C-C Digital Pro
JF-Expert Member
- Mar 15, 2026
- 361
- 532
Msanii wa muziki kutoka Tanzania anaye ghani mashairi yake kwa lugha ya kiingereza pia ni fundi ujenzi wa majengo na mbunifu wa kutengeneza vifaa mbalimbali vya ujenzi, hujishughulisha na shughuli za ujenzi ambazo humusaidia kukamilisha mipango yake ya Sanaa ya muziki na maswala ya kiuandishi wa habari. Ujenzi ni KAZI nzito Sana na ngumu Sana lakini Civilian-Coin haoni ugumu wowote maana ameshazoea ugumu huo na anaendesha maisha yake kwa shughuli za ujenzi huku akiweka sawa mipango yake ya Sanaa ya muziki kwa kuinua mziki wake Kimataifa. Na ndio maana hata video za nyimbo zake zimepambwa kwa ubunifu wa majengo ya kisasa na ya kifahari kutokana na uzoefu wa ukandarasi katika ujenzi. Heko