Jimbo la Hai, ambalo ni Jimbo la kimkakati kwa CCM, lina changamoto kubwa sana za kijamii na kimaisha.
Miongoni mwa changamoto zilizopo ni miradi isiyotekelezeka na ahadi ambazo hazitimizwi na mbunge wa Jimbo hilo.
Kwa mfano, ujenzi wa masoko mbalimbali ni ahadi tupu tu.
Kuhusu ujenzi na ukarabati wa jengo la ofisi ya CCM wilaya, wanaccm wamemsukuma mbunge kwa miaka mitano lakini bado hakuangalia jambo hilo.
Zaidi ya hayo, wanaccm wamechangia fedha lakini vifaa vya ujenzi havijulikani vilikwenda wapi.
Leo mbunge anatutaka tumpige tena kura, huku akishindwa kuunda chama na kujenga ofisi ya chama wilaya.
Hakuna vikundi vya vijana, hakuna ajira, hakuna miradi ya vijana, bado anawakataa madiwani na kusema yeye atachaguliwa tena.