabla ya oberhaul gari ilikuwa na shida hiyo hiyo. Kunywa mafuta sana na kukosa nguvu. Fundi akashauri overhaul. Na baada ya overhaul shida ikaendelea. Nikabadilisha hiyo kwenye picha hapo juu. Fuel pressure pump, Oxygen sensor, MAF sensor, nozzle na bado shida imeendelea. Break pia zimelegezwa. Taa ya check engine inaendelea kuwaka na imetupa code P0172 na P1349.
Je wakati wa kuoverhaul engine hiyo walibadilisha spark plugs na injectors zote? Na kama walibadilisha injectors, je walihakikisha kuwa pressure ye injectors hizo inaendana na pressure y a mafuta kutoka kwenye fuel pressure regulator?

Nina wasiwasi kuwa wakati wa overahul parts uzilzowekewa ni zile aftermarekt au OEM ambazo hazina ubora unaotakiwa kiasi kuwa fundi alitakiwa aweke ujuzi zaidi kufanya injini izikubali.

Mimi kama fundi huwa napinga sana kukimbilia kufanya overhaul Ile inatakiwa ifanyike tu iwapo injini imenoki
 
Thanks...
MREJESHO fundi alibadilisha vacuum sensor gari ikapona. Nguvu imerejea na sasa inakula mafuta vizuri. Imebaki code ya vvti valve najipanga nibadilishe vvti maana kuna mlio unasikika kama rattling au knoking sound fundi akasema ni vvti na ndio faults code iliyobakia.

Faults code ya rich fuel imeondoka baada ya kubadilisha vacuum sensor Zote
 
Back
Top Bottom