Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Zab 94:18 SUV
[18] Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee BWANA, fadhili zako zilinitegemeza.
Fadhili za Mungu ni kubwa sana katika maisha ya mwanadamu, tunapozungumza fadhili za Mungu, ujue tunazungumza upendo wake kwetu na huruma zake, hatukustahili kabisa, lakini kwa upendo wake alimtoa mwanaye wa pekee kuja kutukomboa na kutupatanisha naye.
Inawezekana ulikuwa umesimama vizuri sana kwa Mungu, ikatokea siku ukaanguka katika dhambi, vile unavyojisikia ndani imekufanya uone aibu na kushindwa kurudi tena kwa Mungu.
Napenda nikumbushe fadhili za Mungu zilivyo kuu katika maisha yako, hupaswi kupoteza fursa hii kubwa katika maisha yako, unapaswa kuelewa na kuchukua hatua ya haraka kumwendea Mungu kwa toba.
Napenda nikupitishe katika njia chache alizonazo Mungu, njia hizi zitakusaidia kumwona Mungu kwa mtazamo mwingine mpya;
1. Kusamehe dhambi zetu. Mungu anasema kweli, hili likupe kuona kuwa dhambi zako zote zinaweza kusamehewa na Mungu, bila kujalisha watu walishakukatia tamaa na matendo yako maovu. Ipo nafasi ya kutubu na kuanza upya na BWANA, hii ni moja ya fadhili kubwa sana ya Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Isa 1:18 SUV
[18] Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
2. Kutiwa nguvu na moyo. Katika safari ya maisha haya inawezakana umefika mahali umechoka, umekata tamaa, umeona huwezi kusonga mbele tena, nakukumbusha kuwa yupo Mungu kukutegemeza na ukainuka tena. Mungu anaweza kukujaza nguvu zingine tena za kusonga mbele katika safari yako ya wokovu.
Isa 40:29-31 SUV
[29] Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. [30] Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; [31] bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Huenda ulivunjwa moyo na biashara uliyokuwa unaifanya baada ya kuingia kwenye hasara kubwa, yupo Mungu kukupa nguvu zingine za kusonga mbele katika maisha yako, yeye ndiye hutupa nguvu za kupata utajiri. Ule moyo wa biashara unaweza kurudi tena akishaingilia kati jambo lako.
Hupaswi kuendelea kubaki na hali uliyonayo katika maisha yako, yupo Yesu kukupa nguvu zingine za kusonga mbele, yeye ni mfariji wa kweli, yeye anaweza kutupa nguvu zingine za ndani kuliko mtu yeyote.
3. Kutimiziwa mahitaji yako. Tunaweza kupungukiwa mahitaji yetu, tunaweza kukosa baadhi ya mahitaji yetu muhimu, jambo ambalo linaweza kutusababisha tukavunjika moyo kabisa. Napenda nikuambie kwamba fadhili za Mungu ni kubwa mno kwetu, tukimwendea yeye anaweza kututimizia mahitaji yetu yote.
Flp 4:19 SUV
[19] Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Sisemi haya kwa kutania, nasema nikimaanisha, huenda ukapata wasiwasi kwa kumwona mpendwa mwingine akiwa anapitia hali ngumu. Napenda uone fadhili za Mungu katika maisha yako, vile Mungu anaweza kumtegemeza mtu yeyote anayemwamini yeye.
4. Kutupa ulinzi wa uhakika. Tunaweza kukutana na matisho mbalimbali ya adui, Mungu anapotutegemeza upya, tunakuwa na uhakika wa kulindwa. Hakuna adui ataweza kutugusa ikiwa ulinzi wa Mungu upo pamoja nasi, labda sisi wenyewe tushindwe kutulia kwa mashaka yetu na kukosa kwetu imani kwake.
Zab 121:7-8 SUV
[7] BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. [8] BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
Mwana wa Mungu anao ulinzi mkubwa sana, adui Shetani analijua hili ndio maana anapambana mchana na usiku kuhakikisha unaondoka kwenye ulinzi huu. Kuondoka kwako nI kufungua mlango wa kutenda mambo mabaya, mambo yaliyo machukizo mbele za MUNGU.
5. Tumaini la maisha ya umilele. Ukiwa unapigiwa kelele kila siku ishi maisha matakatifu, alafu ukawa huna tumaini lingine baada ya maisha haya, unaweza usiwe na ujasiri katika kuamini kwako. Lakini unapokuwa na uhakika baada ya maisha haya, yapo maisha mengine ya umilele pamoja na Bwana Yesu, inatupa nguvu tunapopoteza wapendwa wetu katika Bwana.
Zab 42:11 SUV
[11] Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Tunaamini baada ya maisha haya hapa dunia tunaenda kuketi na BWANA wetu, tumaini hili linaweza kutufanya tukatembea kifua mbele tukijua taabu yetu si bure hapa duniani.
Tukiwa tumemwamini Yesu hatuna mashaka, kupata kwetu mashaka ni kukosa maarifa sahihi au taarifa sahihi kuhusu Mungu, tukijua nafasi ya Mungu kwetu hatutavunjika mioyo yetu kirahisi.
Tunapoanguka katika safari yetu tuwe na tumaini BWANA anaweza kutuinua tena, hii itatusaidia tusikae muda mrefu katika hali ya kuonewa na adui katika maisha yetu.
Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kukusaidia kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.
Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana