Njegere nyama Wali

Njegere nyama Wali

Wali kivyake njegere kivyake nianze na hvyo kwanza nikijua taratibu nitamix vyote

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
Wali si unajua kupika?

Njegere zichemshe ziive
Andaa carrot, kitunguu, hoho, nazi na nyanya 1 tu..

Weka sufuria yako jikoni, weka mafuta yakipata moto weka kitunguu kikiwa cha kahawia ‘ usisubiri kiungue’ weka hoho koroga kidogo na uweke carrot, hii carrot utumie grater kuikwangua.
Then utawekamo nyanya 1 tu nayo ikwangue.
Then weka njegere.. subiri zichemke kdg kuivisha nyanya
Then weka tui lako la nazi
Viache vichemke
Tayari hapo.
 
Shukran sana kesho nitapika vitu vingi Nazi karoti hoho du
Nitaanza na kwa nyanya tu afu kesho nitakula pekee angu kikiwa kibichi nipate aibu mwenyewe nisije karibisha wana wakanicheka
Kwahyo njegere kwenye gasi nachemsha kwa Muda gani maximum

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
 
pole sana
Mrejesho nimeshindwa kupika ni aibu tu[emoji21][emoji22][emoji22]

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app

nyama njegere:

mahitaji:-
  1. nyama
  2. njegere
  3. nyanya
  4. vitunguu
  5. pilipili hoho
  6. karoti
  7. chumvi
  8. pilipili manga kidogo (sio lazima)
  9. kitunguu swaumu na tangawizi
  10. mafuta.
hatua za upishi:
  • kataka nyama yako osha kisha changanya kitunguu swaumu na tangawizi na pilipili manga chumvi then weka jikoni (usiweke maji had nyama yako ianza kuchemka)
  • osha njegere zako na uzichemshe kidogo tu ( kama dakika 5 hivi maana zinawai kuiva na zitaiva wakati wa kuunga nyama yako)
  • katakata nyanya zako vipande vidogo vidogo, kata karoti na hoho zako vipande vidogo vidogo.
  • nyama yako ikiiva itoe. bandika sufuri unayoitumia kuungia weka mafuta kiasi yakipata moto kaanga vitunguu vyako vikianza kuwa vya brown weka kitunguu swaumu na tangawizi (kidogo tu ) then weka nyanya zako. vipike kwa moto mdogo had ziive.
  • nyanya zikiiva weka nyama yako, karoti na njegere vichanganye vizuri then ongeza kidogo supu ya nyama then acha ichemke kama dakika 3 alaf uweke hoho zako (hoho zina wekwa mwishon ili zisiive sana zikapoteza radha) utaacha vichemke kwa mda kidogo(dakika 2-3 zinatosha)
  • unaweza ongeza supu kama utaona haikutoshi.
had hapo mboga yako ipo tayari kwa kuliwa.

WALI:
Mahitaji:
  • mchele
  • iliki
  • chumvi
  • kitunguu
  • karoti
  • mafuta
Jinsi ya kipika:
  • osha mchele wako.
  • bandika sufuria jikoni weka mafuta na kaanga vitunguu na karoti zako .
  • vitunguu vikibadirika rangi kidogo tu weka mchele wako na anza kuukaanga kwa kama nusu dakika weka chumvi then tia maji kiasi cha kuivisha dondoshea na iliki kiasi (punje 3-4 inategemea na wingi wa wali wako) then funika acha wali wako uive.
  • ukiiva unaweza zitoa iliki.
NB: sijaweka vipimo maana sijajua idadi ya walaji pia nivumilie mm sio mwandishi mzuri
 
pole sana

nyama njegere:
  1. mahitaji:-
  2. nyama
  3. njegere
  4. nyanya
  5. vitunguu
  6. pilipili hoho
  7. karoti
  8. chumvi
  9. pilipili manga kidogo (sio lazima)
  10. kitunguu swaumu na tangawizi
  11. mafuta.
hatua za upishi:
  • kataka nyama yako osha kisha changanya kitunguu swaumu na tangawizi na pilipili manga chumvi then weka jikoni (usiweke maji had nyama yako ianza kuchemka)
  • osha njegere zako na uzichemshe kidogo tu ( kama dakika 5 hivi maana zinawai kuiva na zitaiva wakati wa kuunga nyama yako)
  • katakata nyanya zako vipande vidogo vidogo, kata karoti na hoho zako vipande vidogo vidogo.
  • nyama yako ikiiva itoe. bandika sufuri unayoitumia kuungia weka mafuta kiasi yakipata moto kaanga vitunguu vyako vikianza kuwa vya brown weka kitunguu swaumu na tangawizi (kidogo tu ) then weka nyanya zako. vipike kwa moto mdogo had ziive.
  • nyanya zikiiva weka nyama yako, karoti na njegere vichanganye vizuri then ongeza kidogo supu ya nyama then acha ichemke kama dakika 3 alaf uweke hoho zako (hoho zina wekwa mwishon ili zisiive sana zikapoteza radha) utaacha vichemke kwa mda kidogo(dakika 2-3 zinatosha)
  • unaweza ongeza supu kama utaona haikutoshi.
had hapo mbona yako ipo tayari kwa kuliwa.

WALI:
Mahitaji:
  • mchele
  • iliki
  • chumvi
  • kitunguu
  • karoti
  • mafuta
Jinsi ya kipika:
  • osha mchele wako.
  • bandika sufuria jikoni weka mafuta na kaanga vitunguu na karoti zako .
  • vitunguu vikibadirika rangi kidogo tu weka mchele wako na anza kuukaanga kwa kama nusu dakika weka chumvi then tia maji kiasi cha kuivisha dondoshea na iliki kiasi (punje 3-4 inategemea na wingi wa wali wako) then funika acha wali wako uive.
  • ukiiva unaweza zitoa iliki.
NB: sijaweka vipimo maana sijajua idadi ya walaji pia nivumilie mm sio mwandishi mzuri
Upo vizuri
 
Back
Top Bottom