Mtanzania mara nyingi mimi huwa natofautiana na baadhi ya watanzania wenzangu kuhusu hawa wazungu(pamoja na Kina Condi na Powell). Ukiangalia wakati wa ukoloni, wizi wa mkoloni uliokuwa wazi kabisa na wakutumia mabavu, kejeli na dharau utaona kuwa watanzania walikuwa na ahueni fulani, wale waliokuwa wakifanya kazi japo kazi ya ushambaboy walikuwa na maana(yaani kipato chao kiliweza kuwafikisha hata next month, Ukiangalia Dar es salaam(Tanzania) ya mkoloni ni much much better, safer, arranged kwa mambo mengi sana kuliko Tanzania ya CCM, hapa maana yangu ni kuwa mkoloni mweupe alikuwa afadhari kuliko huyu mkoloni mweusi tuliyemkubali.
Angalia shule, hospitali, barabara, nyumba au hata ofisi zinazotumiwa leo na serikali alizojenga mkoloni, linganisha na walizojenga mika kumi iliyopita halau uniambie who did good job.
Kuna wakati bado tunakuwa na stigma ya mtu mweupe kutokana na mbegu tuliyopandikizwa tukiwa watoto kuhusu mzungu/mkolonni, lakini mwizi wa siku hizi ambaye ni worse inaonekana kuwa tuna mkumbatia. Mimi naona kwa kiasi fulani hao jamaa wana haki ya kutusaidia kuamua kwa sababu inaonekana wazi kabisa kuwa sisi tumesghindwa kuamua, hata tukipewa pesa za kutusaidia tunashindwa kuzitumia badala yake tunazirudishwa kwenye akaunti zao za huko Ulaya. MImi naona wana haki, what do you think, au unaonea ni bora turudi kwenye sera ya Ujamaa na Kujitegemea na tufunge mlango kabisa, no money from outside no word or order from outside? Is that what you are suggesting?!