Chrix_Tz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 880
- 1,100
1. Weka bajeti
Ni rahisi kusikia watu wakilalamikia bajeti za serekali na kuzikosoa lakini wao wenyewe hawana bajeti zao binafsi. Unawezaje kukosoa bajeti ya serekali wakati ya kwako mwenyewe imekushinda? Fikiri tofauti; tambua umuhimu na jinsi ya kujiwekea bajeti. Bajeti yako binafsi itakuwezesha kufahamu mapato yako, mambo gani muhimu unayotakiwa kuyafanya na yatakugharimu kiasi gani cha pesa. Kwa kufanya hivi utaweza kutafuta na kutumia pesa kulingana na bajeti uliyojiwekea na kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu.
2. Panga manunuzi kabla
Ni muhimu kupanga manunuzi yako kabla ya kwenda sokoni au dukani. Hili litakuwezesha kubainisha nini unachotakiwa kununua na kwa gharama gani. Unapokwenda sokoni au dukani bila kupanga manunuzi yako ni rahisi ukanunua vitu ambavyo hukuvipanga. Unaweza kuorodhesha vitu katika kipande kidogo cha karatasi pamoja na bei zake ili uwe ni mwongozo wako katika manunuzi.
3. Weka vipaumbele
Kuna mahitaji mengi kwenye maisha ya mtu; lakini kuna yaliyo muhimu zaidi kuliko mengine. Jifunze kubainisha mambo ya muhimu zaidi ili uanze kuyatengea pesa kwanza. Kwa mfano maswala kama vile eilimu, uwekezaji, kodi ya nyumba, chakula, ni baadhi tu ya mambo muhimu kuliko gari, pombe, simu pamoja na mambo mengine ya anasa. Ukijifunza kuwa na mtazamo wa kutambua vipaumbele utaweza kutenga na kutumia pesa kwenye mambo ya muhimu kwanza.
4. Tumia kidogo kuliko unachopata
Ni rahisi kutumia kuliko kutafuta; hivyo si jambo la kustaajabisha ukajikuta unapata elfu tano kwa siku lakini unatumia elfu saba. Maana yake hapa unatengeneza deni mahali la shilingi elfu mbili kila siku. Inawezekana unakula akiba au faida katika kile unachokifanya. Jifunze kutumia kidogo kuliko kile unachokipata ili uweze kutunza pesa kwa ajili ya wakati wa uhitaji.
5. Tumia vitu (huduma) vyema
Kuna huduma kadha wa kadha tunazozihitaji kila siku katika maisha yetu kama vile maji, umeme, gesi, simu n.k. Mara nyingi watu hushindwa kutumia huduma au vitu hivi vyema na kujikuta wakijiongezea gharama za maisha zisizokuwa na sababu ya msingi. Mambo unayoweza kuzingatia katika swala hili:
6. Tafuta punguzo
Mara nyingi vitu huuzwa kwa punguzo, hivyo ni vyema ukanunua vitu kwa punguzo kuliko kununua kitu katika bei halisi ili kupuguza gharama. Naamini unafahamu kuwa yapo maduka yanayouza aina fulani ya shati kwa shilingi laki tatu, lakini shati hilo hilo linauzwa kwa shilingi elfu kumi na tano duka jingine. Sasa kwanini usinunue kwenye hili duka la pili linalouza shati kwa shilingi elfu kumi na tano? Epuka sifa na ufahari usiokuwa na sababu, tafuta na nunua vitu kwa punguzo ili kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu.
7. Linda afya yako
Kutokana na watu kutojali wala kufahamu umuhimu wa kuwa na afya njema, wengi wamekuwa wakitumia gharama zisizokuwa na sababu kwenye matibabu. Kuna hatua kadhaa unazoweza kuzitumia kujilinda na maradhi yasiyokuwa na sababu kama vile kula chakula bora pamoja na kuzingatia kanuni za afya kama vile usafi. Chukua hatua mapema ili usipoteze pesa zako hosipitalini kila siku kutibu maradhi ya tumbo au malaria ambayo ungeweza kuyazuia.
8. Acha tabia badhirifu
Kuna tabia kadha wa kadha ambazo watu wengi hawazijui kama ni moja kati ya tabia badhirifu. Tabia kama vile Kuvuta sigara, pombe, unywaji wa soda, ulaji wa pipi, kulipia michezo ya kompyuta, kukodisha filamu, kamari n.k ni baadhi tu ya tabia badhirifu. Unaweza kuepuka tabia hizi na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinapotea bila sababu.
9. Rekodi matumizi yako
Kwenye suala la kutunza kumbukumbu binafsi hasa za kipesa ni suala gumu kwa watu wengi. Lakini ni vyema ukajifuna kutunza kumbukumbu za matumizi yako ili hatimaye uweze kufahamu jinsi ulivyotumia kipato chako. Kwa kufanya hivi utaweza kubaini ni wapi ambapo hukutumia pesa zako vyema na utaweza kujirekebisha wakati mwingine.
10. Weka akiba
Mara ngingi watu hujitetea kuwa hawawezi kuweka akiba kwa kuwa hawana kipato kikubwa. Ukweli ni kuwa kuweka akiba siyo kuwa na kipato kikubwa bali ni maamuzi pekee. Fahamu kuwa kuna wakati chanzo chako cha kipato cha sasa kinaweza kukauka; hivyo kuwa na akiba kutakuwezesha kukidhi mahitaji yako kwa wakati ambao huna kipato cha uhakika au cha kutosha. Unaweza kufanya mambo yafuatayo:
Neno la mwisho: Pesa siyo kila kitu katika hii dunia, lakini ina nafasi kubwa sana. Hivyo ukitaka kuwa na utawala mzuri katika maisha yako ni vyema ukaimarisha misingi ya matumizi yako ya pesa. Epuka tabia za kitoto au za watu wasiokuwa na busara, ambao hula au kutumia kila wanachokipata. Naamini njia hizi 10 zilizoelezwa hapa zitakupa mwanzo mzuri wa matumizi ya pesa.
JAPO NI NDEFU ILA NADHANI WANA UCHUMI TUTAKUA PAMOJA HAPA.