Elections 2010 Niwaonavyo wagombea watatu wa urais

Mikomangwa the great!!!!!!!!! Big up.... Mpe vitu Ami hadi aelimike ila tusimlaumu sana maana kutojua si ujinga ila inambidi ajifunze kuuliza.
 


He he heee! Ha ha haaa! Week end hii napata ze laga na kitimoto hapa Rainbow-Mbezi.

Karibu ndugu Ami.
 
Ami nadhani utakuwa aidha ni FISADI, au utakuwa na UPEO MDOGO WA KUELEWA. Kwa sasa Tanzania haihitaji Rais anayefahamu sana mambo ya uchumi, tunahitaji mtu atakaye rudisha USAWA WA UFAIDIKAJI WA RASILIMALI za nchi, hivyo mtu huyo hatakiwi kuwa muoga, mwenye tamaa, n.k, sasa suala la Dr Slaa na mambo yake binafsi wala si tatizo, kwani hata wewe lazima unanyumba ndogo kama ni mwanaume, lakini wewe kama ni mwanamke basi utakuwa na lijibaba, na kama wewe ni mtoto basi baba yako au mama yako atakuwa na wa nje!!!. Hivyo Dr Slaa bado ni chaguo sahihi kabisa kwa mazingira ya Tanzania ya sasa. Anayempinga Dr Slaa basi hana akili na hapaswi kuwa mtanzania.
 

khaa, maajabu ya dunia haya, hivi kwanin wendawzimu wanaongezeka badala ya kupungua?
i
 
Elewa kuwa ipo tofauti kati ya kuwa mshauri na mtekelezaji wa lile unaloliamini.Mtu kama Mwinyi unadhani ana tofauti gani katika ukichwa ngumu kati yake na Nyerere?.Hata ukimshauri jambo jema akitishwa na akina Mrema alikuwa hawezi kutekeleza jambo.Na Museveni askari wa msituni asingeweza kushaurika na mambo ya kiuchumi.
Pamoja na hivyo kumbuka kuwa Uganda inasifika kupika hatua za kiuchumi kuliko Tanzania.Na wakati wa Mwinyi mpaka leo tunaukumbuka kuwa ulikuwa muongo wa ustawi wa kiuchumi.Jee huoni kwamba yawezekana ni yale machache waliyochukua kutoka kwa Lipumba.
 
Huna muono ila una mahaba ya kutokutaka kuukubali ukweli, hao unaoona wanafaa wamejenga ushirika wa kuhakikisha nchi haikombolewi, mwingine wivu mwingine king'ang'anizi ingawa hata afya haimruhusu huku umma umeshamchoka.
 
Ami,

..Prof.Lipumba alikuwa mshauri wa uchumi wa Mwinyi kwa kipindi kifupi wakati wa awamu yake ya pili ya uongozi.

..awamu ya pili ya Uraisi wa Mwinyi iligubikwa na mambo mengi sana ya hovyo-hovyo. binafsi siamini kama Mwinyi alikuwa akifuata ushauri wa Lipumba, au mtaalamu yeyote yule mwenye uelewa wa fani ya uchumi.

..binafsi nitampigia kura ya Uraisi Dr.Slaa, naamini anazo sifa za kutosha kuweza kuleta mabadiliko nchini.

..ushauri wangu kwako ni kwamba linusuru taifa lako kwa kuiondoa CCM madarakani.

..kama unaamini Dr.Slaa hana qualifications basi mpe kura yako Prof.Lipumba. usiharibu kura yako kwa kumchagua JK ambaye ame-prove kuwa hana uwezo wa kuongoza.
 
Huna muono ila una mahaba ya kutokutaka kuukubali ukweli, hao unaoona wanafaa wamejenga ushirika wa kuhakikisha nchi haikombolewi, mwingine wivu mwingine king'ang'anizi ingawa hata afya haimruhusu huku umma umeshamchoka.
Ukweli ndio huo kuwa tunataka mabadiliko lakini Slaa hana uwezo huo.Ikiwa CCM watabadilika kuleta mabadiliko sawa.Dalili zipo. Slaa hapana!.
 
Dr Slaa kwa mtazamo wangu hafai kuwa Rais bali mbunge tu. Elimu yake ya Bw Yesu Asifiwe itatusaidia nini watanzania kiuchumi. Sana sana ataiingiza nchi katika dimbwi la Ukatoliki na kusababisha kumwagika damu bure. Namshauri arudi msimbazi akamsaidie askofu Pengu
 
Ndugu Ami, sitaki kuamini hili lakini nadhani lina ukweli ndani yake, wewe unaongozwa na itikadi ya KIDINI ingawa hukutaja hapa moja kwa moja. Hivi unadhani elimu ya dr.slaa ni ya upadri peke yake? Je unajua viongozi wote wenye hekima duniani kuanzia karne ya 4 enzi za ROMAN EMPIRE walikuwa wanasoma philosophy? Je, unajua watu wanaosoma philosophy tena kwa undani zaidi ni pamoja na mapadri? Je, unajua duniani hakuna chuo cha kusomea uraisi? IWEJE USEME ELIMU YA DR.SLAA HAIENDANI NA CHEO ANACHOKITAKA?! mi nafikiri elimu yako ndo haiendani na yale unayoyachambua.
 
Fani ya eleimu yake hachaguliki kwa kundi kubwa la wapiga kura.Si muadilifu kwa nafsi yake na hawaheshimu watu wanaomzunguka.Ni mpayukaji.
Sasa kama Dr. Slaa hachaguliki kwa kundi kubwa la wapiga kura, woga wako wa nini ? Kama si mwadilifu kwa nafsi yake na hawaheshimu watu wanaomzunguka, hao wanahudhuria mikutano yake wanafuata nini ? Kwa nini mtu kama huyo asiye na elimu wala sifa , asiyechagulika na mpayukaji anakunyima usingizi, kwani atajichagua mwenyewe ?
 
Ushabiki umeanzia kwenye Avata no wonder ukawapendekeza JK NA LIPUMBA na kumuexclude Slaa.
Acha unazi wa kidini ingekuwa enzi za mwalimu ingebidi tukuogope kama ukoma
 
pole sana kwa kupotea kifikra binafsi tatizo sio kuwa na elimu ya uchumi peke yake bali tunahitaji kiongozi ambae atainua uchumi,huduma nyingine za jamii pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia.Na kuhusu Dk Slaa sio mlopokaji bali ni mtu mwenye uchungu na upoteaji wa rasilimali za taifa.Naungana na wewe sana kwamba Jk anjitahidi kutekeleza ahadi ila maswaiba wake ndio wanampaka matope.Upo hapo:dance:
 
Nakuunga mkono ndugu yangu kabisa naomba huyu bwana tumsaidie kumtoa kwenye itikadi za kidini
 
Hii response kwa Mtoka mbali kuwa "makeke yako ndio sifa za chama chako.Hamtufai.Tukiwapa nchi tutakuwa tukichapana chapana bila mwisho".
Rejea nilipo-bold. Wanajukwaa nataka kuwaonyesha tu kuwa lugha iliyotumiwa na mtoa hoja ni wazi kuwa si yeye anayefikiri na kujadili humu jukwaani bali kawakilisha mawazo ya wengine. JUKWAA hili si kwa watu wa kushikiwa akili.
 

Yaani ulivymuweka Kikwete ndo nakuona hujui kuchambua na hutaki kusema ukweli. Labda una agenda binafsi. Ni kweli Lipumba anaweza kufaa kama alivyo Slaa.

Elewa Pia Lipumba na slaa wasingefaa kama wangekuwa ni wagombea kwa ticket ya CCM. Read between the lines uelewe namaanisha nini.

Vile vile elewa kwamba Kwa mfumo huu tulionao ambao CCM inaukumbutia hata ukimleta OBAMA bado atakuwa anatwanga maji kwenye kinu.Ni kwamba tatizo la CCM sio kuwa na uhaba wa viongozi bora bali tatizo hasa ni mfumo wanaokumbitia ambao ndio unawafanya kuonekana kituko. Sababu kwa sasa kiongozi wao ni JK lawama zote anazibeba yeye.

Kwa hiyo kikwete amekuwa kichekesho zaidi sababu watanzania walikuwa na matumaini makubwa kuwa atabadilisha mifumo lakini mara baada ya kuingia ikulu kaona madaraka ni matamu, wajanja wamemdanganya utajipunguzia nguvu za kiutawala ukibadlisha mambo. Rais anayedanganyika kirais hafai.


  • Kwa nini kashindwa kufanya TAKUKURU iwe huru?
  • Kwa nini Serikali yake imewapeleka mahakamani maofisa wanashtakiwa kwa rushwa na bado anasimama nao kwenye majukwaa kuwapigia kampeni?
  • Kwa nini Hawaundi Tume Huru ya Uchaguzi
Hii ni mifano michache ya mifumo ambayo mfumo wake unamfanya mtawala yeyote awe na zigo kubwa

Kikwete anauma na kupuliza. CCM imejaa chui na kondoo. Na cha ajabu Kondoo wameanz a kula nyama kama chui.

Ningejaribu kukuelewa japo kidogo kama ungemlinganisha Lipumba na na Dr slaa lakini kwa kumuweka dr Jakaya kikwete tena ukamuweka nafasi ya pili unaonyesha jinsi gani umeweka ushabiki zaidi. na si ukweli

FACT ni kwamba CCM ni headache kwa watanzania. Mpaka hapo kiongozi 1ja atakapokuwa jasiri wa kubailisha mfumo.

FACT nyingine CCM kinaweza kuwa chama bora hata zaidi ya CUF na CHADEMA kikikaa nje ya Uongozi japo kwa miaka mitano. Kwa wanaoipenda CCM wasiwe waoga. Tuwaweke pembeni wajipange na kujipangua.they will come back not only stronger but they way wananchi wanavyotarajia.

Kikwete anauma na kupuliza. CMM imejaa chui na kondoo wanaoishi zizi moja kwa amani. Na cha ajabu na kushangaza Kondoo nao wameanz kula nyama kama chui. wananchi tumeshtuka hili zizi la CCM halifai
 

Ahadi za JK alizozitekeleza ni hizi hapa............................

 

Attachments

  • punda na watoto [800x600].jpg
    15.4 KB · Views: 50
Mimi nabisha Kikwete kuchaguliwa tena kuwa Rais. Uchaguzi ungekuwa kati ya vyama vya upinzani tu,kwamba watu waichague CCM ambapo hakuna mgombesa wa upinzani. Kuhusu wabunge ,sijapata muda kufikiria,lakini kuhusu Urais,Kikwete hafai kuwa Rais. Nyani ukimtazama usoni huwezi kumuua. CCM inapaswa kuondolewa tu bila huruma,kwa sababu CCM haijaoyesha huruma yoyote kwa wananchi.
Labda mimi ni biased kwa sababu sioni kwamba CCM imenisaidia kitu chochote,kwa sababu ninazo dollar mia tu katika account yangu ya CRDB.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…