plagiarism
Senior Member
- Jul 14, 2021
- 133
- 296
Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu za kila siku ili aweze kukidhi mahitaji yake. Baadhi ya shughuli hizo ni kilimo, biashara, uzalishaji(viwanda). Tanzania ni moja ya nchi iliyo ingia uchumi wa kati duniani lakini si sawa kuishia hapo lazima tuendele kupambania ili kufikia malengo makubwa zaidi. Uchumi wan chi hujengwa na shughuli za kibinadamu za kila siku, zifuatazo ni baadhi ya njia bora za kukuza uchumi wa Tanzania.
Kuboresha huduma za kijamii, kama vile hospital, maji na shule. Maeneo mengi nchini bado huduma za kijamii ziko chini sana hasa kwenye mashirika ya kiserikali usimamizi na matumizi ya kuboresha huduma hizi sio nzuri, hivyo basi serikali inabidi iweke mikakati mizuri ya kuboresha huduma hizi za kijamaa ili wananchi wake wafaidike na huduma hizo na kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, mfano hospital zikiboreshwa kutasaidia kupunguza idadi ya vifo watu kukosa tiba hupunguza uchumi kwa ujumla.
Ajira kwa vijana. Vijana ndio nguvu kazi hivyo kama kutakuwa na nafasi ya ajira kwao kutasaidia baadhi ya mambo kama mapato ya kodi, itasaidia kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja. Mfano TGSC 1 analipwa 410000 wakiwa 100 kodi ni 30% kwa mzawa. Hii itasaidia serikali kukusanya mapato mengi zaidi kama ajira zitakuwepo na kukuza uchumi zaidi. Lakini pia hata kutoa mafunzo wezeshi yatakayo wasaidia vijana kujifunza na kuweza kujiajiri wao wenyewe bila tegemezi kutoka serikalini.
Usimamizi bora kwenye matumizi ya pesa (ufisadi). Nchi ya Tanzania inahitaji wasimamizi wazuri ambao watakuwa kwa maslahi ya nchi na sio mtu binafsi. Mfano seriakali imetoa pesa kwa ajili ya kujenga kiwanda, hivyo inahitajika mtu huyo akasimamie kweli mali za umma kwamba kiasi kilicho tengwa kimetumika hivi na kama kuna kilicho baki kiweze kurudi ili kuboresha miundo mbinu mingine ya kukuza uchumi wetu.
Kuboresha miundo mbinu, kama vile barabara na mawasiliano. Kama nchi itaendelea kuboresha miundo mbinu yake haswa barabara na mawasiliano kutapelekea chachu ya maendeleo ya nchi kwa sababu kutarahisisha upatikanaji wa bidhaa kiurahisi mfano katika kipindi cha mvua tumeona maeneo mengi ya barabara kushindwa kupitika ambapo hupunguza kasi ya ukuaji uchumi tofauti na barabara ikiwa nzima.
Mikopo na punguzo la riba. Sekta zote hapa nchini zinatakiwa kutoa mikopo kwa watu (wanao anza au kuendelea na biashara) ili mitaji iwe rahisi kwao, lakini pia kwenye kurudisha mikopo hiyo inatakiwa riba iwe ya chini ili kumfanya mfanya biashara huyo kufanya kazi kwa umakini na kurudisha deni lake taratibu kutachochea ongezeko la uchumi kwa vijana wa Tanzania na kukuza nchi yetu kupitia mikopo
Uwekezaji. Ni njia sahihi ya kukuza uchumi wa nchi kama nchi itawekeza kata kada muhimu kama vile viwandani, usafirishaji, madini, biashara. Kama nchi itaamua kijikita katika uwekezaji hizo ni sehemu muhimu za kuwekeza ambazo zitasaidia katika uchumi wan chi kukua ambapo itapanua fursa na ajira pia kwa wananchi wake.
Mwisho, hizi ni baadhi ya njia muhimu za kufanya ili tuweze kufika mbali kiuchumi kama zitasimamiwa kwa umakini uchumi wa Tanzania utapanda na kujivunia kwa kufika mbali kihatua, wananchi tunatakiwa kuamka kila mtu apambane kwa kiasi chake kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa kupitia msaada wa serikali na sio kuilaumu.

Upvote
1