Paul Makonda
Member
- Jul 8, 2011
- 97
- 186
Uadui kwa taifa ni pamoja na kunyamaza wakati unajua ukimya wako unaangamiza wengi
Watanzania, Ni siku nyingine tena ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba taifa bado ni moja na lina umoja ule tunaoufurahia. Tunayo amani Upendo na Furaha si kwamba vitu hivyo vilishuka kama mvua, kuna watu walifanya kazi, wapo wanaofanya kazi na ili kuendela kuwa navyo sisi sote lazima tufanyie kazi. Uvumilivu wa kisiasa sitaha na ustahimilivu wa yale tunayoona ni maumivu kwetu na tusingependa tuyasikie ndivyo vinavyotufanya tuwe katika utendaji kazi utakaoendeleza tunu hizi za taifa. Si jambo jepesi kuwa na amani, umoja na mshikamano tulio nao. Ni vitu adhimu.
Wiki iliyopita niliandika kuhusu makosa kumi ya Msingi UKAWA wameyafanya kabla na baada ya kutoka nje ya Bunge. Kususia kwa bunge kumetengeneza makosa ya Msingi kwa kuwa yote waliyoyasema waliyasema ndani ya Bunge. Lakini kuna hoja ya kuyafanya makosa yao kuwa ni JINAI kwa sababu kwa wao kutoka nje ya bunge ama wanakwamisha mchakato wa katiba kwa makusudi ama wameamua kupotosha taifa. Wanalihalifu taifa kwa kuwa wanajiaminisha kuwa bila wao hakutakuwa na katiba. Wameshau kuwa kanuni zilizotengenezwa zinawezwa kurekebishwa na kuwezesha mchakato kuendelea bila wao. Uhalifu mkubwa utakuwa na umeonekana pale walipoamua kuanza kutumia maneno waliyyoyazungumza wakiwa na kinga bungeni huku hadharani.
ukomavu wa kisiasa umeonyeshwa na Mzee Edwin Mtei Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA kwa kuonyesha dhahiri kukerwa na kejeli zote dhidi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Huo ndio ukomavu kisiasa.
Demokrasia maana yake kuongea, nje ya mazungumzo hakuna Demokrasia. Mazungumzo ni kukaa na kukubali kusikiliza na kusikilizwa. Kama hauko tayrai kusikiliza, umezuia hata sauti yako kusikilizwa. Masharti ya kusikilizwa ni kusikiliza principally binadamu akiongea maneno matano anatakiwa asikilize kumi ndo maana akapewa mdomo mmoja masikio mawili, siyo urembo wa kichwa huo.
Tanzania tumesifika duniani kote kwa tunu ya amani na utulivu. Amani na utulivu wa tanzania ndiyo nguzo ya utahbiti wa Afrika. Tanzania ndiyo nchi pekee Afrika ambayo ilitengenezwa na waafrika wenyewe, nyingine zote zilitengenezwa na wakoloni tu. Jina Tanzania lenyewe ni la kipekee (exceptional).
Dunia nzima inaitazama Tanzania kama kitovu cha umoja na mshikamano wa Afrika. Na nguvu ya Afrika inaitegemea sana Tanzania tangu enzi za mataifa mengi kuwa Makoloni ya wazungu hata baada ya uhuru. Tanzania ilihusika kwa kiwango cha juu kabisa kwa ukombozi wa bara la Afrika na ikabaki kuwa ndiye mlinzi wa amani. Hadi sasa Tanzania imekuwa tegemeo kwa ajili ya vikosi vya Umoja wa Mataifa kulinda amani ya dunia kama kule Lebanon, Sudan kusini, Libya, Somalia, Ivory Coast, Siera Leone, Liberia, Msumbiji, Angola, Congo DRC na hata sasa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati Tanzania itategemewa sana.
Tanzania imekuwa Mpatanishi wa Migogoro mingi iliyoshindikana barani Afrika. Tuna wanadiplomasia waliofanya kazi zao kwa ustadi mkubwa kiasi cha kuifanya Tanzania iheshimike pote duniani. Rwanda na Burundi Arusha ndiko nyumbani kwao kwa Mapatanisho toka miaka ya 1990s. Na kwa jinsi hii, Arusha imekuwa kituo cha Upatanishi wa Afrika hata kuitwa GENEVA OF AFRIKA. Hii ni sifa ambayo Tanzania tunayo na haikuja ghafla au kushuka kama Mana au Mvua bali imetengenezwa.
Ikiwa Tanzania tumekuwa wapatanishi wa mataifa mengi Afrika, tumeshughulika na ulindaji amani ya dunia hii, tuna swali moja la kujiuliza, Je hao tuliowapatanisha au kuwalindia amani yao wanatupenda kutuona tukiwa na utulivu na amani hivi? Huko nje ya Tanzania na nje ya Afrika, wapo wanaouliza "Hivi Tanzania kuna nini; mataifa mengi ya kiafrika yamepalaganyika na kupigana wao kwa wao lakini imekuwa ngumu kutokea Tanzania kwa nini? Swali hili mtu akiuliza ama ana mantiki hii, Ni nini mataifa mengine yanaweza kujifunza kutoka Tanzania; ama ni mbinu gani wanatumia kuwa wamoja hivyo na ili waweze kufikisha chokochoko za kutusambaratisha wafanye nini. Kwa mantiki ya kwanza hakuna shaka hao wanalitakia mema bara la Afrika. Kwa mantiki ya Pili, wamegundua kuna ugumu wa kuisambaratisha Afrika yote kwa pamoja kama Tanzania bado ni Jamhuri ya Muungano inayodumu.
Maadui wa Tanzania wamegundua njia pekee ya kutusambaratisha Tanzania na Utanzania wetu, ni kutufanya tuusambaratishe Muungano. Nje ya Muungano Tanzania itasambaratika kuliko Sudan Kusini ama Somalia. Watanzania tuna nguvu sana ndani ya Muungano, nje ya Muungano ni kama mboga ya "Mrenda".
Maadui wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wamegundua kuwa hoja yoyote waliyowahi kuijenga kwingineko Afrika, hapa haifanyi kazi. Maana huko kwingine walifanikiwa tu kwa kujenga chuki miongoni wa watawala wa tabaka la juu na lile la chini, walipofika Tanzania wakakuta kuna ushirikiano na heshima kubwa kati ya matabaka hayo. Wakajaribu kutengeneza chuki miongoni mwa wananchi kwa itikadi zao za kisiasa, wamegundua hilo halifanyi kazi maana watanzania hawawezi kugombana kwa itikadi wakati wanaishi pamoja. Chokochoko za kidini nazo zimegonga mwamba. Wamegundua, lililo baki ni moja tu, nalo ni Muungano.
Wamegundua nje ya Muungano, hakuna nguvu maana nje ya Muungano hakuna Zanzibar, kuna Unguja na kuna Pemba. Nje ya Muungano kuna Wazanzibari ORIJINO na Wazanzibari AKADEMIA. Na ukifika hapo ni akzi rahisi kuwavuruga watanzania wa sasa kuliko wakiwa wamoja.
Namna pekee ya kufikia adhma ama njema ama mbaya, ni kupitia mchakato huu wa katiba. Niliwahi kusema "BAPHOON" ni Mtu asiyejali usalama wa nyumbani kwake bali anajali maslahi ya wanaomtuma kuharibu nyumbani kwake kwa Ujira mdogo. Neno hili Baphoon lilitumiaka sana Zimbabwe mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu, wazimbabwe wakilitumia kumuwakilisha Morgan Tshangirai ambaye alitumiaka kwa maslahi ya Wazungu kuiangamiza Zimbabwe. Uwezo wa wazimbabwe kuligundua hli walimdhihirishia katika kura, na eti matokeo ya Zimbabwe, yanayohusu Zimbabwe na Wazimbabwe Marekani wanasema si halali.
Wapo Baphoon Tanzania ambao wako tayari kupokea kitu chochote kutoka huko Magharibi ili waliangamize Taifa. Wamekuja na staili eti wanatetea katiba ya wananchi na wameamua kutetea nje ya uwanja halali wa kutetea. Wanataka wawainue wananchi wakasirike ili wakisha kasirika, basi kuwe na mfarakano utakaoyumbisha muungano. Na wakifanikiwa kwa hilo, basi Muungano utakuwa umefika ukingo wake. Zanzibar inatumika kama kichaka cha siasa za kidhalimu na wadhalimu. Mantiki iko wapi, ufanyie mkutano Dodoma ili ikitokea unaamua kurudi bungeni iwe karibu ama Zanzibar? Wapi karibu, Iramba kwa Tundu Lissu ama Zanzibar au kutoka Tabora kwa Lipumba ama Hai kwa Mbowe ama Zanzibar. Ipo namna.
Kauli zote za Wajumbe wa kundi la UKAWA wakiwa nje ya Bunge maalum la katiba hazitakuwa na maana yoyote maana mwisho wa siku rasimu ya katiba lazima kwanza itoke mle Bungeni kabla ya kwenda kwa wananchi ambao wao UKAWA wanadai wanawakilisha.
Ili Kuwa na mchakato ulio halali, haijalishi utakuwa na ugumu upi, mahali pekee pa kujadiliana kwa mahali tulipofikia na mchakato wetu ni bungeni Dodoma. Ratiba iko wazi tulianza kwa kutengeneza sheria ya mabadiliko ya Katiba, tukaunda tume, tukatengeneza mabaraza ya katiba, tukakusanya maoni na kuyapitia, tume ikatengeneza rasimu ya kwanza na yapili, tukaunda bunge maalum la katiba kwa mujibu wa sheria, bunge limekutana tukasiki maelezo ya tume na tume kazi yake imekwisha. Tukimaliza Bunge hili tunakwenda sasa kwenye kura ya maoni ambako sasa tutapiga kampeni tukishawishi wananchi ama wakubali ama wakatae hiyo rasimu ya Bunge. Na hiyo ndiyo itakuwa Katiba ya Wananchi. nje ya Mchakato huu hakuna Katiba
Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
makondapaul@gmail.com