Mangi Moshi
Member
- Jun 21, 2011
- 22
- 11
Hivi jamani ni kwa nini Mabinti/Wasichana huamini kuwa rafiki wa Kiume ni mtu wa kupigwa Mizinga kwenye kila kitu, kuanzia vocha, simu, mavazi, shida zingine za uongo, n.k? Ni kwa nini ukitoka naye anaagiza vitu vya thamani wakati hajui ulicho nacho mfukoni na wakati huohuo mfukoni anakuwa hana fedha za kutosha anachojigharamia? Utasikia niletee Savannah/Heineken/Miller/Serengeti Ndogo. Niletee Chips na nusu Kuku halafu weka na mayai mawili. Utadhani ndo siku mwisho kula. Hivi hawa watu hawana mawazo ya savings/maendeleo? Wanafikiria leo hapo mezani tu? Na ndo maana jamaa wengi huishia kula mara moja, ya pili ni kwa nadra sana.