UPDATES: 28 June 2012 - MALIPO YA AWALI KWA AJILI YA SHAMBA LILILOPO KATIKA KIJIJI CHA NALA:
Shamba nililopata katika kijiji cha Nala lina ukubwa wa heka mbili (2) na litagharimu kiasi cha Tsh. 1,500,000/=. Leo nimelipa malipo ya awali kiasi cha Tsh. 700,000/=, bado Tsh. 800,000/=. Malipo haya ya awali yametokana na mchango binafsi wa Tsh. 100,000/= kutokana na michango niliyopokea kutoka kwa jamii na kiasi cha Tsh. 600,000/= ni mchango binafsi.
Mkono wa Kulia; Mimi, Kutoka kushoto; Mzee Mosha akiandaa makubaliano ya kuuza shamba na kupokea malipo ya awali. Walioketi kwenye matofali; aliyevaa shati jeupe na kuwekewa mkono begani na bwana aliyesimama huyu ndiye mwenye shamba, Mzee Cheni na wengine ni viongozi wa Mtaa wa Nala.
Kulia; Bwana Mwinyi akipokea malipo ya awali kwa niaba ya mwenye Shamba Mzee Cheni (Hayupo katika picha hii)
NB: Katika mchanganuo wa mradi gharama za shamba nilikadiria kiasi cha Tsh.1,000,000/= kwa heka, lakini hapa nimepata heka 2 kwa Tsh. 1,500,000/=; niliamua kuchukua heka mbili kutokana na maoni ya wadau niliokuwa nakutana nao, kwani walishauri ni vyema kuchukua heka zaidi ya moja ili kuwe na eneo la ziada kidogo.
Nawashukuru wale wote waliotoa michango yao mpaka sasa na kuniwezesha kuchukua hatua za awali za utekelezaji, lakini bado naomba mchango wako ili niweze kutimiza ndoto hii.
Msaada: Kwa anayefahamu jinsi ya kukuza picha niomba anielekeze au kufanya hivyo; ningependa picha hizi kuonekana vyema.