Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Je? Ubora wa Asali unategemeana na mabadiliko ya hali ya hewa?

Kwanini kuna asali mbichi na isiyo mbichi? Nini sababu za kuipika? Ipi ina ubora zaidi?
 
Kama nyuki wanaweza kutengeneza asali locally, actually niku_Assemble. Maana nyuki hukusanya necta za maua mbalimbali.
Je sisi binaadamu na teknolojia yetu kuubwa tuliyonayo Je kwanini tusiweze kutengeneza asali yetu??kama vile vile nyuki wafanyavyo.
Kama jibu ni haiwezekan basi ningependa kujua Why?
Na kama jibu ni ndio tunaweza basi ningependa kujua How???
Wanapochukua Nectar wanapoitema kuna ingredients zingine zinatoka mwilini mwao, that's why we can not synthesize honey with similar composition kama natural honey, itaharibika mapema tu!
 
Ni kweli, maana ile mshale wake (sting apparatus) imeungana na utumbo, so mkuki ukiingia kwenye mwili wako hauwezi kutoka bali yeye anafumuka nyuma utumbo unakatika. Atakufa tu. So please dont get stung by bees, utatumalizia nyuki wetu.
Duuh!
 
Ni muda gani(season) ambao nyuki hutengeneza asali ie kiangazi/masika au ni muda wowote wao hutengeneza tu asali?
Nyuki anatengeneza Asali kukiwa na maua ya kutosha, sasa kwa kuwa kila nchi vegetation zake zina misimu ya miti kutoa maua ndio maana tunapata misimu ya uvunaji. Lkn kama maua yapo nyuki wanatengeneza Asali all year round. Mind you, pia kama maua ni mengi mno nyuki hawahifadhi Asali ya kutosha kwa kuwa wanajua hakutakuwa na ukame hivyo they can have food anytime. Ni disadvantage kwa mfugaji.
 
Ni ingredients zipi nyuki anatumia kufanikisha kutengeza asali alafu etii ni kweli asali hata ikae miaka elfu moja haiharibiki? Kama ni kweli je ni kwanini.
Asali ikitunzwa vizuri inakaa hata miaka 10 na bado inaweza kuliwa japo ubora kama harufu itapungua. For this reason, ndio maana tunasema honey does not expire. Ukiwa unapack asali never write expiry date, badala yake weka BEST BEFORE, three years after harvest. Baada ya miaka mitatu Asali inaanza kupunguza ubora hasa inapotunzwa vibaya
 
Nyuki anatengeneza Asali kukiwa na maua ya kutosha, sasa kwa kuwa kila nchi vegetation zake zina misimu ya miti kutoa maua ndio maana tunapata misimu ya uvunaji. Lkn kama maua yapo nyuki wanatengeneza Asali all year round. Mind you, pia kama maua ni mengi mno nyuki hawahifadhi Asali ya kutosha kwa kuwa wanajua hakutakuwa na ukame hivyo they can have food anytime. Ni disadvantage kwa mfugaji.
Okey asante.

Ningependa kujua mgawanyo wa kazi wa nyuki wanapokuwa kwenye makazi yao(mzinga).

Pia nilisikia nyuki dume hatokani na fertilization kati ya sperm na ovum hii imekaaje?
 
Je? Ubora wa Asali unategemeana na mabadiliko ya hali ya hewa?

Kwanini kuna asali mbichi na isiyo mbichi? Nini sababu za kuipika? Ipi ina ubora zaidi?
Ubora wa Asali hautegemei mabadiliko ya hali ya hewa, bali Asali inaweza kuharibika ubora kwa mishandling wakati wa kuvuna, kukamua, kuchuja au kupack. Tunaita adulteration.
Kuhusu neno Asali mbichi, hili ni neno la Lay people. Asali haipaswi kuchemshwa.

Sasa kwa kuwa kuna watu (out of ignorance) wanachemsha Asali ili eti iwe nyepesi wapati nyingi ndio maana isiyochemshwa inaitwa mbichi. Lkn Asali inapaswa kuitwa "Asali asilia" ( Natural honey)
 
Uko vizuri mtaalamu, kuna maneno mtaani tangu tukiwa wadogo kwamba nyuki wanaua hata ng'ombe, kwamba wana sumu? Na km wana sumu kwanini isiwepo kwenye asali?
 
Kuna kitu huwa najiuliza, ukitaka kufuga nyuki unaanzaje?

Kuna mtu kanambia we unatundika tu masega yako watakuja wenyewe. Sasa kama eneo nlilokuwepo hakuna nyuki watatokea wapi?
 
Okey asante.

Ningependa kujua mgawanyo wa kazi wa nyuki wanapokuwa kwenye makazi yao(mzinga).

Pia nilisikia nyuki dume hatokani na fertilization kati ya sperm na ovum hii imekaaje?
Ni nyuki jike au kibarua (worker) ndiye hatokani na fertilization. (Parthenogenesis).
Kwenye mzinga kunakuwa na aina 3 za nyuki. Malkia mmoja tu kundi zima, madume machache tu say in tens or hundreds na workers ndio wengi. Kwenye kundi la say 100k bees, madume yanaweza kuwa 2000 na workers 98k. Malkia anataga mayai yote kwenye mzinga, madume hayana kazi zaidi ya kumpanda malkia tena anafanikiwa mmoja tu, kazi zingine zote zinafanywa na workers, kuanzia kutafta chakula, kulisha watoto, kusafisha mzinga, kumlinda malkia, kutengeneza Asali na kulinda mzinga.
 
Ubora wa Asali hautegemei mabadiliko ya hali ya hewa, bali Asali inaweza kuharibika ubora kwa mishandling wakati wa kuvuna, kukamua, kuchuja au kupack. Tunaita adulteration.
Kuhusu neno Asali mbichi, hili ni neno la Lay people. Asali haipaswi kuchemshwa. Sasa kwa kuwa kuna watu (out of ignorance) wanachemsha Asali ili eti iwe nyepesi wapati nyingi ndio maana isiyochemshwa inaitwa mbichi. Lkn Asali inapaswa kuitwa "Asali asilia" ( Natural honey)
Asante...
 
Uko vizuri mtaalamu, kuna maneno mtaani tangu tukiwa wadogo kwamba nyuki wanaua hata ng'ombe, kwamba wana sumu? Na km wana sumu kwanini isiwepo kwenye asali?
Ni kweli nyuki wanaweza kuua hata Tembo binadamu, ng'ombe n.k.
Sumu ipo kwenye rear (nyuma) na ipo kwenye organs maalumu kwa ajili ya defense.
Asali inatemwa mdomoni baada ya maji (nectar) kutoka kwenye maua, so haviingiliani.
 
Back
Top Bottom