🤣🤣🤣🤣 Wanaenda kutalii tuu hawawajali wachezaji wenyewe.Inasikitisha nikama ile RT
Team ina wachezaji 3
Ujumbe wa team watu 15
Sasa hapo ndio utajua hatujui
Sie ata ukija angalia tuna natural resources kibao lakini management mbovu tunaishi kuchimbiwa vyoo na wamarekani. Waarabu wana mafuta tuu but ona mambo wanayoyafanya.
Mie ndio maana nawaangaliaga watu wanao mlamumu samatta kuwa hajitumi national team. Treatment unayopata ulaya na unayopata kwenye national teams za africa ni mbingu na ardhi.
Kuffo yule beki wa ghana alisemaga yeye kwenye afcon moja kwenye kambi ya ghana hadi maji ya kunywa ilikuwa mpaka washikane mashati. Ghana ilivyotolewa tuu, bayern munich wakatuma private jet ije imchukue awahi game ujerumani. Kafika kesho yake kapiga game na wakashinda na bonus akapewa juu. Sasa wee hapo niambia utajittuma kwenye klabu au kwenye national team?
Wenye mpira wao wanakwambia "it is an honor to play for ur national team, but its ur club that pays ur salary"
Ni fahari kuchezea timu ya taifa, lakini kumbuka klabu yako ndio inayokulipa mshahara