Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Nauli unajitegemea mpaka kufika. Ukishafika unarudishiwa gharama zako za nauli.
Nashukuru sana mkuu!!

1. Hapa Tz ukiwa na buku tano unatoboa siku, je huko gharama za maisha zikoje? roughly kwa matumizi ya chakula inaweza cost ngapi kwa siku?

2. Je account unafungulia huko huko kwao au ni hizi zetu?
 
Huwezi ukadanganya kama hauna leadership experience...sijawahi kuwa kiongozi.
Wabongo huwa hawashindwi kitu. Ila mkuu, leadership experience siyo mpaka uwe manager au CEO au Mkurugenzi. Hata kama una NGO au Community organization yoyote iliyosajiliwa na kutambulika hata kama ni kijijini kwenu, na ukawa unaongoza kufanya activity yoyote katika majukumu yako, tayari hiyo ni leadership experience. Bila shaka umenipata mkuu.
 
 
Nimekupata vizuri mkuu. Naomba nikutafute inbox nikianza kuapply. Shukrani.
 
vp kwa master ilikuwa na uakika wa full funded masters scholarship unatakiwa uwe angalau na GPA ya ngap?
 
vp kwa master ilikuwa na uakika wa full funded masters scholarship unatakiwa uwe angalau na GPA ya ngap?
Sijawahi kuona wakitaja GPA kama kigezo. Japokuwa nadhani ukiwa na atleast Upper second unakuwa kwenye chance nzuri zaidi. Wenzetu hawaangalii sana ufaulu wa kwenye makaratasi. Wanangalia uwezo wa mtu. Hata hivyo kufaulu vizuri ni added advantage.
 
Nadhani TOEFL na IELTS inategemea na chuo bila kujali national language, kuna vyuo vinahitaji hiyo na kuna baadhi ya vyuo havihitaji
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani TOEFL na IELTS inategemea na chuo bila kujali national language, kuna vyuo vinahitaji hiyo na kuna baadhi ya vyuo havihitaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua mkuu mie nili-Generalize kwa sababu nilipata fursa Sweden sikuhitajika kuonesha TOEFL/IELTS certfificate. Hali kadhalika Netherlands pia sikuulizwa, na kwenyewe hawakuhitaji. kuna jamaa yangu kasoma German na yeye anasema hawahitaji. Jamaa zangu wengine kama 10 hivi wanasoma vyuo mbalimbali Sweden na wao hawajawahi kuulizwa hilo. Basi nikawa nime-Generalize, kumbe kuna vyuo specific hata Sweden wanahitaji? Sikujua hili.
 
Ulipataje passport kabla hujapewa joining instructions maana uhamiaji wanataka invitation letter ili upewe passport.Kingine,kuna fursa za kupiga box ili ukirudi bongo uje na mtaji kama ilivyo marekani na Ulaya magharibi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Passport nilipata kwa sababu nilikuwa na admission letter ya kutoka chuo cha Nchi nyingine ya Ulaya nilikuwa nimepata kabla ya kupata admission ya Sweden.

Fursa za kupiga box zipo mkuu, ni bidii yako tu kama utaweza kuhimili masomo na kazi. Tofauti na mitizamo ya watu wengi, shule ya Ulaya hasa niseme Sweden ambako nina uzoefu nako siyo ya kula bata kama wanavyosema watu. You really have to study very hard to survive. Ila hili pia libaki kwa mtu mwenyewe, maana uwezo wa mtu na mtu pia hutofautiana. Mie naweza kutumia muda mwingi kusoma ili ni-survive, at the same time mtu mwingine kwa sababu ya uwezo labda alionao akatumia nguvu kidogo tu na akatoboa. Ila kwa ujumla shule siyo bata kama wasemavyo. Ni shule shule kweli.

Ukiwa na mpango wa kazi za box Sweden unaweza kufanya maandalizi mapema ya kujifunza Kiswid taratibu maana wanatumia lugha yao kwa kila kitu almost 99.99%. Kitu kingine, ukiwa unafahamu kuendesha gari na una leseni ni added advantage. Japokuwa leseni yetu ya Bongo kwa Ulaya haitambuliki, ila angalau hata ukienda kufundishwa kupata leseni yao angalu hautatumia nguvu kubwa sana.
 
Sorry nikimaliza first degree ni lazima nipate KAZI Kwanza na nifanye Kwa muda kidogo ndo niombe scholarship?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni rahisi mtu mwenye uzoefu wa kazi kuchukuliwa kuliko amabye hana,hata hivyo kama hujapata bado ajira but ufaulo wako upo vizuri napo ni rahisi kuchukuliwa.
 
Asante sana kwa majibu mazuri. Kwenye ishu ya passport tunakwama sana hapo. Kama hutojali ungetupa mbinu za kuipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa majibu mazuri. Kwenye ishu ya passport tunakwama sana hapo. Kama hutojali ungetupa mbinu za kuipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbinu muhimu ni kumuomba sana Mungu akujalie ili kila utakachozungumza pale Uhamiaji kiwe na kibali kwao na ufanikiwe. Hiyo ni mbinu muhimu niliyoitumia na nikaona matokeo yake.
 
Nchi zipi huko watu wake wanapewa kipaumbele zaidi kupata scholarships?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…