Kiungo Haruna Niyonzima ametua Dar usiku na taarifa za ndani zinasema baadhi ya mashabiki wa Yanga walikuwa wanamsubiria kumfanyia vurugu. Jamaa unaambiwa aliwakwepa na kuwaacha kwenye mataa.
Niyonzima sasa yuko tayari kujiunga na kikosi baada ya kuwasili usiku.
Niyonzima ambaye aliendelea kubaki kwao Kigali amewasili na kupokelewa na viongozi wa Msimbazi tayari kuanza kazi.
Nguvu zote zinaelekezwa kwa Simba ni kesho kwenye Tamasha la Simba Day wakati atakapotambulishwa rasmi.