Nje ya 18- Simba vs AS Vita

Nje ya 18- Simba vs AS Vita

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
NJE YA 18- SIMBA VS AS VITA

THADEO LWANGA, anaweza kuwa Mwami kutoka Kigoma kwanini asiwe mtu kutokea huku kama anaweza kuwa na nguvu kama Hawafu, nusu ya chini ni eneo lake ameamua kulimiliki, anakaba atakavyo, anascan back four awezavyo ndie mapafu ya mbwa kwenye mfumo wa Simba

AISHI MANULA, Mtuwa kutoka Morogoro na mikono yake salama, kupiga langoni ni kitu kingine, kufunga langoni ni kitu kingine, namwona Aishi kwenye fikra za Isaac Newton, "Two every Manula there is equal and oppy Aishi", mechi nyingine bora sana leo langoni Homeboy.

Kwenye kitabu cha simulizi nzuri msimsahau Mchizi ZEMANGA SOZE wa AS VITA, anacheza na kufurahisha, mpira ukifika kwake ni kama Padre kwenye Altare, pass anaitoa kama Mtumishi na Chetezo, mamlaka yake uwanjani ni kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei pale Kanisani, what a man.

CLATOUS CHAMA, THE FOOTBALL TCRA, yeye ndie Mamlaka ya Mawasiliano ya Simba, yeye ndie anaitafsiri akili ya Mwalimu Gomez, yeye ndie muamuzi wa mwisho kwenye eneo la mwisho, ataamua yeye wapi apeleke mali na wapi panalega lega, Simba ni Chama.

JOASH ONYANGO, ananikumbusha simulizi za Franco Baressi, ananikumbusha dunia ya Paolo Maldini, ananikumbusha maana halisi ya beki wakati, ule mnyororo pale nyuma ni yeye, ile nguvu ya ubora kwenye PPDA ni yeye, ipo siku tutazungumza kuhusu Passes per defensive reaction, Onyango what a man.

LUIS MIQUISSONE, Wacha inyeshe tuone panapovuja, hii ndio marking scheme ya makipa wote Afrika, hii ndio marking scheme ya mabeki wote Afrika, huwezi kuwa bora kama hujapita kwenye miguu yake, ubora wako utategemea na Luis Miquissone.

MOHAMMED HUSSEIN, niliwahi kusikia kuhusu Upinzani, niliwahi kuambiwa kuwa tunakosoa sana na hatuna jina mbadala kwenye eneo la beki wa kushoto, Kuna mbadala wa Mohamed? Basi leteni jina tulijadili, kuna beki wa kupanda na kushukua kwa usahih zaidi yake? Basi eleteni jina tulijadili.

RALLY BWALYA, THE FOOTBALL MAESTRO, Nisamehe kwakuwa unacheza bila kuwa na Luka Modric pembeni yako, tusamehe kwakuwa mbele yako hayupo Cristiano Ronaldo, Kiungo halisi wa mpira aliepaswa kuzibariki nyasi za Camp Nou na kuzpiga pesa za Sheikh Mansour pale Man City, brilliant.

KAMA MMETUSHINDWA SEMENI MSAIDIWE [emoji3]

jr_farhanjr-___CNNYbWjL__X___-.jpg
 
Chris Muga mnamuonaje,anakosa magoli lakini anavitu gani vinayotuletea faida kutoka kwake?
 
Chris leo hakuwa na siku nzuri lakini ni strike mzuri anajua kuituliza timu wakati anawangoja wenzake waje . Makosa ya leo ni sehemu ya mchezo .
Upekee wake ni kukaba tu tim inaposhambuliwa,,ila makosa yake ni yaleyale kila siku
 
Upekee wake ni kukaba tu tim inaposhambuliwa,,ila makosa yake ni yaleyale kila siku
Jamaa finishing mbovu sana. Kwa zile chance zake pale kwa kagere ana goal mbili.
Ila anajua kuwamudu mabeki ana control nzuri kuliko kagere mpira hapo ndipo una maajabu.
 
Back
Top Bottom