SoC02 Niwezeshe nikuwezeshe

SoC02 Niwezeshe nikuwezeshe

Stories of Change - 2022 Competition

Kaka Ibrah

Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
83
Reaction score
65
"NIWEZESHE NIKUWEZESHE " ni kauli mbiu ambayo inafaa sana katika kuhimizana sisi kwa sisi watanzania hasa zaidi ikiwa ni kwa upande wa wafanya biashara na wajasiriamali ikiwa ni pamoja na wateja.

Hapa nalenga kuzungumzia juu ya kipengele cha uchumi ikiwa na maana ya kwamba; Uchumi ni matokeo ya kiwango cha mapato yatokanayo kwa kufanya biashara, kwa kujishughurisha katika ujasiriamali na ajira. Uchumi waweza kuwa kwa mtu binafsi, kampuni, taasisi, shirika ama serikali. Lakini uchumi wa serikali (taifa ama nchi) hutegemea zaidi hasa katika ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wananchi wake. Vilevile pia serikali hukuza kiwango cha uchumi wake kutokana na rasirimali ilizojiwekea kama vyanzo vya mapato kwa taifa kama vile hifadhi za mbuga za wanyama, mito, bahari na maziwa.

Kiwango cha uchumi wa taifa hukuzwa na wananchi wake. Juhudi za wananchi katika kufanya kazi za kilimo,biashara, ujasiriamali na ajira ndio hupelekea kukua kwa uchumi ndani ya nchi. Mbali tu na uchumi kukua, pia hata urafiki baina ya watu ndani ya nchi utaweza kukua ikiwa tu hii kauli ya "niwezeshe nikuwezeshe" itatumika kwa matendo na kwa usahihi. Mfano; kama wewe ni mfanya biashara wa mazao ni lazima ukamnunulie mazao mkulima shambani (hapo tunasema kuwa umemuwezesha yeye kwa kumpatia pesa) na wewe hapo utakuwa umewezeshwa na mkulima kwa kupewa mzigo ambao utaupeleka sokoni na kujipatia kipato kwa faida. Kwahiyo mimi nikinufaika maana yake ni kwamba tunanufaika (tunanufaishana) wote, na hapa ndipo panakuwa ni mwanzo wa kuzikuza chumi zetu binafsi na uchumi wa nchi yetu kwa ujumla.

VIAZI LUMBESA.JPG

Chanzo cha picha; www.ippmedia.com

Kulingana na maelezo ya aya iliyo pita hapo juu mwisho wa siku tunagundua kwamba, ili kukuza uchumi wa nchi yetu, "tunahitaji tuwe na ushirikiano mwema sisi kwa sisi katika kazi zetu". Katika kushirikiana ni rahisi mtu kuweza kupata wazo jipya la kazi au la kibiashara ambalo kwa namna moja ama nyingine litaweza kumsaidia mtu kujikwamua kiuchumi na uchumi wa nchi yake.

Kuna njia mbalimbali ambazo mtu aweza kupata wazo au mawazo mapya ya kibiashara mbali na kukaa pamoja na watu, ambazo ni kama vile:

Kuzungumza na watu; hapa mtu huweza kujichanganya karibu na kila aina ya watu ndani ya jamii huku akifanya uchunguzi wa kibiashara kwa kuuliza maswali ya hapa na pale yahusuyo biashara ya aina yoyote ili ili mwisho wa siku aweze kufanya uchambuzi wa mawazo au wazo atakalo ona kuwa lafaa kwa ajili ya kuanzisha biashara ya aina flani.

Kutalii au kusafiri; kupitia kusafiri au katika kufanya utalii mahali flani, ni vyema kama mtu mwenye malengo ya kupaka kwa kipato ukawa mdadisi kwa kujaribu kuangalia je; kwa haya mazingira ni aina gani ya biashara ambayo inafaa kuwepo, na je vipi kuhusu changamoto zake, je faida zake ni zipi, na walengwa wa biashara husika watakuwa ni akina nani.

IMG_0009.JPG

Chanzo cha picha; issamichuzi.blogspot.com

Kuhudhuria katika semina za ujasiriamali;
kuhusu namna jinsi ambavyo mtu aweza kujiajiri binafsi, semina za ujasiriamali hutoa elimu za namna hiyo. Jambo zuri zaidi semina hizi hutolewa kwa gharama nafuu na wanafunzi huelekezwa kwa vitendo, kwa hiyo ni vyema kwa mtu anayetaka kukua kiuchumi kuhudhuria semina za namna hiyo.

ujasiriamali-1-768x512.jpeg

Chanzo cha picha; globalpublishers.co.tz

Kwa kusoma makala na machapisho mbalimbali mtandaoni;
kuna vyanzo mbalimbali vya habari mtandaoni ambavyo hujihusisha na kutoa elimu kwa watu (wasomaji) wake ili waweze kufahamu kuhusiana na mambo namna jinsi yanavyo kuwa hasa katika swala zima la biashara na ujasiriamali. Kwa mfano; jukwaa la JAMIIFORUMS lijulikanalo kama "Biashara, Uchumi na Ujasiriamali", likiwa limewalenga zaidi kuwapatia elimu wale wanaovutiwa na shughuri za kibiashara, uchumi na ujasiriamali.

I1fYPEtZ_400x400.jpg

Chanzo cha picha; jamiiforums

Baada ya mtu kuwa tayari amekwisha kupata wazo la kibiashara ni wajibu wake sasa kwenda katika jamii na kulifanyia kazi kwa ajili ya manufaa yake na taifa lake. Aidha kama ni wazo la biashara, kilimo ama ajira, vyema mtu akawajibike kwalo kwa ufanisi zaidi ili kubaki kuwa mshindi katika kazi yake.

Angalizo kwa biashara haramu; hizi ni biashara ama ajira zisizo faa wa kuruhusiwa na serikali ya nchi yetu, kwani huhatarisha usalama wa nchi na raia wake. Mfano wa biashara hizi ni uuzaji wa madawa ya kulevya, bangi, nakadharika. Wala biashara hizi hazimo katika orodha ya biashara zinazokubalika na serikali kufanywa na wananchi wake. Madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kudhuru afya ya binadamu. Hapa ningependa kuwashauri wananchi wenzangu kuwa tusije shawishika kujiingiza katika biashara za aina hii. Zipo ajira nyingi za kuajiliwa na za kujiajiri ambazo ni halali kwa kufanya tukaweza kukuza chumi zetu kama vile kilimo, ufugaji, ajira binafsi au ajira za serikalini ama katika kampuni flani, pia kuna biashara.

Lakini pia ni vyema tukumbuke kuwa uchumi hujengwa na aina zote za biashara isipokuwa biashara haramu tu. Na katika biashara hizi zipo biashara za viwango vya juu na biashara za viwango vya chini. Biashara za viwango vya chini ni kama vile machinga, kuuza mbogamboga sokoni, kutembeza vyakula mtaani kama vile sambusa, ubuyu, barafu, nakadharika. Malanyingi biashara kama hizi wengi wetu tumekuwa tukizidharau na kuwadharau wale ambao wamejiajiri katika biashara hizo, jambo ambalo tunakosea sana na kujikuta tukichelewa wenyewe kuyafikia malengo yetu ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi wa nchi yetu.

nairobi-109492_1920-1024x683.jpg

Chanzo cha picha; fififinance.com

Haifai kudharau kazi ndogondogo kwani nazo zinachangia kwa asilimia kadhaa katika kuukuza uchumi wa nchi yetu. Mfano; hebu jaribu kutazama taifa la China jinsi ambavyo limefanikiwa na kupiga hatua kubwa kiuchumi kwa kuthamini kila aina ya kazi hata kama ni ndogo kabisa tena yenye kipato kidogo. Hapa chamsingi ni kutambua umuhimu wa kila aina ya kazi hata kama ni ndogo kiasi gani, ili mladi tu iwe ni kazi halali. Kikubwa ni kwamba tunapaswa kuchakata mawazo ya namna jinsi ambavyo tunaweza kuziboresha biashara ndogondogo ili zikapata thamani kubwa zaidi na kutuletea mafanikio yenye tija katika maisha na jamii yetu.

Lakini pia serikali inalo jukumu la kutekeleza katika kukuza uchumi wa wananchi wake na taifa lake kwa ujumla. Je; ni kwa namna gani basi?; ni kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya namna ya mfumo wa ufanyaji wa biashara wenye tija, kwa kutoa ama kuendelea kutoa mikopo ya kifedha kwa wananchi wenye dhumuni la kuanzisha biashara. Kubwa zaidi ni kwamba serikali inatakiwa kufatilia maendeleo ya kazi ama biashara za wananchi wake ili kujua changamoto ziko wapi na iwapo kutakuwa na changamoto ambazo zinawakumba, basi serikali iweze kujua namna ya kuwasaidia watu wake kuweza kufikia malengo yao na hatimaye kuweza kupata manufaa ya kukua kwa uchumi wa nchi.

emblem.png

Chanzo cha picha; www.tanzania.go.tz

Hivyo basi; litakuwa ni jambo jema kama tukipendana sisi kwa sisi, maana katika kupendana ndipo tutaweza kuwezeshana (yaani kuungishana) katika mambo mbalimbali ya msingi ya kibiashara, kilimo, ajira na hata katika mambo muhimu ya kijamii. Hii itatuwezesha kukua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na nchi yetu yote.


Shukrani za dhati kwa kila mmoja, nawasilisha.
 

Attachments

  • emblem.png
    emblem.png
    41.5 KB · Views: 7
Upvote 1
Back
Top Bottom