Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

kimaus

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
582
Reaction score
707
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
 
Kuna ukweli kwamba nyuki aki sting anakufa?
 
Kwanini nyuki huwa wanaranda randa juu ya mzinga?haswa mida ya mchana
 
Kuna aina ngapi ya nyuki?species?
Kuna species nyingi sana za nyuki, lakini kwa hapa Tanzania tuna species kuu moja yenye sub species 3.
Sisi tuna Apis mellifera.
Wana sub species 3,
Apis mellifera scutellata hawa wanapatikana ukanda wa tambarate kama katikati mwa nchi;
Apis mellifera litorrea hawa wanapatikana ukanda wa pwani na
Apis mellifera monticola hawa wanapatikana ukanda wa milimani.
 
Ni ingredients zipi nyuki anatumia kufanikisha kutengeza asali alafu etii ni kweli asali hata ikae miaka elfu moja haiharibiki? Kama ni kweli je ni kwanini.
 
Nini tofauti ya asali ya nyuki wadogo na ile ya nyuki wakubwa?(nutrition value). Kwanini asali ya nyuki wadogo inauzwa bei kubwa kulinganisha na ya nyuki wakubwa?
Asali ya Nyuki wadogo (stingless bees honey) ni Asali nyepesi na ina virutubisho vingi na ina anti-oxidants nyingi. Ndio maana pamoja na wepesi wake (maana ina maji mengi kuliko ya nyuki wakubwa) bado hai ferment. So hizi anti-oxidants ndio zinaifanya kuwa bora na kuwa medicinal, na hivyo kuwa ghali. Sio kwamba asali ya nyuki wadogo sio dawa, la hasha, ila ya nyuki wadogo ina anti-oxidants nyingi kuliko ya nyuki wakubwa japo zote zina hizo anti-oxidants
 
Asali ya Nyuki wadogo (stingless bees honey) ni Asali nyepesi na ina virutubisho vingi na ina anti-oxidants nyingi. Ndio maana pamoja na wepesi wake (maana ina maji mengi kuliko ya nyuki wakubwa) bado hai ferment. So hizi anti-oxidants ndio zinaifanya kuwa bora na kuwa medicinal, na hivyo kuwa ghali. Sio kwamba asali ya nyuki wadogo sio dawa, la hasha, ila ya nyuki wadogo ina anti-oxidants nyingi kuliko ya nyuki wakubwa japo zote zina hizo anti-oxidants
Kuna aina ngapi za stingless bees?
 
Mi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
Kwànini nyuki hapotei kwenye mzinha wake hata akienda mbali hapotei, je Wana gps?
 
Ni ingredients zipi nyuki anatumia kufanikisha kutengeza asali alafu etii ni kweli asali hata ikae miaka elfu moja haiharibiki? Kama ni kweli je ni kwanini.
Nyuki anakwenda kuchukua maji matamu ya maua (nectar) tunaita mbochi kwa kiswahili, anarudi kwenye sega (comb) ana regurgitate yale maji pamoja na ingredients zingine kutoka kwenye mwili wake. Hapo bado inakuwa haijawa Asali, kwa sababu ina maji mengi sana yaani nyepesi, so wakishajaza vyumba vyote hiyo nectar, wanapiga mbawa zao kwa wingi wao wana create upepo mkubwa ndani ya mzinga kiasi kwamba maji yana evaporate na kuifanya ile necta kuwa nzito zaidi, wanaendelea mpaka wakijiridhisha ipo tayari (yaani maji yawe less than 21 %) kwenye Asali ndio wanaifunga na kuihifadhi ambapo sisi tunaenda kuwa rob.
 
Kwanini nyuki wakiwa porini huko au kwenye mzinga wanakuwa wakali lakini akiwa maeneo ya karibu na binadamu mfano kwenye mashine za kusaga nafaka huwa ni wapole?
Nyuki anakuwa mkali akiwa ana defend mzinga wake unapokuwa na watoto (brood) au Asali. Ukienda pale unapigwa.
Lakini nyuki akija ku forage (kutafuta chakula) attention yake kubwa ni chakula so hawezi kukudhuru. Ndio maana ukijipaka Asali nyuki wakaja kwa kufuata Asali wanakutua wanakula asali bila ya kukudunga, ila usimbane au kumpiga, tulia tu, atakula aondoke. So mashine nyuki wanafuata unga kwa ajili ya kutengenezea bee bread, kama wanavgobeba pollen kutoka kwenye maua.
 
Kama nyuki wanaweza kutengeneza asali locally, actually niku_Assemble. Maana nyuki hukusanya necta za maua mbalimbali.
Je sisi binaadamu na teknolojia yetu kuubwa tuliyonayo Je kwanini tusiweze kutengeneza asali yetu??kama vile vile nyuki wafanyavyo.
Kama jibu ni haiwezekan basi ningependa kujua Why?
Na kama jibu ni ndio tunaweza basi ningependa kujua How???
 
Back
Top Bottom