kelvin mpemba
New Member
- Jun 20, 2017
- 2
- 5
Ngoja nikuambie kitu kitakachokushangaza,siku moja nikiwa ninarudi nyumbani jioni,baada ya kumaliza shughuli zangu za kujenga taifa, nilimuona mzee mmoja akiuza matikiti maji kandokando ya barabara .Orodha ya bei yake ilisomeka tikiti maji1 kwa TSh. 3,000 na matikiti maji 3 kwa TSh.10,000. Kijana mmoja alipita na kununua matikiti maji matatu (3) moja baada ya jingine akilipa TSh.3,000 kwa kila mmoja.
Kijana huyo alipokuwa anaondoka, aligeuka na kusema kwa sauti kubwa licha ya kuwa na barakoa “Haya mzee, unafahamu nimenunua matikiti maji matatu kwa TSh.9,000 badala ya TSh.10,000?, inawezakana kuwa biashara si kitu chako”.Kwa mshangao wangu, mzee alitabasamu na kujisemea,”watu wanachekesha,kila mara wananunua matikiti maji matatu badala ya moja, lakini kunifundisha jinsi ya kufanya biashara”.
Ni kwa hakika kwamba wanadamu wana asili ya ubinafsi; haja ya kujijali na kuwa bora kuliko kila mtu mwingine, mzee alitumia maarifa haya kwa manufaa yake.Mzee huyu mfanyabiashara hana tofauti na watu wa magharibi ambao wanaitumia Afrika kama msingi wa ustawi wa nchi zao zilizoendelea na Afrika ikiwa na jukumu la kutekeleza kama mzalishaji wa malighafi aidha kijana yule hana tofauti na baadhi ya viongozi wa Afrika;siku zote tangu ukoloni kumekuwa na mipango na mikakati ya kuizuia Afrika isifanikiwe kupata ukuaji wa haraka wa viwanda na uzalishaji na hivyo kuweka ugumu kwa bara la Afrika kujikwamua kwenye shimo la umasikni.
Ninachoamini mimi ni kwamba misaada ya kigeni inayotolewa na nchi za Magharibi ni mbinu mojawapo ya kuidhoofisha hali ya uchumi wa nchi za Afrika.Fedha na silaha hutolewa ili kuweka mfumo wa utawala kandamizi wa Afrika madarakani. Inaaminika kwamba migogoro,ukosefu wa utulivu wa kisiasa,kuongezeka kwa madeni vita za kiraia na mapinduzi ya kijeshi amabayo yanatokea Afrika katika miongo mitano iliyopita yanatokana na misaada kutoka nje.Kwa kuongezea,viwango vya juu vya misaada kutoka nje vinaharibu ubora wa utawala na huzalisha mafisadi katika nchi, ambao hawana nia ya dhati ya kutumia fedha kwa ajili ya mageuzi au maendeleo ya jamii.Viongozi huelekeza misaada ya kigeni kwenye akaunti zao binafsi za benki.
Madeni na mikopo ya nje-Fedha inakopeshwa kwa nchi zinazozalisha malighafi ili waweze kuzidhibiti kwa kutumia masharti yanayoambatana na mikopo hiyo.Madeni makubwa ya nje yanatatiza maendeleo ya nchi hizi kwa sababu fedha hutolewa kwa riba kubwa na mara nyingi hazitumiki katika uwekezaji wa vitu muhimu kama vile miundombinu au matumizi ya kijamii
“Economic hitmen” Pia hutumwa kuwalaghai viongozi wa Afrika ambao wanakataa mikopo kwa kuwaonyesha trilioni za dola.Hawa wataalam mara nyingi wa Uchumi hushirikiana na mataifa makubwa kwa lengo la kunyonya rasili-mali zote za nchi masikini.Nchi nyingi za Afrika zinahitaji maendeleo ila hupungukiwa mtaji,vifaa vya teknolojia na wataalam na hivyo hujiweka katika mtego wa mikopo isiyo na unafuu.
Muundo wa ununuzi wa ukiritimba - Baadhi ya mataifa ya magharibi huamuaa ku-ungana na kuanza kununua malighafi wanayoyahitaji kutoka Afrika, wanaweka viwango wanavyohitaji katika bidhaa husika ili waweze kununua,lengo kuu ni kuweka udhibiti wa soko na kushusha bei ya bidhaa husika katika kiwango cha chini
Taasisi ya kimataifa ya kiuchumi-Nchi tajiri wameunda taasisi hizi ili waweze kudhibiti kwa uwazi nchi zinazoendelea kwa kuzifanya ziendelee kuwa tegemezi;hii ni kwa kuhamasisha nchi za Afrika kuendelea kutengeneza malighafi na pia kutengeneza matatizo katika urari wa malipo
Kupunguza uwezo wa kujitosheleza kwa chakula.Hii ilianzishwa wakati wa ukoloni na inaendelezwa na Benki ya dunia,kukiwa na udhibiti wa upatikanaji wa chakula kwenye nchi ni rahisi sana kuiendesha hiyo nchi.Mfano mzuri ni nchini Malawi ambao walikumbwa na balaa la njaa mnamo mwaka 2001.Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya utafiti ya Jubilee yenye makao yake nchini Uingereza,ambayo inahusiana na deni la kimataifa na fedha imeilaumu shirika la fedha la kimataifa(IMF) na Benki ya Dunia kwa kuweka shinikizo kwa Malawi kuuza tani 28,000 za mahindi kwenda Kenya na kusababisha njaa kubwa nchini humo mnamno mwezi Aprili-Mei 2001, kabla tu ya kushindwa kupata mavuno mengine,lengo ikiwa ni kupata fedha za kigeni na kuhudumia deni lake la dola milioni 13 inayodaiwa na IMF,inaendelea kuelezea kuwa,tangu wakati huo,nchi imekuwa ikikabiliwa na njaa,iliyosababishwa na upungufu wa kimkakati wa kilimo,kwani mahindi ndio chakula kikuu nchini Malawi, japo kuwa mwakilishi wa hazina nchini Malawi alikanusha shtaka hilo.”IMF ilishauri serikali kupunguza kiwango cha hifadhi ya nafaka lakini isiiuze”alisema Begashaw.
IMF sasa inapitisha pesa kwa Benki ya Dunia na EU,wafadhili wakuu wawili.”IMF haiwezi kufanywa mbuzi wa kafara kwa kila kitu. Ushauri wa kuuza mahindi ulitolewa na Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya,na ni makosa kulaumu IMF,” Horst Koehler,Mkurungenzi Mkuu wa IMF aliripotiwa akisema hayo.Maelezo haya yameleta mkanganyiko na kuacha mafumbo mengi juu ya nani alipaswa kulaumiwa: ila kwa akili za kawaida ni kwamba hizi taasisi zilikuwa na lengo baya.
Mfumo wa Mitaala mibovu ya elimu.Binafsi nilibahatika kupata elimu ya mambo ya Uchumi katika ngazi ya Secondary na Chuo kikuu,mitaala haribifu ya kimagharibi kama vile mafundisho ya faida linganishi (Comparative Advantage) ambayo lengo ni kutuaminisha kwamba hatima ya Afrika ni kuzalisha malighafi tu,kitu ambacho si kweli.Mtu anafaida ya kulinganisha katika kuzalisha kitu (comparative advantage) ikiwa anaweza kukitoa kwa gharama ya chini kuliko mtu mwingine,kuwa na faida ya kulinganisha(comparative advantage) haimanishi kwamba unakuwa bora katika jambo husika,mtu anaweza kuwa hana ujuzi wa kufanya kitu lakini bado akawa na faida ya kulinganisha katika kuzalisha bidhaa flani.
Na ili kutuchanganya zaidi wameunda modeli za kihesabu amabo wengi wetu hatuelewi lakini mwisho wa yote yanaonekana ni ya kisayansi na yanamanufaa kwa jamii husika.Kushindwa kwa hii mbinu ambayo hutumika na nchi za kiafrika,watu wa mgharibi hueguza kibao tena kwetu na kuleta suala la rushwa kwa viongozi na wananchi wa Afrika kuwa chanzo cha kushindwa kwa mbinu hii kufanikiwa,lakini wanasahau kwamba wao ndio chanzo kikubwa cha rushwa kupitia misaada wanayoitoa kwa nchi za Afrika.
Kwa maoni yangu Afrika inatakiwa itoke kwenye nadharia ya kutegemea kilimo tu,kigezo cha kuwa gharama ndogo hutumika katika uzlishaji inatakiwa ipuuzwe badala yake wawekeze katika kufanya utafiti wa mbinu bora za kuchakata malighafi zinazoptikana katika ardhi yetu kupata bidhaa bora na tuweze kujitegemea.
Ili kujenga uchumi wa kisasa na shirkishi,watunga sera wa Afrika wazingatie mabadiliko ya kiuchumi,kuweka wafanyakazi katika sekta ya juu kama viwanda na huduma; kuboresha sekta zenye tija ya chini kama kilimo, pamoja na kuongeza ukuaji wa viwanda na urekebishaji wa mitaala ya elimu.

Upvote
2