OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wakuu nataka kuwa moja kati ya wanaJF wenye nyumba kali. Hii ni idea ya kunipeleka huko. Hii ndio nyumba ya kudumu ya mkuu wenu itakayowekwa kwenye kiwanja cha mita za mraba 2,000. Inatakiwa kuwa nyumba kali kushinda zote pale. Iwe kali mpaka watu waseme nimejiunga Freemason, wazushe humo ndani nimevuga majoka. Kisha mimi niseme ni kwa neema tu za Bwana.
Nyumba inatakiwa kuwa bangaloo. Hizo picha mbili zinatakiwa ziungwe (merged) ili kuwa plan moja kali sana.
Pamoja na kuwa itakuwa ni single storey, sio ghorofa lakini inatakiwa kuwa ile upper canopy ya juu kwa ajili kutulia pale juu na kula mema ya nchi. Itafanyikaje,mimi sijui mafundi ndio wanajua.
Fundi mwenye uwezo wa kuweka hizo ideas kwenye ramani moja anakaribishwa tufanye biashara. Wakuu wa kutoa kasoro mnakaribishwa sana ili niweze kuwawakilisha wana Jukwaa la Ujenzi