Niwezeshe kutimiza ndoto yangu

Niwezeshe kutimiza ndoto yangu

Mkuu Mgombezi,
naona jina langu kwenye list ya waliochangia umelikosea.
Ni Muhinda sio Milinda.
nakutakia kila la kheri.

Samahani kwa kukosea jina na nashukuru kwa masahihisho; nitasahihisha.
 
Nawashukuru wale wote waliyopitia post hii ambayo niliweka hapa tarehe 3 June 2012, mpaka leo tarehe 28 June 2012; watu 1331 wameweza kupitia post hii, kati ya hawa nimepokea maoni 60 na nimepokea michango kutoka kwa watu 12 ambapo ni asilimia 1% kati ya waliopitia post hii.

niwezeshe.png

Jumla ya michango yao ni kiasi cha Tsh 120,000 ambapo ni sawa na idadi ya watu 24 kama kila mmoja angetoa kiasi cha Tsh 4970/= kwa kila mmoja, ambapo ni sawa na asilimia 1.8 kati ya waliopitia post hii. Nilikuwa nahitaji watu 1000 kuweza kunichangia kila mmoja kiasi cha Tsh 4970/= ili niweze kuanza mradi huu; hivyo basi kutokana na idadi ya waliopitia post hii na kama kila mmoja angeweza kuchangia ningekuwa nimepata kiasi kinachohitajika katika kuaza mradi huu, lakini naelewa dhamira ya mtu kuchangia inategemea na jinsi alivyopokea ombi hili na uwezo wa mtu biafsi.

Vile vile inawezekana kuna changamoto mbalimbali ambazo waliopitia post hii wamekutana kutokana na mazingira au utamaduni uliojengeka katika jamii yetu, ikiwa ni pamoja na: "Je huu sio usanii", kwani jamii imepoteza uaminifu kutokana na vitendo vya baadhi ya watu katika kujitafutia fedha kwa njia za udanganyifu. Naomba nihakikishie jamii kwamba nia ya dhati katika kutekeleza mradi huu ninayo na sio kwa manufaa yangu binafsi tu bali na kwa jamii kwa ujumla, kwa wale waliopo Dodoma na wangependa kufuatilia kwa karibu hatua za utekelezaji wa mradi huu wanaweza kuwasiliana na mimi na tunaweza kufanya ziara katika eneo husika.

Natanguliza shukrani kwa wale wote watakaoendelea kutoa michango yao na kuniwezesha kutimiza ndoto yangu, bado nahitaji wachangiaji 973 watakaoweza kunichangia kila mmoja kiasi cha Tsh. 4970/=.

NB: Ikiwa upo nje ya nchi na unahitaji kunichangia basi unaweza kuwasiliana nami au ni-PM na nitaweza kukupatia dola akaunti namba.
 
Hongera sana. Umefikia wapi na hii kazi? Nataka kuilima mipapai, nimeshaadaa kitalu cha miche.
 
hii sikuwahii kuiona aiseh kweli kufaa masikini ni ufala?? kama mpaka furusa kama izi tunafundishwa na namna yakuzipata na kufanya umu umu jf alafu bado mtu una shindwa kuamka na kufanya kazi .jf naipenda sana jamani aaaha?
 
Mkuu mgombezi najua ni wa Korogwe wewe!
Hongera kwa wazo la maana!!
 
Nimevutiwa na na huu mradi japo nilichelewa kuuona
Nina eneo kubwa dar la kuweza kukaa miche 200+ ila sijajua mbegu nzuri na changamoto

Huu uzi umeanzishwa 2012 naomba mrejesho kama ulifanikiwa au ulikwama wapi
 
Mgombezi kumbe alishafariki
Nimemua sana nimepiga simu katika number alizoandika hapo juu ndio akapokea mke wake na kunielezea huku akilia
R
I
P
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom