Niwarudishie mkopo wao NMB au niondoke kimyakimya?

Niwarudishie mkopo wao NMB au niondoke kimyakimya?

benikiko

Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
15
Reaction score
0
Naomba niulize swali, nafanya kazi serikalini, kwa Bahati nzuri nimepata kazi nyingine ya private ambapo wananilipa vizuri na kwa mda huo nimechukua mkopo NMB na katika makato cjafikisha hata mwaka.

Je niwalipe pesa yao au niondoke kimyakimya?, je kuna madhara yoyote yatakayo nipata?.
Naomba ushauri wako.
 
chomoka kmykmy coz kwanza yale makato yako ya PSPF yata fidia,pili mndhamini wako ni mkurugenz.Mbona wengi tu wamechoka nao
 
Hata kama utaondoka kimya kimya hilo deni litalipwa na aliekua mwajiri wako,
Ndio maana lazima ktk mkopo uwe na mdhamini.
 
dhamana ni kwa mwajiri wako hiyo ambayo ni mkurugenzi mzee
 
Je nao wana tabia ya kuoneza riba kama wanavyofanya Standard Charterd benki. Maana wakija wanakulaghai kwa riba fulani say 19% baadaye kidogo wanakuja na hadithi kuwa gharama zimeongezeka na hivyo wanakwapua pesa yako zaidi wakati mwingine hadi 24% na hivyo kukukwamisha ktk malengo yako. Hivyo kama wanayotabia hiyo sepa kimya kimya kama hawana basi waeleze uendako watakupa utaratibu wa kulipa
 
Labda ukabidili jina huko unakoenda otherwise utalipa tu huo mkopo, labda mshahara usiwe unapitia benki ndo utasevu!!
 
Wakati unaomba mkopo ulikatwa bima, iyo bima ni kwa ajili ya maishu kama ayo, we chomoka kama Jay Mo, wameshakukata sana service charges mkuu na wewe haya ndo malupu lupu yako. Usiwe kama mbayu wayu changanya na za kwako
 
Kama ulipewa kwanini usilipe?,toa taarifa,wata clear mkopo kwa kutumia mafao yako ktk mifuko ya jamii ok,point to note mkuu:kuwa mwaminifu na taasisi za fedha utafaidika,tuache mawazo ya kitapeli tapeli shida cio ya siku moja!
 
Ingekuwa kwa wenzetu ningekushauri ulipe usije kujiharibia record zako, lakini hapa bongo we charaza lapa atajua mwajiri, pesa zenyewe za serkali hizo acha zikulipie bana wamezidi ufisadi na wewe ndiyo share yako hiyo! Nyie wafanyakazi hamna shida sana kama wajasiriamali, mjasiriamali sifa kubwa ni kurejesha mkopo kwa wakati ili kesho ukope mara mbili.
 
sepa haraka sana!! ila nasikia wanataka kuweka mfumo wakuwatambua wadaiwa wa mabenki!!!!!!!!!!!!! ila mpaka wakishtuka baadae sana!!!!!!!!!!!!!
 
wamekupa mkopo kwa vile ulikuwa na shida. sasa sa hivi umepata kazi kubwa unasahau kwa vile unahisi hela yako ya sasa itakutosha. lakini kumbuka you may need kukopa kwao siku za usoni. na hilo deni litakuwa limeongezeka zaidi ya hilo la sasa
sasa hivi kuna kitu kinaitwa credit reference bureau, taarifa zako zote za ukopaji na urejeshaji zinapelekwa huko kupitia central bank. kwa hiyo there is a chance that ukitaka kukopa mahali pengine your credit report itachukuliwa na utaonekana huna historia nzuri ya kurejesha mkopo na hiyo ni negative kwako
ushauri; kama deni lako ni kiasi ambacho unaweza kurejesha mara moja basi kalipe uachane nao, vinginevyo, wasiliana nao mkubaliane namna nzuri utakayotumia kupeleka marejesho yako
 
Credit reference bureau imeshaundwa na sasa wako katika kuweka kumbukumbu za wasiokopesheka.

Ukiwekwa kwenye hiyo black list, utakuja kujuta baadae.

Lipa mkopo, muogope haa mungu wako basi si unajua hizo pesa ni za depositors wengine?
 
Hembi niambie we unaimani ya Dini gani?

Na ukienda kanisani unapoinama kumuomba mungu unajua kwamba kuna dhulma umafanya na yeye anaijua na kila unapo sali wakati wa kula chakula unajua kwamba mungu anataka ule jasho lako la halali,na je unahisi kwamba dua ya mtu mwenye kula dhulma mungu anaipokea?jibu hapana,mungu anajua yaliyomo mioyoni mwetu,na wenye kumuhadaa kwa maombi yao yeye hujitenga na heri na baraka zote kwa watu hao,na pia huwaadhibu katika hali ambayo hawataitarajia na kuwadhalilisha hapa hapa duniani ili iwe mfano.

Ujana usikuhadae,lipa pesa za watu nautoe taarifa.
Dini zote zinasemakwamba dhulma ni mbaya sana na haina baraka kuanzia duniani na siku ya mwisho ndio mbaya zaidi.
Usifikire huko unakoenda kwamba ndio patakuwa salam kwa hilo,maana mungu anakuona na anaona dhamira yako moyoni.
Anaweza kukupa mtihani mkubwa kama adhabu juu ya hilo,tambua kwamba unahaki ya watu.

Mifano ipo mingi tu ya mwisho wa watu wenye kudhulumu,na siku hizi mungu hakopeshi,hapa hapa tu duniani tunaona watu wanavyoadhirika.Utapea kwa muda tu ila kuna muda utakumbuka comments zangu
 
This is what we call Real talk,shortcut is always a wrong cut.Mungu kakujalia hatimaye umepata kazi ya kipato kikubwa lakini bado unataka kufanya dhuruma.sio sawa mkuu,walipe tu
 
Ulikopa ukitarajia nini? We walipe tu. Vinginevyo jiandae maumivu mbeleni!
Hamisha malipo yako kwenye kazi mpya.
Uadilifu ni funguo ya mafanikio, acha ujanja ujanja!
 
Ingekuwa kwa wenzetu ningekushauri ulipe usije kujiharibia record zako, lakini hapa bongo we charaza lapa atajua mwajiri, pesa zenyewe za serkali hizo acha zikulipie bana wamezidi ufisadi na wewe ndiyo share yako hiyo! Nyie wafanyakazi hamna shida sana kama wajasiriamali, mjasiriamali sifa kubwa ni kurejesha mkopo kwa wakati ili kesho ukope mara mbili.

Soon Bank of TAnzania wataanzisha "Credit Reference Bureaus" ambazo zitakuwa na kazi ya kutoa information za mikopo ya wakopaji wa mabenki yote. watu kama hawa watajiharibia records ambapo akienda kukopa BAnk inachukuwa information kutoka CRD kuona kama mkopaji anakopesheka kama utakuwa na silika ya kutokulipa ndio hapo umejiharibia...

Muwe na mtindo wa kulipa mikopo muweze kukopesheka, ukikopa Mil 5 leo ukazilipa, ukakopa tena mil 8 kesho ukalipa umejiwekea record nzuri ya kuwa mlipaji mikopo mzuri ambae kesho na keshokutwa utakopa pesa zaidi na kupata maendeleao.

NAkushauri ulipe kwa kuwa sasa hivi Benki kuu inakusanya data za wakopaji wote. so ikifika wakati wa kuanza kutumia CRD utakuwa umeumbuka! TAnzania ya kikwete sio ile ya Nyerere!
 
we chapa lapa tu, mimi ninA RAFIKI yangu alichukua mkopo NMB na faidika na akachapa lapa, kilichofanyika hadi leo mshahara wake unatoka wenye meno wanaula palepale halmashauri na madeni yanaendelea kulipwa kila mwezi na salary slip ya kila mwezi tunamchukulia, huu ni mwaka wa tatu sasa
 
Back
Top Bottom