Nje ya lodge ni mazingira hatarishi kukaa!

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kuna vijana wa hovyo sana nchi hii. Utakuta mijitu imeweka kijiwe nje ya lodge/guest house inapiga stori zisizo na kichwa wala miguu.

Hivi nyie mmekosa mahali pa kwenda mpaka mje mkae hapo nje ya guest na kusababisha watu wanashindwa kutoka humo ndani. Si muende uwanjani au sehemu nyingine mkapigie hizo stori zenu?

Nje ya lodge ni mazingira hatari unaweza kuona vitu/watu ambao hukutakiwa kuwaona ikawa shida tena.

Naomba mjiheshimu
 
Fuata kilichokupeleka, ya nje achana nayo.
 
Acheni kupeleka wake za watu lodge za kiwaki😃
 
Sijui ni kwa nini ni rahisi kuingia humo ila kutoka ni kazi ngumu sana!
Mtu umeingia vizuri palikua na utulivu nje hakuna aliekuona. Unashangaa mda wa kutoka unakuta kundi la vijana wamekaa apo wanang'aa ng'aa mimacho tuu na hawaondoki! Inaudhi sana
 
Na hatutoki hapa leo utajuta
 
Ishi maisha yako broo,,achana na kuishi mawazoni kwa Wana itakua haina maana ya kuishi sasa!!!
 
Kipindi na balehe niliendaga kuulizia chumba Lodge nkamkuta bi mkubwa mmoja counter nilishindwa kuuliza bei nkageuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…