Njaa mbaya, nimeangalia salio leo si chini ya mara 25, hadi nahisi nitatumiwa SMS ya onyo kutoka benki

Mwanangu nashangaa wamekuwa wagumu sana. Sielewi kwanini

Mkuu, hivi unajua crdb kuna limit ya salio?
Kwamba ukikomba ulichonacho, ikifika nadhani ni buku 9 au 10, huwezi kuitoa!
Sasa unavyoangalia salio, inakatwa hiyo!
Lakini pia kadri unavyozidi kuangalia salio inavyoendelea kupungua, kuna wakati salio inafikia linasoma negative! Acha zile ada za kila mwezi, hivyo siku hela ikiingia si ajabu ukafyekwa hata elfu 8...

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wakuu ngoja twende kwenye mada,

Ndani ya miaka miwili yenye miezi 24 na ushehe mwezi huu nimepigika sana kuliko miezi mingine nadhani ingawa sina kumbukumbu sahihi.

Sasa kuanzia jana kuna fedha niliitazamia kuangia kwenye account yangu ya CRDB, jana ikapita patulo yaani kappa, leo kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa na mbili jioni hii nimecheki salio si chini ya mara 25 bilabila. Ila mzigo leo lazima uingie.

Nikimaliza kuandika hapa nacheki tena maana si kwa kufulia huku.

CRDB chondechonde msinipige ban
Jiunge na SIM banking
Salio likiongezeka kwenye account unatumiwa meseji ya notification
 
Nilikuwa nacheki kupitia sim banking na CRDB app. Lengo halikuwa kujua kama kuna nyongeza Lengo ni kuona salio na kwenda kutoa. Halafu sms za alert wakati mwingine hazifiki kabisa au huja kwa kuchelewa
 
Mkuu, hivi unajua crdb kuna limit ya salio?
Kwamba ukikomba ulichonacho, ikifika nadhani ni buku 9 au 10, huwezi kuitoa!
Sasa unavyoangalia salio, inakatwa hiyo!
Lakini pia kadri unavyozidi kuangalia salio inavyoendelea kupungua, kuna wakati salio inafikia linasoma negative! Acha zile ada za kila mwezi, hivyo siku hela ikiingia si ajabu ukafyekwa hata elfu 8...

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mzigo umeingia ila wamenifyeka. Kweli hakuna free lunch Africa
 
Hali imekuwa ngumu sana huyu jamaa anawakilisha kundi la watanzania ambao wanapoteza matumaini usikute njaa ndio inampa msukumo kila saa aangalie salio
 
Anayebisha huwezi kuangalia salio bure hayupo sahii kwa sababu;
Ukiwa na salio ukiangalia salio utakatwa 350.
Ukiwa huna salio, hata uangalie mara 1000, utajibiwa You do not have enougha fund. Please fund your account and try again.
Salio likishaingia, kuna msg ya faraja sana huwa inaandika
Dear MR EASY PUNTER Your balance is TZS 825000 (huo ujumbe utakatwa 350 na kwa kweli huwa una faraja ya hali ya juu sana hasa kama ushaangalia salio mara 50)
 
😀
 
Back
Top Bottom