Niulize chochote kuhusu zao la nyanya nitakujibu kama mkulima

Niulize chochote kuhusu zao la nyanya nitakujibu kama mkulima

Nyanya zangu zina miezi miwili tangu nimepandikiza shambani zimeanza kuiva. Ila nyingine zina baka jeusi chini hii ina sababishwa na nini?
 
Karibuni kwa maswali japokuwa kitaaluma ni mwalimu ila miaka saba niliokaa kitaa na kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji hasa nyanya na mahindi kuna mengi nimejifunza nawakaribisha
Nyanya zangu zina miezi miwili tangu nimepandikiza shambani zimeanza kuiva. Ila nyingine zina baka jeusi chini hii ina sababishwa na nini?
 
Nunua mbegu za hybrid za F1 na fuata taratibu za uandaji wa kitalu cha kusia mbegu ya nyanya
 
Naomba ushuhuda wa nyanya kwako binafsi.

Je imekufilis, imekutoa au bado unaisikilizia iije ikutoe?
 
Nyanya zangu zina miezi miwili tangu nimepandikiza shambani zimeanza kuiva. Ila nyingine zina baka jeusi chini hii ina sababishwa na nini?
Kuna upungufu wa madini ya calcium na ndiyo maana mtaalamu kushauri kutumia mbolea ya CAN; lakini pia inaweza kuwa madini ya calcium yapo na bado tatizo likawepo, hapo itakuwa ni maji kidogo, yaani mmea hauwezi kupata hiyo calcium bila maji ya kutosha, ndiyo maana mtaalam kaushauri utumie maji ya kutosha.
(kwa kiingereza wanasema low calcium intake - which may be caused by lack of calcium in the soil or lack of medium to transport calcium to the plant that is water)
 
Back
Top Bottom