Nje ya Dharau na Nyodo zake za Kiasili, ila Kocha Mourinho ni Bonge la 'Genius' halafu anatupenda na kutujali mno Waafrika

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Jose Mourinho wants FIFA to stop African players from representing other countries other than that of their origin. He believes once this is done, Africa countries would start winning the World Cup.

Chanzo: Africa Archives

Binafsi huwa ninawapenda Watu wenye Dharau, Nyodo na Jeuri Kiasili, ila wakiwa ni 'very bright' halafu Wanajiamini pia.
 
Kuhusu mengine sijui ila nakubaliana na wewe. Watu wenye kiburi,jeuri na dharau wako smart sana.
 
Jamaaa hapindishi mambo ananyoosha mle mle. Anajua kusimamia kwenye ukweli. Hapo dunia ya leo haitaki wa kweli inataka wanafiki
 
Mimi kocha wangu bora kabisa ni Selemani Matola! Yaani siku zote akiletewa kocha mkuu kwenye timu, na yeye kuwa kocha msaidizi, basi lazima timu itasua sua kupata matokeo!

Ila akisimama yeye kama yeye sasa baada ya kocha mkuu kutimuliwa, timu inashinda kila mechi! Halafu hana jeuri, nyodo, dharau, wala kiburi! Yaani yuko tofauti kabisa na huyo Mourinho. Na anawapenda wachezaji wake mpaka raha.
 
Wakimpa timu yatatokea yale ya Man u na Ole sendeka
 
Mkuu lakini hapa issue ni mourinho
 
Jadili mada acha kutoka nje ya mada
 
Morinyo anapenda sana wachezaji weusi hasa namba tisa.
Drogba
Lukaku
Etoo
Pogba
Odoi
Wote wameshine akiwa. Kocha
 
Jadili mada acha kutoka nje ya mada
Sawa mkuu! Ngoja nirudi kwenye mada. Hakika Mourinho ni kocha jeuri, kiburi, na mwenye dharau sana.

Pia anawapenda sana wachezaji weusi kama Michael Essien, Didier Drogba, Tammy Abraham, na wengineo wengi.
 
Mkuu huyu mwamba anajua anacho kufanya
Ila je sie waafrica tupo tayari kubadilika
Mtu kuitwa national team mpaka utoe mlungula
ie mbappe alivyotoswa na Cameroon kisa tuu hakuwa na connection
Tatizo lenyewe waafrica hatuthamini vipaji...huku kwenyewe hamna academies za maana, kuchaguliwa mchezaji mpaka mzazi atoke hela.
Mara posho hazijalipwa, mara watu wanawekwa kwenye kambi mbovu basi shida tupu. Timu inaenda world cup eti president wa federation na familia yake wana fly first class huku wachezaji ambao ndio watendaji wanapandishwa economy. Sii ujinga huo.

Mpaka pale waafrica watakapo anza kuwathamini wachezaji wao ndio tutakapo kuwa na ndoto ya kushinda world cup.

Pele alitabirigi kuwa mpaka 2010 timu ya africa itakuwa imeshinda world cup kisa wana vipaji. Alisahau kua mis management, corruption na ubinafsi vingekuwa na mchango mkubwa katika kudidimiza mpira africa.
 
Sasa umeandika nini
 

Attachments

  • 20220623_152502.jpg
    50.7 KB · Views: 6
Inasikitisha nikama ile RT
Team ina wachezaji 3
Ujumbe wa team watu 15

Sasa hapo ndio utajua hatujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…