Niunganishe soko la Kitunguu Kampala

Mkuu yaani kitunguu kimoja tu nacho utafute soko la nje?
 
mkuu muda mzuri wa kuvuna kutokana na soko letu ni upi? na je wewe ulipanda mwezi wa ngapi?
Inategemeana Na soko likoje bt kama utafanikiwa kutoa mwezi wa pili soko Huwa nzuri gunia Huwa linaenda laki 2 Na nusu hadi laki 3
 
Inategemeana Na soko likoje bt kama utafanikiwa kutoa mwezi wa pili soko Huwa nzuri gunia Huwa linaenda laki 2 Na nusu hadi laki 3
mwezi wa pili mtihani sana huku mvua huwa zinanyesha katikati hapa mwezi kuanzia mwezi wa kumi na moja hapo kama ndio vikaribia kuvunwa mvua ikija hasara lazima itokee
 
Ndio mkuu huyu jamaa anaetumia kilo 3 kwa heka ana panda umbali gani kati ya mche Na mche
Yaani mi nawambia mbegu ya kutosha eka ni kilo 3 niko field, siyo notes za kwenye makaratasi. Hiyo picha nimeatach nimepiga leo shambani kwangu. Kuhusu spacing ni kama inavyoonekana kwenye hiyo picha, yaani 10 adi 15cm. Mbegu ambayo siyo hybrid udipomwaga kilo tatu jiandae kuja kununua miche kwa wakulima wenzako ambao wanauza ghari kuzidi maelezo.
Labda nianze hivi, jambar ni mbegu bora ya kitunguu ambayo inauzwa bei ghari kuliko. Inakadiriwa kuwa kilo moja hadi moja na nusu inatosha kuoteshea shamba la eka moja. Na inauzwa laki tatu na therasini kwenye ujazo wa nusu kilo. Kwahiyo ya kutosha heka ni laki sita hadi laki tisa. Na mbegu hii inatumika kidogo kwa sababu ni hybrid. Ina 99percentage of germination hivyo ukimwaga inatoka yote.
Mbegu nyingine inayofuatia ni Neptune. Nayo ni nzuri ila haifiki kwa jambar japo nayo ni f1. Inauzwa kilo laki tatu na sitini ila bei inategemea na wauzaji. Hii inahitajika kilo mbili hadi mbili na nusu kutoshea heka moja. Na nina ushahidi wa wakulima waliokuwa wameiotesha kilo moja na nusu kwa eka, matokeo wamenunua miche kujazia.
Mbegu hizi za hybrid zina matokeo mazuri kwani heka moja waweza pata gunia mia na....,
Changamoto ni kuwa vitunguu vyake ni vikubwa kiasi kwamba sokon haviuziki. Wataalam wanashauli ili kuminimize ukubwa wake ni lazima upande kwa kubananisha. Kama ndo mtu unaanza siyo mzoefu, bora lima hizi mbegu nyingine.
 
OK bt Mimi mkuu nilimwaga kilo Moja tu Na nikapanda heka Moja Na mwisho wa mwezi huu navuna Sasa Mimi sijajua hio yako ya kilo 3 kwa heka
 
Spacing yako mkuu ikoje, pia ebu attach picha
OK kesho nitapiga picha nikienda shamba bt mkuu Mimi nilichofanya kwanza kwenye heka nilikata majaruba nikapata Mia Na 50 na space nilifanya cm 3 mche kwa mche
 
mwezi wa pili mtihani sana huku mvua huwa zinanyesha katikati hapa mwezi kuanzia mwezi wa kumi na moja hapo kama ndio vikaribia kuvunwa mvua ikija hasara lazima itokee
Kweli mkuu bt Mimi nataka nikishavuna kesho kutwa nipande tena nitoe mwezi wa pili mwishoni Na changamoto hio ya mvua itakuwepo bt Mimi nitajitaidi kujenga machanja kwa ajili ya kukaushia
 
Kweli mkuu bt Mimi nataka nikishavuna kesho kutwa nipande tena nitoe mwezi wa pili mwishoni Na changamoto hio ya mvua itakuwepo bt Mimi nitajitaidi kujenga machanja kwa ajili ya kukaushia
changamoto ya mvua mkuu nazumgumzia kwenye mavuno yani vitunguu vikakaribia kuvunwa halafu mvua ikapiga hapo si vitaoza au uzoefu wako unasemaje kuhusu kitunguu kilichokomaa chini halafu kikakutwa na maji ya mvua? maana kuanzia mwezi wa 12 nchi nzima mvua inaweza kunyesha wakati wowote ule
 
OK kweli Vitunguu kama nitakuwa viko shamba Na tayari vimeshakauka vikikutwa Na mvua vinaoza bt mkuu Mimi nikienda December itakuwa vizuri Na mvua hata kama itanyesha itakuwa hamna shida Na vile vile itanipunguzia cost ya kumwagilia
 
OK kesho nitapiga picha nikienda shamba bt mkuu Mimi nilichofanya kwanza kwenye heka nilikata majaruba nikapata Mia Na 50 na space nilifanya cm 3 mche kwa mche
Umekosea mkuu, unajua 3cm ni nchi moja, very small not enough, labda umesahau vipimo ulivyotumia
 
Ahsante Mkuu ngoja nifatilie hyo sehemu
Poa fuatilia na hiyo kibati kuna mtu alichangia alisema kibati pia wanalima, kibati ipo Wilaya ya mvomero, Wilaya mvomero na kilosa zipo karibu karibu hasa kwa upande wa njia ya kwenda dodoma kutokea moro mpaka pale njia panda ya kwenda kilosa iliyopo dumila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…