Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
Pole sana ndugu yangu; kadhia uliyopata inaweza kutokanana na moja ya sababu tano kuu au zote kwa pamoja kama ifuatavyo, yaani sababu moja ikisababisha nyingine.Mkuu Kichuguu na mimi leo nina jambo geni kidogo nimeliona linanitokea kwenye gari....
Gari linaendesheka Vizuri kama kawaida ila nikiwasha AC gari linapungua nguvu sana....nikizima tu AC, hapo hapo unasikia gari linakuwa lepesi sana na linachanganya faster...
Ni ishu mpya kabisa kuwahi kunitokea...
Shida yaweza kuwa ni nini..?
Gari Nissan Note 2005, HR15 Engine, CVT gear box....
Valve guides ndo valve seal mkuuJina langu siyo Kitunguu aisee, hebu badilisha; mimi ni Kichuguu, ".....huwezi kulinganisha Kichuguu na mlima Kilimanjaro"
Bila shaka gari yako huwa inatoa moshi mwingi sana, yaani kuna oil inavuja na kuingia kwenye combustion chamber na kuunguzwa pamoja na mafuta. Iwapo injini yako ina nguvu kama kawaida, basi kuna vipete fulani ambamo valve stem hupita (vinaitwa valve guides) huenda vimepanuka sana na kuacha mwanya wa oil kupenya ndani ya injini. Fundi wako akifungua cylinder head cover anaweza kuvikagua na kuona kama vimepanuka. Ni rahisi kuvibadilisha kwani viko kwenye cylinder head, ila utahitaji cylinder head gasket mpya.
Kama Injini haina nguvu kama zamani na vile vile inakula mafuta mengi sana basi huenda piston rings zako zimekwisha; hapo utahitaji kazi kubwa kidogo ya karibu na overhaul kwani itabidi ufungue injini yote kuweka piston rings mpya. Usifanye makosa ukabadilisha piston kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kazi ya namna hiyo fundi anaweza kuifanya kikamilifu bila kuangusha injini kabisa; utahitaji cylinder head gasket mpya pia.
Piston rings hufa iwapo hubadilishi air filter yako mapema kwani huruhusu vumbi (ambalo ni silica na ni ngumu kama msasa) kuingia ndani ya cylinder na kusaga hizo piston rings na vile vile iwapo hubadilishi engine oil katika muda unaotakiwa.
Ndiyo
Injini kuzimika wakati wa idling kunasababishwa na sababu nyingi sana ndogo ndogo ambazo hazina madhara kabisa kwenye injini yako. Ngoja nitaje ambazo ni za kawaida sana.
(1) Inawezekana air filter yako imeshajaa uchafu; iangalie na ukiweza uibadilishe.
(2) Inawezekan air flow sensor imeshachafuka au imekufa. Air flow sensor ni kiwaya chembamba sana kinachoweza kukatika hasa iwapo air filter ni chafu. Kama imechafuka, kuna mafuta ya kuisafishia, na kama imekufa unaweza kubadilisha na kuweka nyingine. Zinagharimu kati ya dola mbili hadi kumi na tano tu.
(3) Inawezekana injector zako zina uchafu, kwa hiyo hazipitishi mafuta wakati pressure ni ndogo. Kama tatizo ni hili, kuna injector cleaners ambazo unaweza kuongeza kichupa kimoja kwe tanki la mafuta likiwa full tank kukusafishia injector hizo.
(4) Inawezekana throttle position sensors kwa upande wa chini haifanyi kazi, kwa hiyo ukiachia accelerator basi computer inakuwa haipati taarifa za position ya accelerator yako kwa hiyo inashindwa kujua ni kiasi gani cha mafuta kinahitajiwa na hivyo inaamua kukata mafuta kabisa. TPS zinazuwa kati ya dola tatu hadi 15 tu.
(5) Inawezekan fuel pressure regulator imeshachoka kwa hiyo inavujisha mafuta kurudi kwenye tank wakati pressure ni ndogo na kuiacha injini na ukame wa mafuta. Hii ikitokea, gari inaaza kupungukiwa na spidi hata ikiwa katika mwendo wa barabarani wa kawaida, kwa hiyo iwapo ukiwa barabarani hunaoni tatizo lolote basi ni wazi hili siyo tatizo ulilo nalo.
Sababu namba (2) hadi namba (4) zikitokea, ni lazima zitaregister kwenye computer ya gari na utapata checki engine light. Kama inakuonesha check engine light, ipeleke kwenye computer scan ujue ni sensor gani. Kama hakuna check engine light, basi kwa asilimia kubwa ni kwa air filter yako imechoka sana.
Weka kwenye tanki la mafuta; chupa moja ya STP kwa full tank ya petroli; inasafisha hizo injectors kwa kwa kama wiki nzima hivi kulingana na unedeshaji wako.Samahani mkuu STP unaweka kwenye tank la petrol au ni unapoweka engine oil mkuu
Hizo valve seals zikiharibika, basi oil inakuwa inaingia ndani ya coimbustion chamber na kuchomwa, utakuwa unapata moshi mweupe hivi kwenye exahust. Ila sasa kama injini inachafuka kwa oil, basi itakuwa ni cylinder head cover gasket ndiyo mbovu. siyo hizo valve guides (kwa jina jingine valve seals). Test mojawapo rahisi sana ya kuona kama oil inaingia kwenye combustion chamber ni hivi. Washa gari, halafu weka chukua kipande cha pamba au toilet paper, weka pale kwenye exhaust kama dakika kumi hivi. Kikishika masizi meusi utakayoweza kuona kirahisi kwa macho yako katika muda huo mfupi, basi ni dalili kubwa kuwa valve guides zimepanuka. Daima kutakuwa na masizi kidogo sana lakini siyo mengi ya kuona mpaka yanatia weusi.Carina yangu inachafua engine, nikiiosha leo engine baada ya3-4wks,nakuta engine imechafuka na oil imekua nyeusi, fundi akanishauri nibadilishe valve seal
Ndiyo; AC inaendeshwa na injini na inahitaji nguvu sana, ndiyo maana ukiwasha AC lazima muunguruma wa gari ubadilike kidogo kwa vile inaaza kunywa mafuta mengiNi kweli kamba matumizi ya AC yanaongeza ulaji wa mafuta kwenye gari...??
Siyo kweli. Mafuta yakiungua ndani ya injini hutoa Carbon Dioxide na maji katika hali ya mvuke. Wakati gari linawashwa asubuhi lingali la baridi, mvuke huo uifika kwenye exahust huganda na kuwa maji ambayo ndiyo yanayodondoka kutoka kwenye Exhaust. Hiyo itatokea kwa injini yoyote iwe ina matatizo au haina matatzio mradi tu imewaka. Exhaust ikishakuwa ya moto, basi mvuke ule hauwezi kuganda tena na hivyo huwezi kuona maji yakitoka. Ila sasa iwapo gari linatoa maji kwenye exhaust muda wote hata pale ambapo exhaust imeshakuwa ya moto basi ujue kuwa injini ina matatizo makubwa. Ama cylinder head gasket imekufa au engine block ina ufa, kwa hiyo maji ya radiator yanapita moja kwa moja hadi kwenye exahust, na unaweza kuanza kuona kuwa injini inakausha maji mara kwa mara.Kuna mafundi wanasema ukiwasha gari alafu ukienda kuangalia kwenye exhaust ukikuta inatoa maji basi ujue engine ya gari ni nzima sana(kinanda) mpyaaaaa ??
Inazuia gari isteleze ukikamata breki ya ghafla. kwenye barabara yenye utelezi ABS huwa inastabilize gari barabarani lakini unaweza kugonja kitu kilicho mbele yako kwa vile gali litaendelea bila kukwaruza barabara mpaka itakaposimama yenyewe. Ukiwa na ABS jiachunge uwe unaendesha kwa makini, breki za ghafla hazifanyi kaziNaomba kujua kazi ya ABS kwenye gari ?
Fuata maelekzo ya mtengezaji (manufacturer)Tyre za gari inatakiwa ubadirishe kwa muda gani,na zinafungwaje mana nimewai kuskia fundi anasema gari haikimbii sana hizo tyre zimegeuzwa kashata sijui
Kuna mwana specs za gari zinataka 5w-30 yeye akang'ang'ania hio SAE40 kisa ni bei rahisi(kuna sehemu lita 4 wanauza Tsh.28,000) wkt 5w-30 lita 4 nanunua Tsh.80,000,aisee gari yake hua inaunguruma kama tractor/matatizo kwny gari yake ni kila mara imebidi juzi hapa aweke engine nyingine.
Huu uzi umenipa msononeko kidogo sina gari wala pikipiki,lakini nimejifunza mambo makubwa anyway..
Kuna gari ni automatic transmission ila navyoiendesha sasa kama manual transmission..
Iko hivi
Uki start engine inawaka vizuri ukiweka gear D au L au R inazima sasa nikitaka isizime nashika break.
Navyotaka kuondoka nakanyaga pedal ya mafuta na break kwa wakati mmoja alafu naachia break taratibu gari ndio inakubali kuondoka,nikitembea kidogo inaanza kusinzia nakanyaga break tena hapa inasimama kabisa nakanyaga mafuta mengi huku nimeshika break naachia break taratibu gari inaondoka..
Sijawai kuiendesha kwenye foleni mana ningekua na case ya kugonga gari za watu..
Kuna fundi pump ya kuvuta mafuta ipo mbele kwenye engine imekufa,manake hii gari ina pump kwenye tank na myingine ipo mbele kwenye engine
Mwingine akasema computer inatatizo inashindwa kichambua nini sijui
Mwingine akasema tuliweka mafuta machafu,
Engine ya gari ni D4 inatoa moshi kuna muda ukikanyaga mafuta sana wakati umesimama unakuta nyuma kwenye exhaust imemwaga kama unga mweusi hivi chini
5w30 ni 56000 pale total mcity boss tena og from france.. hio 80000 itakua castrol ndio wana bei za ajabu za oil nahisi sababu ni brand kubwa wamejitangaza sana..
5w30 ni 56000 pale total mcity boss tena og from france.. hio 80000 itakua castrol ndio wana bei za ajabu za oil nahisi sababu ni brand kubwa wamejitangaza sana..
Thnxs mkuu,natumia castrol na niko huku mkoani so kidogo gharama zinakua juu kidogo lkn juna sehemu 5w-30 ya total nimeona wanauza Tsh 60,000 ila sijawahi kuitumia mkuu.
Gari yoyote ya Automatic ukiwasha lazima uwe umebonyeza brake ama sivyo haliwezi kuwaka. Brake ile pia hufanya kazi kama clutch, kutenganisha injini na gearbox.
Wakiuza 60000/- hiyo total siyo mbaya inategemea unaishi wapi coz maeneo mengi inaanzia 55000/
Mimi naitumia na ninaona mashine ya gari inafanya kaxi vizuri....injini inakuwa nyepesi vizuri
Gari yoyote ya Automatic ukiwasha lazima uwe umebonyeza brake ama sivyo haliwezi kuwaka. Brake ile pia hufanya kazi kama clutch, kutenganisha injini na gearbox.
Ni kweli; magari mengi ya zamani yalikuwa hayana tatizo la kukanyaga brake kabla ya kustart, yalikuwa yanakubali tu iwapo upo kweny parking position. Lakini magari ya siku hizi nadhani baada ya 2005 au 2006, hayakubali kustart iwapo hutabonyeza breki; vile vile huwezi kuzima gari na kuondoa ufunguo kabla ya kuliweka kwenye parking position wakati magari ya zamani yalikuwa yanaruhusu tu.Kaka mbona huwa nawasha bila kukanyaga brake na linawaka hapa imekaaje?