Niyonzima: Natamani niwafunge Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Kiungo wa kimataifa wa Klabu ya Simba Haruna Niyonzima amefunguka na kudai haikuwa jambo rahisi kwa yeye kutoka Yanga kwenda kuchezea Simba ila anamshukuru Mungu kwa kuwa yeye ndiyo mpangaji wa kila jambo.

Niyonzima ameeleza hayo muda mfupi ulipomalizika mtanange wao wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports FC ya Rwanda.

"Siyo rahisi kutoka Yanga kwenda Simba au kutoka Simba kwenda Yanga lakini yote ni maisha. Naamini kuna wanayanga pamoja na mashabiki wangu wameumia kuniona mimi nacheza Simba lakini niseme kwamba yote ni maisha kwa sababu mimi ni mchezaji wa mpira siwezi kujua nitaishia wapi, kikubwa ni kuifanya kazi yangu", amesema Niyonzima.

Pamoja na hayo, Niyonzima ameendelea kwa kusema "Niishukuru timu ya Yanga unajua ni timu ambayo mpaka sasa hivi nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani 'so' ni kitu cha kuwashukuru nimeishi nao vizuri. Najua katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga haitokuwa mechi rahisi ila natamani japo niwafunge goli ili niwaage kwa heshima".

Kwa upande mwingine, Niyonzima amesema yeye binafsi hakuwa na ndoto za kucheza soka nchini Tanzania ila mipango ya Mungu ndiyo imemfanya awe hapo

Chanzo: EATV
 
hahaha manara ana kiraru raru hapo pichani
ndala sijui
 
Yanga anachukua ngao ya jamii acha yeye afunge ajifurahishe
 
Amesahau alipotoka lakini mpira ndio kazi yake yuko sahihi.
 
Niyonzima anafanya mzaha sana ,,,,,,,sisi tumemlea sana
 
hivi hii taarifa inahusu nchi gani vile?
 

Haruna Niyonzima

Haruna Niyonzima ambaye ni mchezaji mpya wa klabu ya soka ya Simba SC aliyekuwa akicheza kwa mahasimu wao Yanga, amefunguka maneno ambayo yanaonekana ni kama madongo wa watu wanaomchukia kwa sasa.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Rayon Sports ya Rwanda, mchezaji huyo amesema hakuwahi kuwa na ndoto za kuja kucheza Tanzania lakini mpira ndio kazi yake na kazi ni sehemu yoyote hachagui.



“Yanga wameumia na nini, wapenzi wa Haruna lakini mimi niseme yote ni maisha na mimi ni mchezaji wa mpira siwezi kujua nitaishia wapi lakini kikubwa ni kufanya kazi yangu. Pia nawashukuru Yanga ni timu ambayo mpaka sasa hivi nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani, ni kitu cha kuwashukuru nimeishi nao vizuri mashabiki, wana Yanga, wapenzi wa Haruna ambao walikuwa wanampenda akiwa Yanga na watu wote ambao wameni support nikiwa Yanga,” amesema Niyonzima.

“Wamenionyesha ushirikiano lakini Mwenyezi Mungu anakuwa na mambo yake mengine, nimekuja Simba na ninaamini nimekuja kufanya kazi. Mimi niseme kuwa sikuwa na ndoto za kucheza Tanzania lakini Mwenyezi Mungu ndio anajua wapi mtu ataenda mimi sioni tatizo ni kitu tu cha kushukuru kwa sababu kila kitu kinapangwa na Mungu na hii ni kazi unajua kazi ni sehemu yoyote, mimi naomba Mwenyezi Mungu anibariki niweze kufanya kazi zangu vizuri tu basi,” ameongeza.

“Mimi naamini tukifanya kazi kwa ushirikiano tukawasikiliza walimu na sisi wenyewqe tukapendana kwa sababu tunawatu wenye experience ni watu wakubwa, watu wazima ambao tukiamua hatuwezi kukosa pointi tatu naamini tutakuja kufanya vizuri zaidi.”

Niyonzima amesisitiza kwa kusema kuwa anatamani kufunga goli katika mechi ya Ngao ya Jamii ambayo itachezwa August 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa ili aweze kuwaaga watu wa Yanga vizuri.

Nitawawekea michoro ya kisayansi ya ''rula'' alizokuwa akipiga Niyo pale Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…