The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Daudi Silanga, ameweka wazi mafanikio makubwa ya maendeleo katika wilaya hiyo, akieleza kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta shilingi bilioni 85 kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Itilima uliofanyika Uwanja wa Stendi, Kata ya Lagangabilili, siku ya Jumamosi Februari 15, 2025, ambao Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye mgeni rasmi, Silanga amesisitiza kuwa fedha hizo zimewezesha utekelezaji wa miradi muhimu kwa wananchi kwa usimamizi wa Mkurugenzi wa Halmashauri na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Kwa upande wa sekta ya afya, Silanga amesema Serikali imepeleka zaidi ya shilingi bilioni 6 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya. Fedha hizo zimejenga zahanati mbalimbali wilayani humo huku ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ukiendelea kwa viwango vya juu. Amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya afya kwa kuleta zaidi ya Shilingi bilioni 6.3 zaidi kwa ajili ya huduma bora za matibabu kwa wananchi wa Itilima.
Silanga ameeleza kuwa tangu alipoingia madarakani, idadi ya shule za sekondari katika wilaya hiyo imeongezeka kutoka shule 89 hadi 108, hatua inayosaidia watoto wa Itilima kupata elimu bora.
“Tumejenga shule za kisasa za sekondari katika maeneo mbalimbali ya wilaya hii. Hizi ni fedha za Serikali ya CCM zinazosimamiwa na Rais Dkt. Samia, na ndizo zitawajengea vijana wetu ujuzi wa hali ya juu ili wawe wahandisi, marubani na wataalamu wa kuendesha mitambo,” amesema Silanga.
Mbunge huyo amewataka wananchi wa Itilima kuendelea kushirikiana na Serikali katika kusimamia miradi hiyo kwa maendeleo endelevu ya wilaya hiyo.
Pia soma: Pre GE2025 Naibu waziri maji: Ukituma mbunge anayekubalika kwa mawaziri miradi ya maendeleo itajazana jimboni kwako