Zanzibar 2020 Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi

Kukosea tarehe ndio itunyime kumpata Rais bora.. mbona watanzania tunakua wehu kiasi hiki.

Kama terehe imekosewa inarejebishwa na mambo yanaendelea...
Umeongea vyema sana, kule Bungeni ambako tulihitaji watu wasomi watunge Sheria na wasimamie serikali eti " wanapaswa kujua kusoma na kuandika" wengine husimama na kushindwa kusoma kwa ufasaha lakini ni viongozi.

Leo hii kukosea tarakimu moja watu wanaona nongwa sana. Kwann wasisahihishe? Tarehe sio issue ya msingi, cha maanani ni taarifa za muhusika zipo sahihi?
 
Kuna wagombea ubunge wa ACT waliandika jina la chama kama Maalim hapo "ACT Wazalendo". Wameenguliwa kwa kutokuweka "-" yaani "ACT-Wazalendo". Naona Maalim naye hakuweka hako ka-. Yaani hata mimi mkulima nilikwishajua kuwa kutokuweka hako ka - inaweza kuwa nongwa. Maalim bado hajajua tu?
 
Tena ukiangalia ni mgombea mwenye uzoefu aliekuwa Makamu wa Rais.
 
Viongozi wangu wa upinzani. Mkishajua kuwa mnatafutwa kwa udi na uvumba, punguzeni sababu za shetwani kuwavamia. Naona hata mwandiko wa mwapishwaji na mwapishaji uko sawa. Fomu imejazwa pote na mtu mmoja. Wino tu wa kalamu ndio umebadilishwa (mweusi na bluu). Maalim hawezi kujaza fomu mwenyewe ili kuepusha uwezekano wa "kuuzwa"?
 
Kiapo chake ametia saini 07/07/2020 ambapo tume ilikuwa bado haijatoa fomu!

Unasoma kiapo kipi wewe?

Ni hiki ambacho kiko scanned hapa au unacho chako kingine?

Hiki tarehe inasomeka vizuri kabisa kuwa ni 07/09/2020...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…