Niunganishe soko la Kitunguu Kampala

Uko wapi mkuu, moshi huwa kuna mhindi mmoja anakuuzia mbegu anakupa na guarantee, zisipoota atahusika, anasifika kwa kuuza mbegu poa
Mkuu me nipo dar,ila kilimo nafanyia morogoro
 
Uko wapi mkuu, moshi huwa kuna mhindi mmoja anakuuzia mbegu anakupa na guarantee, zisipoota atahusika, anasifika kwa kuuza mbegu poa
Huyo mhindi ndio anauza bei hiyo au?ukienda kariakoo kopo la gram 50 ni sh 6000 halafu chance ya kuota ni ishu
 
Kwa dar, balton wanauza mbegu nzuri tu, hawababaishi tena bei ni poa kabsa
asante kwa taarifa mkuu me nilikua najua bei za balton ni kubwa sana, maana niliwahi kuuliza kuhusu greenhouse mpaka nikakata tamaa, unaweza kujua bei za balton kwenye hizo mbegu?
 
asante kwa taarifa mkuu me nilikua najua bei za balton ni kubwa sana, maana niliwahi kuuliza kuhusu greenhouse mpaka nikakata tamaa, unaweza kujua bei za balton kwenye hizo mbegu?
Kweli sijui, ila nimekuwa na uzoefu wa mda mrefu kuwa balton wanauza mbegu nzuri tu na bei ni poa kabsa
 
Kweli sijui, ila nimekuwa na uzoefu wa mda mrefu kuwa balton wanauza mbegu nzuri tu na bei ni poa kabsa
Poa haina shida nitawacheki,kilo tatu za mbegu mkuu space yake ngapi kwa ngapi ukipanda shambani?
 
Poa haina shida nitawacheki,kilo tatu za mbegu mkuu space yake ngapi kwa ngapi ukipanda shambani?
Kama ilivyo ona kwenye hiyo picha yaani kumi hadi kumi na tano cm
 
Kama ilivyo ona kwenye hiyo picha yaani kumi hadi kumi na tano cm
sawa, ekari moja inaweza kutoa magunia mangapi, mkuu kwa bei hiyo ya 70,000 ukiuza faida inakuwa hakuna? maana naona kuna mtu hapa kasema mpaka mwezi wa pili bei itakuwa vizuri lakini naona mwezi wa pili singida huwa wanatoa vitunguu vingi halafu vina flood market then bei inapungua kabisa
 
Reactions: MC7
Acha woga mkuu. Kila kitu kimejaa changamoto, there's no flat way toward success. Wewe ukiamua kulima na ulime. Procrastination results into regression. Ukianza kuchunguza sana haya mambo ya uchumi pamejaa visiki. Hata ungeuza kwa hiyo 70000 bado una faida, assume for minimum yields 60 bags per acre, milioni 4 na vilaki, lakini gharama ya kuhudumia haitafika huko
 
nimekuelewa kabisa mkuu, kweli uoga ndio umasikini, mfano watu waliolima mahindi mwaka huu watakuwa wamepata hela ya kutosha sana,mahindi kila siku yanapanda bei si mchezo
 
Huyo mhindi ndio anauza bei hiyo au?ukienda kariakoo kopo la gram 50 ni sh 6000 halafu chance ya kuota ni ishu
Kama mkuu alivyosema mbegu nzuri Ni red bombay ambayo inatoa kitunguu chekundu. Lakini hizi mbegu kuna makampuni mengi yana tengeneza kwahiyo Ni vizuri kuwa makini

Kampuni inayo sifika Ni East African seeds ipo kenya mbegu Yao ya red Bombay inaitwa African best.

Nyingine inakuwa Simlaw, hii inatengenezwa kenya lakini kuna mawakala wa kuifanyia packaging wapo Uganda wengine hapahapa bongo

Hizo ndio mbegu ambazo binafsi mtaalamu wangu anatumia Na hazijawahi kumuangusha. Kuna red Bombay inatengenezwa hapahapa Tz Na kampuni inaitwa Meru seeds, hii Sina uhakika nayo sijawahi itumia

Mbegu za kienyeji Zina ishu moja ratio ya kilo za mbegu Vs idadi ya gunia zitakazo toka Haina uhakika sana. Unaweza kumwaga mbegu nyingi usipate uhakika wa kuvuna gunia 70 Kwa ekari.

Mwisho usinunue mbegu nyingine yoyote zaidi ya red Bombay maana wengine huwa wanakosea wana nunua red cleori, hii Ni kimeo.
 
sasa mkuu, vitunguu ukitumia hiyo mbegu ya Bombay unaweza kuvihifadhi kwa muda gani baada ya kuvuna?
 
Mkuuu Mimi ni mkulima wa Vitunguu bt siku zote Huwa natumia mbegu za dukani Na Zinaota Na mpaka Sasa Nina Vitunguu viko shamba karibu ninavuna
 
sasa mkuu, vitunguu ukitumia hiyo mbegu ya Bombay unaweza kuvihifadhi kwa muda gani baada ya kuvuna?
Mbegu ingene nzuri ya dukan ni neptune f one ingawa ni ghali sana ila mavuno yake yako juu sana, kama umehudumia vizuri unaweza pata zaidi ya gunia 120 kwa eka moja.
 
Reactions: MC7
Mkuuu Mimi ni mkulima wa Vitunguu bt siku zote Huwa natumia mbegu za dukani Na Zinaota Na mpaka Sasa Nina Vitunguu viko shamba karibu ninavuna
mkuu muda mzuri wa kuvuna kutokana na soko letu ni upi? na je wewe ulipanda mwezi wa ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…