Njia 10 za kuondoa Stress na Uchovu kwa haraka

Njia 10 za kuondoa Stress na Uchovu kwa haraka

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1. Pitia picha zako zako za zamani kidogo, Picha za tukio moja wapo lililokufurahisha au za mtu mwingine yeyote wa karibu yako!

2. Fungua madirisha na kuruhusu mwanga na hewa kupita kwa kiasi kikubwa. Epuka kukaa sehemu yenye mwanga mdogo kwani hufanya hali yako ya uchovu au stress kuwa juu zaidi.

3. Imba huku unaoga! Sio lazima uwe muimbaji mahiri bali chagua tu wimbo wako unaoupenda, imba kwa namna yeyote huku ukiendelea kuoga.

4. Epuka kubaki mpweke. Tafuta mtu yeyote uongee nae (hata mtoto mdogo) itakusaidia kupunguza mawazo au uchovu.

5. Sikiliza muziki au mpigie simu rafiki yako mliyepotezana muda mrefu.

6. Fanya Mazoezi (japo kwa dakika moja)

7.Badilisha Mazingira, Mfano kama unapita njia hiyohiyo moja kutoka kazini/shule, badilisha na upite nyingine.

8. Fanya utafiti wa kijinga kwa kuwaangalia wapita njia na kutoa kasoro zao kimavazi, muonekano wao bila ya wao kujua.

9. Nenda Saluni kunyoa/kuosha/kusuka nywele zako.

10. Chukua kalamu na karatasi, anza kujifunza kuchora
 
Natamani ka likizo kama siku tano hivi, nikakae mbali sehemu yenye miti mingi niwe nasikiae ndege tu, pakiwa na maji pia itapendeza....niwe peke angu 😔
 
Nyingine 11. Socialize ktk group zako za Whatsapp/Telegram ya O-level, A-level au Chuo. Au Group zozote za rika moja lenye jokes, nk.. Chat sana, cheka sanaaaaa.
Kuna watu wana stress na wanaumia, huku wakiona aibu ku socialize ktk ma group. Punguza stress humo.
 
Stress nyengine hazitoki mpaka uzitatue wewe sasa ukute mtu anadaiwa vikoba huko ati aangalie picha wakati akikaa kidogo tu simu na meseji za vitisho zinaanza!.
Nikuulize mkuu hivi ulishawahi kuachwa na mdada mzurii anaejua kuifinyia kwa ndani halafu anakasauti fulani hivi ka kumtoa nyoka na mayai yake pangoni..?

Sasa uachwe na mdada wa namna hiyo utanyoa mara ngapi..? Mpaka mwenye saluni atakuchoka aanze kukukoa makwenzi ya kipara chako kilichokubuhu...😂
 
Natamani ka likizo kama siku tano hivi, nikakae mbali sehemu yenye miti mingi niwe nasikiae ndege tu, pakiwa na maji pia itapendeza....niwe peke angu 😔
Sasa ukiwa peke yako si ndio itazidi kujiumiza mamii?
 
Kama serikali ya bi tozo isingefunga websites za ngono huko pia palikuwa pahala pa kuondoa stress
 
Stress nyengine hazitoki mpaka uzitatue wewe sasa ukute mtu anadaiwa vikoba huko ati aangalie picha wakati akikaa kidogo tu simu na meseji za vitisho zinaanza!.
Nikuulize mkuu hivi ulishawahi kuachwa na mdada mzurii anaejua kuifinyia kwa ndani halafu anakasauti fulani hivi ka kumtoa nyoka na mayai yake pangoni..?

Sasa uachwe na mdada wa namna hiyo utanyoa mara ngapi..? Mpaka mwenye saluni atakuchoka aanze kukukoa makwenzi ya kipara chako kilichokubuhu...[emoji23]
Tafuta mwingine mzuri zaid yake .
 
Stress zangu naziondoa kwa ku lala nahakikisha nikitoka job straight home dk5 ya kucheza na watoto wasijione wapweke there after niusingizi mzito kuondoa stress tena usio na makelele naitaji utylivuuu
 
Natamani ka likizo kama siku tano hivi, nikakae mbali sehemu yenye miti mingi niwe nasikiae ndege tu, pakiwa na maji pia itapendeza....niwe peke angu 😔
Sio tena kuimba kwaya kumsifu yesu kristo
 
Back
Top Bottom