Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu, gari langu Vitz old model, inagoma kurudi reverse, msaada wako pls
 
Mkuu, gari langu Vitz old model, inagoma kurudi reverse, msaada wako pls
Hiyo inaweza kusababishwa na mambo mengi, mengine yakiwa ni mazito zaidi ya mengine.
Yale mepesi ni pamoja na mafuta (ATF) kupungua, mafuta kuchafuka kupita kiasi, transmission position sensor kuharibika. hayo hayahitaji Transmission kuwa overhauled. Yale mazito ni pamoja na meno ya gear kusagika, kuharibika kwa valve, kuhalibika kwa solenoids; haya yanahitaji transmission itelemshwe chini ifanyiwe overhaul. Kama taa ya check engine inawaka, peleka kwenye computer wakuambie tatizo ni lipi.
 
Shukrani sana, nimepata mwanga wapi a kuanzia. Ubarikiwe.
 
NAOMBA KUFAHAMU ENGINE OIL YA KILOMETA 5000 AU 9000 NAWEZA KUIJUAJE NA WAPI WAMEANDIKA HAYO MAELEZO MAANA NIMESHA TUMBUA MACHO KWENYE MAELEZO YA KWENYE GARONI LAKIN SIJAONA
 
NAOMBA KUFAHAMU ENGINE OIL YA KILOMETA 5000 AU 9000 NAWEZA KUIJUAJE NA WAPI WAMEANDIKA HAYO MAELEZO MAANA NIMESHA TUMBUA MACHO KWENYE MAELEZO YA KWENYE GARONI LAKIN SIJAONA
Usije kaa na oil km 9000 utaua injini yako, oil ina provide lubrication pale injini inapokua on,, so whether gari inatembea au imesimama ili mradi injini ipo on basi oil inafanya kazi yako.. so ukiwa mtu unae angalia kilometers kubadili oil utakuja kuchuma janga. Pia kama gari inachangamoto ya kula oil kufika km9000 utakuta either oil imeisha au ipo chache..yet mazingira ya tropical ni too hot so oil inawahi kuchoka.. so hapa risk ya kuua injini ni kubwa. So be careful..mbaya zaidi oil unazo zitaja hapa ni mineral oil not synthetic oil. Change oil after every 3000 to 4000km.
 
Soma kwanza kitabu cha gari yako, kuna injini nyingi zinataka 5W-30 na 5W-20. Hata hivyo kwa Dar es Salaam ambayo ni sehemu yenye joto sana, unaweza kutumia 10W-30 au 10W-20.
Mimi huwa natumia 20w 50 kwenye starlet yenye engine ya 4e iyo ikoje kwenye swala la ubora?
 
Mimi huwa natumia 20w 50 kwenye starlet yenye engine ya 4e iyo ikoje kwenye swala la ubora?
hiyo oil ni nzito sana kwa gari ndogo kama hiyo, hata kama ina umri mkubwa sana.
 
hiyo oil ni nzito sana kwa gari ndogo kama hiyo, hata kama ina umri mkubwa sana.
Mkuu, bongo kitu kinaitwa oil viscosity wengi wazangatii, mtu anaweka brand name-utasikia naomba oil ya total au bp ila ukimuuliza viscosity gani inakua majanga... Ukimpa 20w-50 twende kazi, ukimpa mono grade ya SAE40 ili mradi tu ni brand anayoikubali anaweka kwenye gari, kumbe mdogo mdogo gari inakufa bila ya yeye kujua.
 
hiyo oil ni nzito sana kwa gari ndogo kama hiyo, hata kama ina umri mkubwa sana.
Duh kwaiyo mtaalam unashaurije maana nimeweka Sina hata siku 3,,madhara yake hasa kwa ingini ni yapi?
 
engine yenye ukubwa 6400 cc kwa km 1 itatumia litre ngapi?!!
Ni ya dizeli au petroli? Naturally aspirated, turbocharged, biturbo, supercharged? Ni V8, V10, V12, W12, straight 6, 8, 4 au 5? Inaendesha gari gani, na inaendeshwa kwenye mazingira gani? Mzigo unaobebwa ni kiasi gani?
 
Baada ya kuipeleka kufana service kigari changu Vitz kinatoa mlio Kama Mashine , shida Ni Nini mkuu?
 
Maji kuisha kwenye rejeta gari vitz 2sz kila siku nikitoka najaza maji nikijisahau tu gari inachemka na kuzima. Tatizo nini?
 
Maji kuisha kwenye rejeta gari vitz 2sz kila siku nikitoka najaza maji nikijisahau tu gari inachemka na kuzima. Tatizo nini?
Inategemea na mambo kadhaa. Je gari inatoa moshi mweupe? Je ukifungua mfuniko wa oil unakuta una maziwa maziwa? Ukiona mambo hayo basi ujue ama cylider head gasket imchoka au engine block ina ufa. Vinginevyo, inawezekana coolant inavuja kutokana na water pump kuchoka, au radiator imetoboka ay bomba la coolant lina tundu. Kama coolant inavuja, utagundua kwa kuwa unakuta maji chini ya sehemu uliyopaki.
 
Kuongezea tu au radiator cap ina vujisha maji pale pressure inapokua juu ndan ya cooling system.. so acheki pia kama mfuniko wa radiator upo sawa au lah
 
Kuongezea tu au radiator cap ina vujisha maji pale pressure inapokua juu ndan ya cooling system.. so acheki pia kama mfuniko wa radiator upo sawa au lah
Uko sawa ndugu ni ufuniko wa rejeta ulikua unavujisha. Nimebadili gari iko poa thoo nimechelewa kugundua tatizo imepelekea kuharibu cylinder head kwa mujibu wa fundi.

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Gari nissan qashqai inachelewa kuchanganya. Pia imekua nzito. Nimefanya diagnosis hakuna kinachoonekana. Oil iliyotumika ni 5w30 na ni service ya pili... Gear box oil haijawahi kubadilishwa...

Gari imekua nzito mno...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…