Pre GE2025 Njaa ni mbaya sana: Mbunge amepitishwa, madiwani watasubiri taratibu za kiserikali!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jimbo la Hai, ambalo ni Jimbo la kimkakati kwa CCM, lina changamoto kubwa sana za kijamii na kimaisha.

Miongoni mwa changamoto zilizopo ni miradi isiyotekelezeka na ahadi ambazo hazitimizwi na mbunge wa Jimbo hilo.

Kwa mfano, ujenzi wa masoko mbalimbali ni ahadi tupu tu.

Kuhusu ujenzi na ukarabati wa jengo la ofisi ya CCM wilaya, wanaccm wamemsukuma mbunge kwa miaka mitano lakini bado hakuangalia jambo hilo.

Zaidi ya hayo, wanaccm wamechangia fedha lakini vifaa vya ujenzi havijulikani vilikwenda wapi.

Leo mbunge anatutaka tumpige tena kura, huku akishindwa kuunda chama na kujenga ofisi ya chama wilaya.

Hakuna vikundi vya vijana, hakuna ajira, hakuna miradi ya vijana, bado anawakataa madiwani na kusema yeye atachaguliwa tena.
Haya unayosema yote siyo kazi ya mbunge. Mbunge kazi yake ni kuisimamia na kuiongoza serikali na kutunga sheria. Unatakiwa useme kuwa bungeni hafanyi hizo kazi.
 
Mbunge, Kama mwanachama wa chama, anaweza kushiriki katika shughuli za chama bila kuathiri wajibu wake kwa wananchi, lakini kuna baadhi ya mambo ya kuzingatia:

1. Mipaka ya ushiriki: Mbunge anapaswa kuwa mwangalifu asije akajihusisha sana na shughuli za chama hadi kushindwa kutekeleza majukumu yake bungeni.

2. Uwazi na uwajibikaji: Mbunge anapaswa kuwa wazi na wananchi kuhusu ushiriki wake katika shughuli za chama ili kuzuia mgongano wa maslahi.

3. Kipaumbele: Wajibu wa mbunge kwa wananchi wake ndio kipaumbele cha kwanza. Shughuli za chama zinapaswa kuwa sekondari.

4. Usimamizi: Mbunge anapaswa kuzingatia kanuni na taratibu za bunge ili kuhakikisha ushiriki wake katika chama hauathiri utendaji wake wa kiutawala.

Kwa ufupi, mbunge anaweza kushiriki katika shughuli za chama kama mwanachama, lakini anapaswa kuwa mwangalifu asije akajikuta akifanya hivyo kwa kiwango kinachoathiri wajibu wake kwa wananchi.
 
Nakubaliana na wewe kabisa.
 
Tanzania kubwa hii nipo wilaya moja huku kanda ya ziwa kwa sasa kuna sehemu diwani ndie pia mwenyekiti wa kijiji yaani mtu mmoja ana hizo kofia mbili hili limekaeje wajuvi?
 
Back
Top Bottom