GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Tukiwa tunawaambieni kuwa mna njaa halafu hamna 'wataalam' wa mpira katika klabu yenu ya Yanga muwe mnatuelewa kwani ni aina yenu ya 'ubishi' ndiyo ambayo imekuwa 'ikiwagharimu' na hatimaye mnajikuta mnafanya vibaya katika mechi zenu mbalimbali kisha mnadai Simba SC inabebwa wakati si kweli.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa huku wakijua kuwa Jumapili ijayo tarehe 27/10/2019 wana mechi ngumu na muhimu sana ya kimataifa, leo klabu ya Yanga imepata 'pigo' kubwa baada ya mchezaji wao ambaye ni mshambuliaji mzuri na 'tegemeo' Kalengo kuumia vibaya wakati Yanga ikicheza mechi ( isiyokuwa rasmi ) na klabu ya Pamba, hivyo kupelekea mchezaji huyo ambaye ni hivi juzi tu ametoka kuwa 'majeruhi' kurejea tena huko huko ambako sasa atakaa nje kwa wiki kati ya 8 hadi 12.
Na inasemekana moja ya sababu kubwa iliyopelekea Yanga SC leo kucheza hiyo mechi (isiyokuwa rasmi ) ni kupata pesa kidogo za kununua chai, vitafunwa na vyakula kwa wachezaji wao huku hela nyingine ikitumika kwa kukodi gari la kunyonya 'kinyesi' katika hoteli waliyofikia hapo mkoani Mwanza ambayo huwa yanajaa kwa haraka kwani hali ya maisha hapo kambini 'kiuchumi' ni mbaya sana.
Yaani una Mechi 'ngumu' na 'Mwarabu' kutoka nchini Misri, Pyramids, badala ya kuwalinda ' wachezaji wako ili wasipate majeraha kuelekea huo mchezo wewe unaendekeza njaa njaa zako kwa kucheza mechi za 'ndondo' ambazo hata kocha mkuu hakutaka ila mmelazimisha tu kwa 'ubabe' wenu kama viongozi na sasa mumempoteza mchezaji wenu muhimu ambaye nina uhakika angekuwepo Jumapili angalau angeweza kuwabebeni na mkabahatisha kushinda.
Ila habari za chinichini zinadai kwamba huyu mchezaji Kalengo anaumizwa 'kiuchawi/ kindumba' na mshambuliaji Mkongo wa Yanga SC, David Molinga, na kwamba hili hata viongozi waandamizi baadhi wanalijua ila wamegawanyika katika kulikabili na kulitatua kwa haraka. Na si kwa huyu tu, bali pia kuna malalamiko hasa kwa wachezaji wa kigeni kuwa hapo Yanga 'wanaumizana' mno kiushirikina, hali ambayo inaweza ikaathiri mwenendo mzima wa klabu/ timu.