Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Umejuaje mkuu?Umeangalia kitu gani?

Speaker ukiingalia tu unajua hi ni ipi
Speaker za mid bass zinakua na mpira mdogo kiasi na spider yake inakua imeachia matuta
zinakua zinauwezo wakudunda
Kifupi ndio hizi zinazotumika kwenye ma redio ya hifi
Ila mid normal inakua haina mpira kabisa
Inakua na mikunjo kiasi ya kuiwezesha kutoa sauti tu
Japo inakibass ila sio kubwa
Tweeter inakua ni ndogo sana inaeleweka
Ila bass sasa[emoji23][emoji23] mpira mpana
Spider matuta yake yamejikusanya
Na sumaku inarud nyuma
 
Mkuu
Nimesoma huu uzi woote, nikalinganisha na music systems nilizowahi ziona, nimekubali Hi Fi ndo iko poa kwa tunaopenda mziki mzuri.
So now nataka nijue kibongo bongo hasa kwa wew ulie jirani na mimi (niko Makambako ) naweza pata Hi Fi kwa bei ya kawaida ata ikiwa used? Maana tozo wengine zimetukaba.
Natanguliza shukrani
 
Hii bass yake ni hiyo speaker ya tatu kutoka kushoto?
 
Wafanyabiashara wanaenda na upepo, watu walikimbilia Home theatres, Sub woofers na sasa sound bars ndio maana biashara ya Hi-Fi kwa bongo ikadolola, lakin huko Duniani Hifi zipo sana.
 
Hapo uki parallel mzigo unaenda 2ohms
Ila me siifanyi hivyo
Hivi hzi ohms zina impacts gani hasa kwnye sound quality ya kifaa husika??

Pioneer naona karibu subwoofer zao zte zinaanzia 2ohms kwenda chini

Hyo spl 3001d4 umepqnga kununulia wapi? Kwa sababu najua ni toleo la nyuma snaaaa sio rahisi kuipata
 
Woofer ni hiyo spik inayocheza low frequency
Au niseme inayodunda
Kwa mfano zote hapo zina woofer
Unajua maana ya 2.1 channel
Hivi mkuu hpa bdo nachanganyikiwaga

Kuna utowauti wa woofer na subwoofer??

Sio kwamba woofer ndiyo midbass/ midrangw speaker inayocheza mid frequencies??

Halafu subwoofer ndo inacheza low frequencies??
 
Kwanza kwa vyovyote vile haiwezi fika huko

Mziki wa watts 10000 unasikika km 15 kutoka ulipo sio mchezo

Ile miziki ya sherehe tu unayoiskiaga total output imezidi sana watts2000

Sasa chukulia 10000 watts[emoji16]

Inakua ni noma sana
 
Hivi hzi ohms zina impacts gani hasa kwnye sound quality ya kifaa husika??

Pioneer naona karibu subwoofer zao zte zinaanzia 2ohms kwenda chini

Hyo spl 3001d4 umepqnga kununulia wapi? Kwa sababu najua ni toleo la nyuma snaaaa sio rahisi kuipata

Ohms ni ukinzani wa coil ya ndani ya speaker
Zile coil zinatofautiana mizunguko
Ikiwa ina mizunguko mingi basi itakua na ohms nyingi
Ila ikiwa na mizunguko michache basi itakua na ohms chache
Coil zinatofautina unene
Hapo ndio watts inapokuja
Ndio maana utaona inaandikwa 4ohms watts2000 au vyenginevyo
Ikiwa hautazingatia ohms kuna madhala
Kama usipozingatia watts pia
Hivi vitu vyote vinaenda pamoja..

Je unaweza kutofautisha hi
Scania kufunga engine ya hiace
Au hiace kuvuta mzigo wa scania[emoji23]



Ndio haya mambo mawili
Watengenezaji wa amplify lazima wakupe ohms ya spika
Lazima wakupe na watts pia
Ukiweka ohms nyingi kuliko ila watts chache inaungua spika
Ukiweka ohms chache ila watts nyingi unaunguza mashine

Kuweka ohms nyingi au chache ni maamuzi ya amplify yenyewe kutokana na ilivyotengenezwa
Unaweza piga 2ohms kwenye amp hi ukienda kupiga kwingine unaharibu
Kwahyo kifupi ni kusoma specifications
 
Hivi mkuu hpa bdo nachanganyikiwaga

Kuna utowauti wa woofer na subwoofer??

Sio kwamba woofer ndiyo midbass/ midrangw speaker inayocheza mid frequencies??

Halafu subwoofer ndo inacheza low frequencies??

Zinaweza kua kitu kimoja ki maana au ki muonekano Muda mwingine ila
Zote kazi yake ni kucheza low frequency
Ila zinatofautiana freqnc zenyewe
Subwoofer inakita zaidi ya woofer
Na woofer inaweza toa maneno kidogo
Ila sio subwoofer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…