Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 

Je hiyo subwoofer ukigeuza nyuma kule ina ki plastic tu hivi ambacho ukifungua hicho ki plastic ndio kimebeba raman kwa ndani?
Au inafunguka yote huku nyuma?
 
Sabufa yangu inanguruma sana boss.....nashindwa kujua tatzo ninini
 
Mkuu leo nimeiwasha gafla ikatoa mlio fulani hivi ikazima moja kwa moja sa sijui ndo imeungua au vipi

Na je kama imeungua uwezekano wa kuwaka tena upo mkuu?
 
Mkuu leo nimeiwasha gafla ikatoa mlio fulani hivi ikazima moja kwa moja sa sijui ndo imeungua au vipi

Na je kama imeungua uwezekano wa kuwaka tena upo mkuu?

Mala ya mwisho uliniambia inakwangua bass speaker ? Je imezima display ya hapo mbele au imezima mziki ila inawaka?
 
Nilikuwa ninautafuta sana huu uzi.
Nataka kununua sabufa simple tu ya kuanzia maisha.Naomba kuuliza ni kampuni gani nitaweza kupata sabufa original?
Naogopa kupigwa na wajanja wa mjini

Mama unapozungumzia subwoofer original unasemea labda hizo sonny. Samsung au lg labda
Ila hizi zingine kama seapiano,aboda hizi common unazoziona nyingi mtaani ni zakichina zooote!

Kama utanunua seapiano basi hiz zote zilizojaa madukani ni digital mode
Inahitaji ustaarabu kuitumia!
Usipige kwa sauti kubwa muda mrefu!
Usiruhusu mende au panya kuingia ndani!
All in all subwoofer zote ......zakichina usiitumie kwa fujo itakusumbua

Upo mkoa gani kama dar @Extrovert anasema kuna duka la hawa kodjec angeweza kukuelekeza zile naonaga zipo vizur sana
 
Inanguruma spika kubwa ya sabufa boss twita hazina tatizo inaimba boss ila inanguruma na kuna saa mngurumo unapotea na kuna muda unarudi

Capacitor zimelegea ,kazi ya capacitors ni ku stabilizer flowing currents
Hivyo diodes zinatoa dc current ila muda inapokoloma maana yake capps zimeachia hivyo current zinaingia kwenye raman zikiwa hazijakaa sawa
Muda inapopiga vizur hizo capps zinakua zinafanya kazi

Uliiamisha hamisha au kuidondosha redio?
Kam ndio bas ndio maana ila kama haikufanywa hivyo yaweza kua ile soda waya imeachia.
 
asante kwa maelezo mazuri.a
Niko Morogoro
 
Bahati mbaya haioneshagi display (niliinunua hivyo hivyo_used)japo ilikuwa inapiga fresh bila hata display.

Itanipa wakati mgumu sana
Mkuu kwahyo kujua kama inewaka ulikua ukiwasha inalia puu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
By the way huenda fuse za circuit zimekatika
Ila lazima tujue why zimekatika
Kama speak ilikwangua coil bas huenda imepelekea ic ku short
Ukichome kwenye umeme haiungulumi kabisa?
 
Nimeikagua mda huu nimekuta na mende wengi japo niliziba sehemu ya kupumulia hewa na chekecheche sielewi wameingiaje mkuu.

Kikubwa naomba Mungu iwake tu, lile swala la kukoroma najua siyo kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…