GE2025 Njau: Tukampige kura Samia Oktoba ili tumdai haya aliyo tuahidi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mbunge wa Viti Maalum mstaafu kupitia CHADEMA, Felista Njau, ameendelea na mbinu yake ya kampeni kwa kuingia moja kwa moja sokoni badala ya mikutano ya hadhara, akiwahimiza wananchi kumpa kura ya urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao wa Oktoba 29.

Akiwa katika Soko la Kiboriloni, Njau aliwaambia wafanyabiashara na wananchi waliokusanyika kuwa Rais Samia amejidhihirisha kwa miaka minne
iliyopita kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kusukuma mbele maendeleo ya taifa.

"Tumeshampima, ametufaa. Ndio maana ninawaomba tumpe ridhaa ya muhula mwingine ili aendelee kuongoza taifa letu," alisema Njau, akisisitiza kuwa uongozi wa Samia umeonyesha dira, mshikamano na matokeo ya kweli kwa wananchi.

Njau pia aliwaeleza wafanyabiashara wa Kiboriloni kuwa Rais Samia amekuwa msitari wa mbele kuboresha mazingira ya biashara ndogondogo, sekta ya afya na elimu, akiongeza kuwa siku 100 za mwanzo za muhula wake mpya zitakuwa na mageuzi zaidi.

Wananchi waliomsikiliza sokoni walipata nafasi ya kueleza changamoto zinazowakabili, ikiwemo miundombinu ya soko na upatikanaji wa mitaji nafuu. Walibainisha matarajio kwamba iwapo Samia ataendelea kuongoza, maboresho hayo yatawafikia moja kwa moja.

Ameshindwa miaka 5 ,BIMA saizi hakuna,tozo ukiuliza unatekwa na unaambiwa uende Burundi...kipiga Kura ni kupotezaa muda wako
 
Mbunge wa Viti Maalum mstaafu kupitia CHADEMA, Felista Njau, ameendelea na mbinu yake ya kampeni kwa kuingia moja kwa moja sokoni badala ya mikutano ya hadhara, akiwahimiza wananchi kumpa kura ya urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi ujao wa Oktoba 29.

Akiwa katika Soko la Kiboriloni, Njau aliwaambia wafanyabiashara na wananchi waliokusanyika kuwa Rais Samia amejidhihirisha kwa miaka minne
iliyopita kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kusukuma mbele maendeleo ya taifa.

"Tumeshampima, ametufaa. Ndio maana ninawaomba tumpe ridhaa ya muhula mwingine ili aendelee kuongoza taifa letu," alisema Njau, akisisitiza kuwa uongozi wa Samia umeonyesha dira, mshikamano na matokeo ya kweli kwa wananchi.

Njau pia aliwaeleza wafanyabiashara wa Kiboriloni kuwa Rais Samia amekuwa msitari wa mbele kuboresha mazingira ya biashara ndogondogo, sekta ya afya na elimu, akiongeza kuwa siku 100 za mwanzo za muhula wake mpya zitakuwa na mageuzi zaidi.

Wananchi waliomsikiliza sokoni walipata nafasi ya kueleza changamoto zinazowakabili, ikiwemo miundombinu ya soko na upatikanaji wa mitaji nafuu. Walibainisha matarajio kwamba iwapo Samia ataendelea kuongoza, maboresho hayo yatawafikia moja kwa moja.

😁😁🤣
 
Wana Chadema humu mbona mumeupita uzi huu!!!!
Mwenzenu huyo mumshangilie au kajipachika kwa chama chenu bila nyie kujua 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom