Kufikia hatua ya kuteuliwa kugombea uraisi si kipimo cha ubora wa mgombea.Mara nyingi hatua hiyo hufikiwa kutokana na kubebwa na vyama tu, ambavyo navyo si kipimo cha akili za wananchi bali matakwa ya kimfumo unaotawala ulimwengu kwa sasa.
Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa. .............................................
Yaani ulivymuweka Kikwete ndo nakuona hujui kuchambua na
hutaki kusema ukweli. Labda una agenda binafsi. Ni kweli Lipumba anaweza kufaa kama alivyo Slaa.
Elewa Pia Lipumba na slaa wasingefaa kama wangekuwa ni wagombea kwa ticket ya CCM. Read between the lines uelewe namaanisha nini.
Vile vile elewa kwamba Kwa
mfumo huu tulionao ambao CCM inaukumbutia hata ukimleta OBAMA bado atakuwa anatwanga maji kwenye kinu.Ni kwamba tatizo la CCM sio kuwa na uhaba wa viongozi bora bali tatizo hasa ni mfumo wanaokumbitia ambao ndio unawafanya kuonekana kituko. Sababu kwa sasa kiongozi wao ni JK lawama zote anazibeba yeye.
Kwa hiyo kikwete amekuwa kichekesho zaidi sababu watanzania walikuwa na matumaini makubwa kuwa atabadilisha mifumo lakini mara baada ya kuingia ikulu kaona madaraka ni matamu, wajanja wamemdanganya utajipunguzia nguvu za kiutawala ukibadlisha mambo. Rais anayedanganyika kirais hafai.
- Kwa nini kashindwa kufanya TAKUKURU iwe huru?
- Kwa nini Serikali yake imewapeleka mahakamani maofisa wanashtakiwa kwa rushwa na bado anasimama nao kwenye majukwaa kuwapigia kampeni?
- Kwa nini Hawaundi Tume Huru ya Uchaguzi
Hii ni mifano michache ya mifumo ambayo mfumo wake unamfanya mtawala yeyote awe na zigo kubwa
Kikwete anauma na kupuliza. CCM imejaa chui na kondoo. Na cha ajabu Kondoo wameanz a kula nyama kama chui.
Ningejaribu kukuelewa japo kidogo kama ungemlinganisha Lipumba na na Dr slaa lakini kwa kumuweka dr Jakaya kikwete tena ukamuweka nafasi ya pili unaonyesha jinsi gani umeweka
ushabiki zaidi. na si ukweli
FACT ni kwamba CCM ni headache kwa watanzania. Mpaka hapo kiongozi 1ja atakapokuwa jasiri wa kubailisha mfumo.
FACT nyingine CCM kinaweza kuwa chama bora hata zaidi ya CUF na CHADEMA kikikaa nje ya Uongozi japo kwa miaka mitano. Kwa wanaoipenda CCM wasiwe waoga. Tuwaweke pembeni
wajipange na kujipangua.they will come back not only stronger but they way wananchi wanavyotarajia.
Kikwete anauma na kupuliza. CMM imejaa chui na kondoo wanaoishi zizi moja kwa amani. Na cha ajabu na kushangaza Kondoo nao wameanz kula nyama kama chui. wananchi tumeshtuka hili zizi la CCM halifai