Nsansa, Matobolwa, makewe , uyoga, asali, kumbikumbi ,matini, nyama pori, mahama vilindo vyungu, wadudu wengine wanaoliwa kama wale wanaopatikana kwenye miti iliyooza na wale wenye mafuta mithili ya siafu lkn wana tank lenye mafuta
Vitu hivyo vipo?
Sijazungumzia ukubwa jombaaa, nimezungumzia hatari ya nyoka huyo koboko ni hatar kuliko AnacondaUsimfananishe ANACONDA, the world biggest snake na vitu vya kijinga.
Kuna hoteli moja tu nzuri, kuku wa kuchoma wapo sehemu moja tu (kwa mujibu wa muda nilipopita huko) wilaya ni kubwa mno mno mno. Wakati tunapita maporini tuliambiwa tusiache vioo vya gari wazi tusijegongwa na koboko.
kuna muhenga humu anaitwa Sikonge
Mkuu nimekuuliza kuhusu Iwensato Lodge ya Sikonge hujanijibu,au siku hizi haipo?we we ndio mmiliki?Hilo siwezi kumjibia
IMkuu unamaanisha gari au Punda?
Dah!!!! We jamaa ni shemeji yangu ...Wilaya ya Sikonge ipo Kusini ya Mkoa wa Tabora, Wilaya hii inapakana na Wilaya ya Uyui Kaskazini na upande wa Mashariki inapatikana na Mkoa wa Singida.
Kusini inapakana na Mkoa wa Mbeya Kusini Magharibi inapatikana na Mkoa wa Katavi na upande wa Magharibi inapatikana na Wilaya ya Urambo.
Wenyeji wa Wilaya hii ni wanyamwezi huku shughuli zao zikiwa ni kilimo ufugaji na uwindaji.
Mazao yao makuu yakiwa ni Mahindi, Maharagwe, Karanga, Mhogo na Mpunga. Huku zao kubwa la biashara likiwa ni Tumbaku.
Wilaya hii inajishughulisha pia katika ufugaji wa nyuki na inasemekana kuwa asali ya Tabora ndiyo asali iliyobora kuliko maeneo mengine yote katika nchi yetu.
Mkuu laki 149.8 ndiyo kiasi gani?Kwa inakadiriwa kuwa na watu laki 149.8 kwa majibu wa sensa ya 2012
Tabia za kufukuza gari hizo hana wala sijawahi kusikia.
DuhWilaya ya Sikonge kwa muda mrefu haikuwa na barabara ya kukatisha kuingia na kutoka kwenye mikoa mingine - kifupi Wilaya ilikuwa kama kisiwa hivi. Kwa sasa ndiyo kuna barabara inajengwa toka Tabora mjini kupitia Sikonge hadi Katavi.
Barabara hii sasa ndiyo itahuisha biashara kati ya wilaya ya Sikonge na Katavi hadi Kigoma.
Ardhi ipo ya kumwaga, lakini kilimo chochote kinahitaji Mbolea, Mzunguko wa pesa hakuna - maisha ni magumu mno hasa wa vijana na kina mama.
Chakula kikuu ni Ugali wa Mahindi - Mboga ni Mlenda, Swalu, nsansa, kisanvu ma msusa - Mboga zote hizi zikiungwa kwa tui la karanga!! Uhodari wa wanawake wa Kinyawezi ni ile sifa yao katika mapishi - ni hatari.
Huko nasikia furniture za mninga ni bei nafuu mnoIwensato hongera kwa kuitangaza sikonge vizuri.Huo ni Uzalendo kweli.
Naomba niweke takwimu sahihi kidogo kuhusu SKG.
Nyoka hatari zaidi ni Hugo uliyemtaja kwa kiswahili -Koboko (Black Mamba).sio Cobra(Swila).
Wanajamii Sikonge ni pazuri kama sehemu nyingine Tz.
Zipo changamoto ambazo Mimi kwa uzoefu wangu wa muda ambao niliishi skg(2010 - 2017).
1. Unyamwezi umezidi sana - Wizi wa kuku,kuvunja nyumba watu wakiwa makazini umezidi aisee.
Sio wanaofanya hivyo ni wanyamwezi wote ni baadhi ya wakosa kazi wa Usega/Misheni na madukani kwa waarabu,wanapachafua sikonge sana,Hawawachukulii sheria mkononi kama watu wa mikoa mingine wanavyofanya! Unakuta mwizi wa kuku na TV za watu ni Mtoto wa Shangazi inabidi mnyamwezi atupe fimbo aanze kumtetea binadamu yake.
Wanyamwezi wanapata hela lakini sio risk takers! Wameucha uchumi mikononi mwa waarabu (I don't like it).
Wageni njooni sikonge mfaidike Luna fursa balaaa.
Asali,mbao,Mazao,Maeneo na nk.
Naomba kutoa hoja.