Mdondoaji , kwanza nikupongeze kwa kuwa mkweli na mwaminifu. Kubadili mtazamo si jambo baya na wala haliwi. Kusimamia unachokiona ni sahihi kwa hoja ni ukomavu.
Na kuzungumza bila innuendos au insinuation za ukabila na udini ili ku-justify tu hoja ni jambo zuri.
Mitazamo tofauti si upungufu, kwa kingledha 'difference does'nt mean deficiency''
Ujerumani kutwaa Kombe. Nimefurahi sana. Imewachukua miaka zaidi 15 kutengeneza timu kwa euro million 9.
Watoto wa Argentina wanalia kwa kukosa ushindi, hawajazoea na wanajiuliza kwanini.
Watoto wa Tanzania wanawashangaa wa Argentina nini kinawaliza! Anyways nizirejee hoja zako kwa mafungu
Mdondoaji;10055579]Nguruvi,Nyerere ameyafanya na sio mazuri ila pia yana makovu ambayo hayawezi kuzibika...sio msingi wa kuendelea kungangania makovu yaliyopita
Alikuwa mwanadamu kama wengine.
Nilidhani muhimu ni kuwafundisha jamii mazuri aliyoyafanya na kumsamehe kwa makosa.
Kinyume chake jamii inafundishwa ubaya wa mazuri ya Nyerere.
Leo ukisema Nyerere znz unaambiwa 'laanatullah' hata wanaota meno.
Watu wamefundishwa kumchukia tu bila sababu, na wala hawaelezwi kuwa umoja wao una mchango wa Nyerere, na aliwapendelea zaidi ya watu wake, nashashangaa laantullah watu hao hao wanataka muungano wa laanatulah Nyerere.
Muungano unafaida na hasara kwa wazanzibari ila faida hizo zinaweza kuonekana kama jambo la mazoea na sio tunu kwa taifa. Pia zipo hasara hatukatai ikiwemo kutoheshimiwa kwa taifa la zanzibar, sintofahamu kwenye mapato ya zanzibar na mchango wa zanzibar katika benki kuu. Vyote vinahitaji kujadiliana na kuondoshwa,sio msingi wa kuuvunja umoja uliodumu muda mrefu.
Ni kwa msingi huu wengine tunataka taifa hilo liheshimiwe. Lipewe hadhi ya mambo kama kukopa, misaada, uwezo wa kupanga mipango yao bila kuingiliwa na kuondoka katika mambo 22 hadi 7 ili znz iwe na hadhi zaidi.
Hii ni pamoja na kupewa fungu lao la Benki kuu tofauti na sasa kupata aslimia 4.5(7%) pato la Tanganyika.
Mapato ya znz hakuna maana ni bilioni 400 tu, tunataka wapewe access za IMF ili tusituhumiane kuiba kischokuwepo. Mdondoaji, hivi unajiasikiaje ninikutuhumu umemuiba Matonya(marhum).Tunaotaka Tanganyika tunawatakia heshima
Tatu muungano wa Tanzania ni wa kindugu na kiukoo, Zanzibar kuna koo asili yake zimetokea Tabora wakati wa utumwa na biashara, zengine ni koo asili ya wamakonde hasa wapemba..... Hivyo asilimia kubwa ya wazanzibari wana ndugu zao Tanganyika na kuanzisha utengano sidhani ni jambo la busara.
Hii ni hoja dhaifu sana. Mwaka 1927 kulikuwa na uhusiano wa kisiasa bila muungano.
Uhusiano na msumbiji ni wa ndugu wa kimakonde, kiyao n.k. Pale Songea kuna watu wa Mbamba bay na Blantyre kwa Pande zote. Kigoma kuna watu wa Kalenzi n.k. Rwanda na Uganda, kuna watu wa pande zote, Mara, Arusha, Tanga-Mombasa kuna watu wa karibu wa undugu wa damu si kuoeleana. Kote huko hautuna muungano nako.
Naweza kusema Mombasa kwangu mimi pale mjasani nina ndugu zaidi ya Znz, lakini hatuna muungano.
Kuna watu wameoa America, Norway, Arhentina n.k. Kote huko hakuna muungano.
Ninachotaka uelewe hapa ni kuwa muungano si kwasababu ya undugu wa Damu na znz, kama unajenga hoja hiyo lazima uisimamishe kwa miguu kwa kuangalia factors nyingine na si hiyo unayosema.
Na pia, kuvunjika kwa muungano hakuna maana kuvunja kwa undugu.
Kwani undugu huo si umeanza miaka karne, mbona mwaka 1961 hadi 1964 hatukuwahi kuwakana wznz kama ndugu zetu. In fact tunawatambua watu wa visiwa vya FIJI kama watu warufiji, seuse znz. Hatuna muungano na fiji!!
Nne Zanzibar kuna matabaka yanayohasimiana muda mrefu tangia kipindi cha usultani , mapinduzi hadi sasa haya matabaka hayaaminiani hadi kesho na mfano halisi ni pale Bunge la Katiba lilipoanza watu wakaanza kuitana majina ya kibaguzi sasa imagine wakiwa huru watakuwa vipi?
Hilo ni tatizo lao kwasababu kwasasa adui yao mkubwa ni Tanganyika.
Adui Tanganyika anatakiwa akae pembeni na kuwapa nafasi wa-sort out matatizo yao.
Hii habari ya kutufanya sisi ni matatizo yao wakati hatufaidiki na lolote isipokuwa lawama sasa basi.
Kama wanataka heshima kamunavyosema wajiheshimu kwanza, hatuwezi kuwaheshimu kama hawajiheshimu.
Matatizo yao wayamalize wenyewe hatuna sababu za kutumia resource zetu kuingilia mambo yao.
Solution ya wazanzibari ni kuwa na Serikali moja tu au Dola Moja. Serikali moja inaweza kuja sasa au hata baadae baada ya muungano kuvunjika kwani thamani ya muungano itajulikana baadae. Kwani wazanzibari wakienda kuanzisha nchi yao na matatizo watakayokumbana nayo ndio watafahamu muungano una faida au hasara.
Vile vile Tanganyika wakiwa wamepakana na nchi isiyotulivu na wakakumbana na migogoro mbali mbali watatambua thamani ya kuungana na Zanzibar.
Usinitaje maana unataka 'kifo'.
Serikali moja ni haramu znz, hapo sipo.
Ninakubaliana nawe kuwa kwavile wznz wamekuwa wanafaidika na muungano bila kujua gharama zake, hawajui thamani yake. Huu ni ukweli. Nilidhani tunatakiwa tuwe na miaka 3 ya kutengana ili kila mmoja ajitahmini kama anaweza kuishi peke yake. Of course Tanganyika hahitaji kujitahmini kwasababu hamtegemei znz kwa lolote.
Baada ya miaka 3 wznz wangeweza kutanguliza ada za muungano tofauti na sasa wanapotanguliza favor.
Tanganyika mpaka wake na znz ni mzuri kuliko ule wa Rwanda, Burundi, DRC au Malawi.
Hakuna tatizo lolote wznz watakapokuwa na nchi yao. Hiyo haitatuathiri kwa lolote kwasababu hadi sasa bado tunachukua wznz wengie kuliko taifa lolote duniani.
Mpaka na znz ni mzuri sana, ni mdogo na una buffer zone. Hatutegemei kujuta kwa kuwa na jirani asiye na utulivu.
Ni bora jirani asiye na utulivu kuliko jirani anayeleta uchafuzi na kuharibu utulivu kwako. Tutawaambi wakae pamoja wasuluhishe matatizo yao, lakini hatutegemei kuwa kuwaacha wazungumze wenye kutaharabika jambo.
wa ufupi hatujui thamani ya mambo tuliyo nayo hadi tuyakose.
Ila Zanzibar huru sidhani kama ni busara wala serikali 3 kwani tukiyamaliza ya serikali mbili tutayaanza ya serikali tatu na kumbuka Serikali ya muungano wakati huo haitakuwa na mamlaka kama iliyonayo sasa
Serikali 2 hazina majibu na ndizo zimeifanya znz ikose heshima kwa mujibu wako. Ndizo zinawanyonya utajiri wa znz.
Ni makosa kusema S3 zina matatizo, hatujawahi kuwa na mfumo sheikh, kwanini mnaingia katika unajimu na kupiga ramli? Kwani S2 za ajabu maana hazieleweki, mimi naita 1.5 zilipatikana kwa mwongozo wa kitabu gani?
Sisi tunaotaka Tanganyika tunasababu zinazotjitosheleza
1. Mfumo uliopo unatishia muungano zaidi ya kuimarisha, ni wakati tufikirie mbadala
2. Tunataka fiscal autonomy kwa kila mmoja, Tanganyika isinyonye znz, na wala znz isiwe tegemezi kwa Tanganyika
3. Kuwe na uhuru unaozingatia tamaduni za sehemu ili kutoathiri historia na maisha ya watu
4. Kuleta stability ya nchi baada ya S2 kuleta instability kubwa
5. Kupunguza gharama za muungano kwa kupunguza mambo yanayoleta tabu, na kutoa uhuru wa washirika
6. Kudumisha undugu, ili kuepuka hasira za kuchoma watu.
Tukiwa na S3, wznz watajivunia uznz bila kuminywa au kinyongo.
Na wala Watanganyika hawatakuwa na kinyongo kama wasivyokuwa nacho na majirani wengine.
7. Sisi Watanganyika inatuuma tumebeba mzigo wa muungano wenyewe, mzigo usiothaminiwa na waznz hadi wanapohitaji msaada. Imefika mahali pa kudharau katiba yetu.
Tanganyika tumechoshwa na lawama za kunyonya znz, na tumechoka kutumia resource zetu kuisaidia znz ambayo wamekataa wao si Watanzania na si sehemu yetu ni nchi kamili ya jirani.
Tunahitaji kuamua hatima yetu na kupanga mipango yetu bila kwaingilia wzn wa nchi jirani na wao kutokutuingilia
Tunataka tuepuke mbegu ya ubaguzi inayopandwa kwa uwepo wa znz.
Mfano, WZNZ wakaitaka upendeleo wanatanguliza neno Uzanzibar na si utanzania. Kuanzia masomo hadi ajira na fursa nyingine. Hii mbegu mbaya hatuitaki ichanue, hauwezi kuwa na raia wa nchi jirani wakaja kupanga mipango na taratibu za nchi yetu.
Kibaya zaidi ubaguzi huo unafanywa dhidi ya wananchi wa nchi yetu katika nchi yetu kwa kutumia rasilimali zetu.
Mbegu ya Utanganyika imepandwa na wznz sasa inachanua, lazima wavune walichopanda. Hapa ni 3 tu sheikh.
Wao kwao sisi kwetu, nasema wao kwasababu wamekataa siyo sehemu ya sisi, wao ni waznz.
Kama hatutaweka mpaka wa znz na Tanganyika, wananchi wataweka mpaka, hapo sheikh itakuwa ni hatari kubwa sana!
Na hatari hiyo atalipia mkulima aliyepanda mbegu.
Salama tuwe na mambo machache, mengine kila mtu ajihudumie, sheikh hiyo ndiyo salama.
Watanganyika wameshajitambua!
watu hawataki kusikia ukweli huu, wznz sasa wanaangliwa tofauti kwasababu ya mbegu ya ubaguzi waliyopanda.
Na kwamba mbele ya safari kama hatutaweka mambo yakaeleweka, basi itakuwa ngumu sana kwao.Nasema wazi sina sababu za kuficha ficha. Mdondoaji niambie kama hakuna tension ya uznz na Utanganyika! ipo tena kubwa sana
Watu wanaogopa kusema, sisi tunasema tension iangaliwe, tusijifanye wajinga wa kusema tumeoleana n.k.