Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,125
- 1,435
Duuh! Sasa hiyo inatisha mazee kwa sababu kama hiyo ndio kanuni basi ina maana sisi wabongo wote ni mafisadi na hamna hata mmoja wetu/ wachache ktk watu milioni 40 ambao si mafisadi. Bora lipi? Kuwaondoa mafisadi waliokwishatuthibitishia ufisadi wao au kuwaacha waendelee kutawala kwa vile tu watakaowarithi nao wataishia kuwa mafisadi? Bado sijakata tamaa kuwa hatuna watu wasafi wasio walafi.
Nyani, hoja yangu ya msingi ni kuwa misingi mibovu ya "superstructure" tulizonazo ndizo zinazochochea huu ufisadi. Hakuna mtu aliyezaliwa na chapa ya ufisadi usoni. Ni mazingira ndio yanamfanya mwanadamu kujikita kwenye ufisadi. Pamoja na pressure tunayotoa sasa hivi kwa hawa jamaa kuachia ngazi, hata wengine watakaoingia serikalini bado wataendeleza ufisadi. Maana kichaka bado hakijabadilika. Tunahitaji kutia kiberiti hicho kichaka ili mafisadi waonekane waziwazi--mabadiliko katika hizo superstructures. In the shortrun, ni kuwatimua hawa mafisadi. However, in the medium term, overhaul ya superstructure ni muhimu.
Naomba kuwasilisha.