Niulize chochote kuhusu zao la nyanya nitakujibu kama mkulima

Mathayo Christopher

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
413
Reaction score
289
Niulize chochote kuhusu zao la nyanya nitakujibu kama mkulima.

IMG_0222.jpg

Yale mavuno ya nyanya ambayo huwa yanaandikwa kwenye package ya mbegu ni kweli yanatokea? Mfano Asila F1 mavuno yake ni 50tonne/acre
Hayo mavuno ni sahihi kama utaheshimu kanuni za kilimo kuanzia unapo sia mbegu kwenye kitalu, kupandikiza,uwekaji wa mbolea,upuliziaji wa fungicide + insectide, umwagiliaji na steming ya miche
 
Karibuni kwa maswali japokuwa kitaaluma ni mwalimu ila miaka saba niliokaa kitaa na kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji hasa nyanya na mahindi kuna mengi nimejifunza nawakaribisha
Nahitaji kulima kilimo Cha umwagiliaji eneo la wazi unanishauri niandae kitaru mwezi gani ili nitoe nyanya kipindi ambacho soko linakua zuri?
 
Soko la nyanya huwa juu nyakati za masika na husababishwa na changamoto za ukungu hivyo mda sahihi wa kusia mbegu kwenye kitalu ni mwezi desember ili uvune mwezi march .
 
Ingia shambani standard ya faida ya kilimo kwa zao lolote ni 50% of the input surplus kwenye zao la nyanya husababishwa na demand and supply
 
Kitalu cha miche ya nyanya kinatengenezwaje kitaalamu kuanzia kuandaa kitalu hadi kupanda na kuota naomba nipate kujua maana mwezi wa tisa naanza rasmi
 
Kwanza tifua sehemu unayotaka weka kitalu kisha weka majani makavu na kuni ndogo sehemu uliotifua kisha choma .acha kitalu kipoe kwa siku mbili ,baada ya kitalu kupoa tengeneza vifereji vidogo vyenye kina cha sm 2 utakavyochora kwa kijiti chenye ukubwa wa penseli na tofauti ya mstari wa mfereji mmoja na mwingine ni sm 15 weka mbegu katika kila mstari kisha nyunyiza mchanga kidogo kufukia mbegu .weka matandazo na uanze kumwagia siku ya tatu baada ya kusia mbegu puliza sumu ya wadudu na siku ya sita utaondoa matandazo na kufunika neti siku ya saba utaweka DAP kwa ajili ya kukuza mimea michanga na siku ya nane puliza sumu ya ukungu na kuanzia hapo utapuliza sumu ya ukungu kila baada ya siku tano .mbegu ya nyanya huota ndani ya siku tano hivyo baada ya kuota siku ya saba puliza sumu yenye kiambata cha emmamectine benzoate au abamectine hii ni maalumu kwa kudhibiti kanitangaze pia miche ya nyanya kwenye kitalu utamwagilia katikati ya mstari na mstari kwa kuweka maji katika chupa ya maji na kunyunyiza kati ya mstari na usimwagie kwa juu
 
Asante saana mkuuu
 
Niulize chochote kuhusu zao la nyanya nitakujibu kama mkulima.

Nimezaliwa kijijini ambako tumelima Nyanya na majirani pia wakilima nyanya lakini Tangu nizaliwe sijawahi kuona Mzao/ mti wa nyanya ukitoa Mbegu. Hizo mnazopandikiza zinatoka wapi? Kwanini miti ile haitoi mbegu tukaziona shida ni nini?

Asante ndugu Mwl Mkulima
 
Na mm nina swali kama hili
 
Back
Top Bottom