TOEFL na IELTS sanasana ni kwa nchi ambazo their first language is English kama vile UK, US, CANADA, Australia n.k
Kwahiyo kwa nchi za Ulaya kama vile Scandinavian (Sweden, Finland, Norway, Denmark) na nchi nyingine za Ulaya kama Austria, France, Germany na Netherlands ambako lugha yao ya kwanza siyo English, hizo mambo za IELTS na TOEFL kwa uzoefu wangu, kwa kiasi kikubwa sijaona wakiomba uwe umefanya hiyo mitihani.
Hivyo, kwa jibu fupi, ili usome Sweden kwa sisi Wabongo ambao tunatumia English kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, tunahitajika kuwa tumefaulu English O-level. Hicho ndicho kigezo pekee ninachokifahamu.
Katika swali lako la pili; nchi zilizoendelea(Ulaya) wanathamini sana Utamadumi wao; hivyo lugha ya mawasiliano ni lugha yao. Kwa Sweden wanatumia Kiswidi(Swedish). Hata hivyo; karibia 85% ya Waswid wanazungumza English vizuri kabisa. Ukipata Scholarship, lugha ya kufundishia kwa Masters ni English.
Suala la Ubaguzi naomba nilisizungumzie sana; binafsi sijawahi kukutana na changamoto hii. Sweden na Nchi nyingi za Scandinavian wanajitahidi sana kuthamini utu wa kila MTU. Ila siku zote, mweusi ni mweusi na Mzungu ni Mzungu tu. Japo hutaona Ubaguzi kwa kusikia wala kwa macho, ila kiasili mweupe ni mweupe na mweusi ni mweusi tu.
Generally, nchi nyingi za Ulaya kwa sasa Ubaguzi siyo agenda kubwa. Sanasana labda Ubaguzi utausikia kwa Wazee na Watoto. Ila vijana wamestaarabika. Mwisho kabisa, kwa mtizamo wangu, nadhani Sweden ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ustaarabu Duniani.
Sent using
Jamii Forums mobile app