Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Mkuu utajuaje kama hii asali nzuri? Huku mitaani wengi wao wanauza asali feki imejaa sukari guru

Naongezea, mtu anayetaka kununua asali atajuaje haijaongezwa kitu chochote?
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
Mimi nina maswali mengi kuhusu hivi vitu lakini najua pamoja na kujisifu hapa na nia yako nzuri mambo mengi huyajui kuhusu nyuki na hutaweza kunijibu.Unayoyajua ni machache kuliko usiyoyajua.Afadhali umesema utajibu kadri ya uwezo wako hivyo nikiuliza na ukashindwa omba msaada kwa wengine.
 
Mpaka nimetamani kujua namna anavowaeleza wenzake.... Mungu ni waajabu sana
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
unaweza kupata asali mara ngapi kwa mwaka kwenye mizinga?
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
nahitaji nionane nawe unipe somo refu sana kwani nataka nianze kufuga asali mwezi wa saba pls nahitaji sana somo hili nimekufuatilia hapa nimeona huu mwalimu mzuri
 
Nina mizinga miwili, ni dalili zipi nikiziona ili nijue kuwa wana asali na naweza kulina?

Nawezaje kuhamisha nyuki/njia ya kuwahamisha walioweka mzinga wao karibu na makazi bila kuwadhuru?
 
Nishawahi kusikia asali inaweza kukuondolea Uhai endapo utaichanganya au utaila baada ya kula;
1. Tango
2. Chungwa
3. Wali
Ni kweli??
 
Mpaka nimetamani kujua namna anavowaeleza wenzake.... Mungu ni waajabu sana
Siasa kidogo...
Usiseme mungu wa ajabu sana (kwakuwa inakuwa kama amejidhihirisha mbele ya macho yako)

Badala yake
Sema mungu ana maajabu sana (kwakuwa ameyadhihirisha na unayashuhudia)
 
1. Ni kweli nyuki ana viini 600 vya macho? (Kama jibu ndiyo tuchambulie kila kimoja)

2.Madume mengine yanaponea wapi kuhusu sex maana mnatuambia madume ni mengi lakini anayempanda malkia ni dume mmoja tu wakati huohuo yale majike mengine (workers) yenyewe ni kazi tu hakuna sex
 
Je swala la kuwa asali inaongeza nguvu za kiume ni kweli au maneno ya mtaani tu??
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!

Nyuki wanapoingia kwenye mzinga au kufika popote kuweka makazi yao, inachukua muda gani kuwa na asali tayari kwa kuvuna? Kuna nyuki wameingia kwenye jengo langu nimeishia kupaua tu tena hata kofia sijaweka lakini nyuki wamekuja wameingia na kuweka makazi yao kule juu kabisa kwenye kona ya kench. waiingia mwezi wa nne mwishoni na sasa nikihesabu naona masega zaidi ya kumi.
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
Napenda kujua nikiwa na mizinga 500 naweza kuiweka kwenye eneo la ukubwa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…