Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 

[mention]Behaviourist [/mention] [mention]Extrovert [/mention] kwa wadau wanao tumia hi!
Mala nyingi unaponunua utapewa tu speaker mbili yeen R,L
Ila pengine ungetaka kupata mdundo wa subwoofer
Nyuma huwepo na pin mbili za woofer outpost
Japo wengi hawajui inatumikaje
Chakufanya nunua single amp ya watts zozote unazotaka.,ambazo zitakua matched na speaker yako ya bass

Nyuma za receiver yako itakua kama hivi
Kuna pin zimeandikwa woofer out
Ambazo hapo n hizo zenye uweupe
Kisha nunua cable hi[emoji1370]
Hi utaunganisha hapo kwenye receiver yako na hiyo amp uliyonunua
Cable hi itapeleka signal kwenye amp yako
Kwahyo utapata mdundo kutok kwenye receiver yako.
 
Nilikutana na hii kitu ilikuwa imeua transformer
 
Je watts kwenye home theater ndio kipimo cha upigaji muziki wa kifaaa chenyewe

Sio kwenye home theater....
Kwenye kifaa chochote cha umeme ni nguvu ya kutenda kazi
Taa ikiwa na watts nyingi maana yake inamwanga mkubwa
Redio ikiwa na watts nyingi manaa yake imetengenezwa kwa power supply kubwa inayopeleka umeme mwingi kwenye circuits zake,sawa na kusema amply yake n kubwa hivyo inauwezo mkubwa hivyo itakua na sauti kubwa.
 
Nina swali moja mkuu,
Miaka ya nyuma kidogo kama miaka ya 2000 hivi kulikua na radio OG na mziki mkubwa mzuri,
Kama Sony, Panasonic
Kenwood
Pioneer, na wengine.
Lakini tuplipokuja kwenye ulimwengu wa Home Theatre mbona kama music sio mzuri kama wa zile radio?

2.Nimeona mahali Sony Mutek..kama 5.2, 7.1,2 had 8
Ni toleo jipya baada ya Home Thietre au ni vya zamani??
 

Muziki ili utoke vizuri unahusianisha vitu vingi
Power supply
Amplifier yenyewe
Op amp( operation amplifier)
Speaker selection
Na box design
Hiv vitu vyote pamoja vinaunda mziki
Ikiwa kimoja wapo kitaenda vibaya definitely huwez kupata unachokitaka
Nowadays watu wanaangalia hata muonekano,hata kama sio fresh sana ila kama muonekano utakua wakuvutia basi kitauza sana( ndio maan mchini anapiga hela hapa)
Miziki mizuri still ipo mkuu n nadra tu kukutana nayo,na ukiipata inakua ghali)

Hizo number za 1,2,3,4,5-8 .1,2 ni channel tu ambazo zinaelezea system ya redio husika,hazina uhusiano na usasa au u zaman wa kitu
Zazaman zilikua 2.0 nyingi
Baadae wakaingiza woofer ikawa 2.1 na baadae HT zikaingia
 
Naomba mfano halisi napata wapi mziki mzuri ulioshiba, nimewahi kua na Sony Home Theatre 600W, mziki mzuri kiasi ila haukuwa mkubwa.
Nikaja kua na LG 1000W.
Still naona ni wa kawaida.,then ni opt aina gani tena labda jitapata ninachohitaji.?
 
Naomba mfano halisi napata wapi mziki mzuri ulioshiba, nimewahi kua na Sony Home Theatre 600W, mziki mzuri kiasi ila haukuwa mkubwa.
Nikaja kua na LG 1000W.
Still naona ni wa kawaida.,then ni opt aina gani tena labda jitapata ninachohitaji.?

Unataka mziki mkubwa wa HIFI wenye woofer pembeni?
 
AV receivers, system za matajiri hizo.
 
Av receiver kwa Bongo bado sana, ila kwangu nahisi ndio powerful home music system.


AV receivers speakers


Hizi zinakuja na features nyingi ukiachilia mziki mzito, ina vitu vya ziada kama

HDMI ports,
Built-in Chromecast,
DTS Play-Fi,
Wi-Fi
Spotify Connect,
AirPlay and Bluetooth.
Set up tofauti tofauti za speakers 2.0, 2.1, 6.1, 7.1. 7.2.1, etc
 

Pole mkuu,sorry nmechelewa ku reply sababu ya kazi na mazingira.....
Hua inasemekana japo sija verify sababu sijacheza sana n STK ila wanasema stk og ni ile inayokuja na mashine zingine hizi ni majanga matupu,ndio bola uweke amp ya kawaida,.....
Nikupe mfano mdogo unakuta engine fulani ya gari vipiri vyake havipatikani au ghali sana...unatafuta engine ambayo iko wide..rahisi na salama...ambayo unaweza kuitumia kwenye mazingira yako bila shida!
Hi ni sawa na hiyo issue yako
Hapo ni kuona ilikuepo stk ngap...yenye watts ngp
Kisha itasukwa amp inayoendana n hiyo stk (watts) kisha itaingizwa humo na kufanya kazi kama kawaida
Pia kama hiyo radio haina Bluetooth unaweza weka pia
Hi hata mimi naweza kufanya ila sijui upo wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…