Yaani mi nawambia mbegu ya kutosha eka ni kilo 3 niko field, siyo notes za kwenye makaratasi. Hiyo picha nimeatach nimepiga leo shambani kwangu. Kuhusu spacing ni kama inavyoonekana kwenye hiyo picha, yaani 10 adi 15cm. Mbegu ambayo siyo hybrid udipomwaga kilo tatu jiandae kuja kununua miche kwa wakulima wenzako ambao wanauza ghari kuzidi maelezo.
Labda nianze hivi, jambar ni mbegu bora ya kitunguu ambayo inauzwa bei ghari kuliko. Inakadiriwa kuwa kilo moja hadi moja na nusu inatosha kuoteshea shamba la eka moja. Na inauzwa laki tatu na therasini kwenye ujazo wa nusu kilo. Kwahiyo ya kutosha heka ni laki sita hadi laki tisa. Na mbegu hii inatumika kidogo kwa sababu ni hybrid. Ina 99percentage of germination hivyo ukimwaga inatoka yote.
Mbegu nyingine inayofuatia ni Neptune. Nayo ni nzuri ila haifiki kwa jambar japo nayo ni f1. Inauzwa kilo laki tatu na sitini ila bei inategemea na wauzaji. Hii inahitajika kilo mbili hadi mbili na nusu kutoshea heka moja. Na nina ushahidi wa wakulima waliokuwa wameiotesha kilo moja na nusu kwa eka, matokeo wamenunua miche kujazia.
Mbegu hizi za hybrid zina matokeo mazuri kwani heka moja waweza pata gunia mia na....,
Changamoto ni kuwa vitunguu vyake ni vikubwa kiasi kwamba sokon haviuziki. Wataalam wanashauli ili kuminimize ukubwa wake ni lazima upande kwa kubananisha. Kama ndo mtu unaanza siyo mzoefu, bora lima hizi mbegu nyingine.