Njaa ni nini?

Mpondoshilla

Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
36
Reaction score
132
Kwa wale msioijua njaa ikoje

Njaa ni kitendo cha kukaa muda mrefu bila kula huku ukiwa hujui utakula nini na ni wakati gani

Hiyo ndo inaitwa njaa,

Achana na hizi njaa ndogo ndogo
 
Eti mtu ana hela sema kaona uvivu kwenda nunua msosi analalamika njaa.

Ishawahi niuma njaa kama 6 days sili msosi wa kueleweka nikamkuta mshikaji anakula muhindi wa kuchoma njiani (mkoani njombe huko) nikamuomba na akanipa.

Kuna siku nina njaa natembea from ubungo to Mbagala Kongowe nikamkuta jamaa amekaa pembeni ya roli hafu ana maji uhai lita moja kapiga nusu nikamfuata nikamsalimia kistaarabu nikaomba maji akanipa.

Kuna siku nilikuta washikaji wanachimba mtaro wa kupitisha nyaya za internet nadhani mkoani iringa/mafinga sasa wakawa break wanakula ugali na maharage nikaenda nikazuga naomba maji ya kunywa wakasema karibu tuliunge aisee nilikula knm kwasababu uhakika wa kula kesho yake nilikua sina.

Na chuo aisee hahahaa chuo anajua Mungu tu ngoja nikaushe vyuoni kuna siri nyingi sana.
 
Eti mtu ana hela sema kaona uvivu kwenda nunua msosi analalamika njaa.

Ishawahi niuma njaa kama 6 days sili msosi wa kueleweka nikamkuta mshikaji anakula muhindi wa kuchoma njiani (mkoani njombe huko) nikamuomba na akanipa....
Pole mkuu mimi ilinikuta kigoma sina mwenyeji nikakomaa siku nzima nakunywa maji we tumbo likaanza kuuma nilikutana na muhogo umetupwa mbichi, mbona niliushangiliaa
 
Mim nikiwa na hela tu sisikii njaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nikiwa sina hela hata kama chakula kimo ndani uwiii njaa kali balaa
 
Acha na njaa Mzee.

Nilipokua chuo ilikua kila nikiamka sijui nakula Nini basi unajikuta unashinda mpaka jioni ndo napata rizki..mlo mmoja kwa siku.

Kuna kipindi nilikopa mgahawani hela ikifika 50k+ basi nikaenda Tena Yule mama alinifokea kishenzi na kuninyima msosi nikaondoka ilikua asubuhi...jioni nikarudi Tena pale pale kula sina kitu mfukoni ilibidi acheke tu Yule mama akanipa msosi baada ya wiki nikapata pesa nikalipa Deni lote.

NB:ukiwa na njaa aibu huondoka na kwenye Maisha Mungu atakunyima vyote Ila sio kula,,kula utakula tu hata kwa kuchelewa.
 
Sawa, unaonekana mtu wa kuombaomba sana , kuwa makini Kuna mamende mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…